Filamu ya Royal Tour Ingezinduliwa Tanzania Badala ya Marekani kuepuka gharama

Filamu ya Royal Tour Ingezinduliwa Tanzania Badala ya Marekani kuepuka gharama

Tunaambiwa kwamba filamu ya Royal Tour yenye kupromote Utalii imegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni tisa. (9).

Leo tunaambiwa Rais ana safari ya kikazi yeye na delegation yake marekani na moja wapo ya mambo atayoyafanya ni kuzindua filamu ya Roya Tour.

Kwakua hizo kazi nyingine atazofanya hatujaambiwa ni zipi hivyo main task inakuwa ni Kuzindua filamu yake.

Ukiachana na matumizi ya Bilioni Tisa kwenye maandalizi ya filamu bado tunatumia tena mapesa mengine kwenye Uzinduzi na badala ya kuufanya hapa nyumbani tunaufanyia Marekani.

Matumizi ya mapesa haya yanafanyika kipindi tukiwa kwenye wave ya Corona maana tumeambiwa ipo na Vita Vya Ukraine.

Ukiachana na uwepo wa korona na vita ya Ukraine , Uchumi wetu umekumbwa na pigo la kupanda kwa bei za bidhaa muhimu jambo linaloongeza ukali wa Maisha kwa wananchi wa kawaida.

Inaleta ukakasi wa matumizi ya aina hii ya mapesa wakati Taifa likipitia kipindi kigumu namna hii.

Sijui viongozi wetu wanafikiria nini ila haipendezi kuzindua Filamu huko ughaibuni kwa mapesa mengi wakati kuna mtanzania hapa hata mlo wake tu unakua wa kuvizia na wakati juzi tu hapa Waziri Ummy anatuletea takwimu kwamba bado kuna idadi ya watanzania wanaojisaidia maporini(hawana vyoo)

Ningeiomba tu Serikali ijaribu kubana matumizi hasa kipindi hiki badala ya kuendelea kutumia fedha ambazo hatuna kwa mambo ambayo yanaonekana kabisa yasingefaa kufanyika kwa kipindi hiki.

Vile vile timing ya uzinduzi nayo sio nzuri maana jumuia za kimataifa zinahangaika na vita vya Urusi na Ukraine hivyo mwamko wa filamu hiyo utakua mdogo.

Wangesubiri mambo yatulie kidogo kama kweli tunataka kuipromote hiyo video.

Asanteni.

On top of that,

Uzinduzi unafanyika Marekani kuvutia watalii wakati Taifa la Marekani limekataza Raia wake kuja Tanzania kutokana na uwepo wa Korona.

View attachment 2186609

Watalii wapo USA wewe unataka ifunguliwe Dodoma? Jiulize Ndugai ndiyo wa kwenda kutalii !!
 
Wamarekani hawawezi kuja kwakua wanaisikiliza serikali yao iliyowaambia kuwa hapa Tanzania kuna Korona, Ugaidi na pia hatuzingatii haki za Mashoga.

Au huelewi kingereza.
Wamarekani wanaokuja hapa Tanzania ni wengi sana hasa blacks. Nenda bunju uone walivyochukua majumba ya kifahari.

Marehemu magufuli kupitia waziri wake wa mambo ya nje alitoa tamko kumpinga makonda kwamba serikali haihusiki kuzuia mashoga.
 
Watalii wapo USA wewe unataka ifunguliwe Dodoma? Jiulize Ndugai ndiyo wa kwenda kutalii !!
Screenshot_20220413-232427.png
 
Sijui viongozi wetu wanafikiria nini ila haipendezi kuzindua Filamu huko ughaibuni kwa mapesa mengi

Pesa inayowekwa mezani na makampuni makubwa ya KiMarekani ni nyingi mno na walengwa ni watu wa kipato cha juu Marekani ya Kaskazini. Channel kubwa kama Amazon Prime, Apple TV+, Disney n.k bajeti zao zinazidi pato la nchi masikini huku zikiwa zimedhamimiwa matangazo na kampuni kubwa zenye bajeti nono kuzidi nchi zinazoendelea.

Ubora wa vyombo vya uhakika vya mawasiliano TEHAMA mafundi kurusha matangazo bila chenga, wageni waalikwa wanaofahamika huko celebrity , social influencers Kaskazini ya dunia hii n.k n.k

Sababu ni nyingi itoshe kusema hizo tatu hapo juu zinatosha kuonesha kuwa tukio hili linafaa kufanyika huko Marekani kwa faida ya wadau wote ikiwemo Tanzania

Pia tofauti ya masaa sijui tukio hilo lingefanyika saa ngapi Tanzania ili wale walengwa potential tourist toka Marekani wangetizama tukio hilo muda gani.

"Tanzania : The Royal Tour" Premiering on public television stations across the U.S. beginning April 18th 2022

Tanzania: The Royal Tour, the latest in a series of global television events, hosted by Peter Greenberg with the President of Tanzania Samia Suluhu Hassan as his very special guide. An epic journey through this remarkable country through the eyes of its leader.

Source : Tanzania: The Royal Tour - Peter Greenberg Travel Detective
 
Pesa inayowekwa mezani na makampuni makubwa ya KiMarekani ni nyingi mno na walengwa ni watu wa kipato cha juu Marekani ya Kaskazini.

Pia tofauti ya masaa sijui tukio hilo lingefanyika saa ngapi Tanzania ili wale walengwa potential tourist toka Marekani wangetizama tukio hilo muda gani

Tanzania: The Royal Tour " on public television stations across the U.S. beginning April 18th 2022

Tanzania: The Royal Tour, the latest in a series of global television events, hosted by Peter Greenberg with the President of Tanzania Samia Suluhu Hassan as his very special guide. An epic journey through this remarkable country through the eyes of its leader. Premiering on public television stations across the U.S. beginning April 18th 2022

Source : Tanzania: The Royal Tour - Peter Greenberg Travel Detective

Screenshot_20220413-232427.png
 
Halafu katikati ya muda ambao attention ya watu ipo kwingine.

Nenda kampe support "mama".
Mimi niliitwa kwenda kuongea na Kikwete nyumbani kwa balozi, nikakataa.

Sitaki ujinga.
 
Hakukuwa na haja ya kucheza hii sinema kwanza , tungeweza kutangaza utalii kwa njia zingine tu.

Halafu unatangaz utalii huku unaleta kesi za abunuwasi kuwa kuna ugaidi Tanzania , kesi hii japo imefutwa ni doa kubwa .
 
Kikwete hajawahi kuacha kusafiri wala kubana matumizi.

Kivuli hufanana ma mwenye kivuli.

Hawa ni waumini wa "ILI ULE LAZIMA ULIWE" hivyo wanaamini ni lazima kulamba ASALI ili kupata ASALI!!!
 
Meanwhile Russia wanapambana hela yao isishuke thamani.Africa,Africa,Africa.
 
Mkuu inaonekana unapata tabu sana na mimi.

Nikushauri tu uniignore.

Kwakua huna mamlaka ya kunipangia cha kufanya zaidi sana utaendelea kuumia tu.

Nizoee au nipotezee.
Sasa wewe mbona unachojibu ni irrelevant? Ukisoma between the lines wewe ndio unapata tabu.
 
Meanwhile Russia wanapambana hela yao isishuke thamani.Africa,Africa,Africa.
Africa ni matumuzi yasiyokuwa na tija na tukitoka hapo mikopo na misaada.
 
Mama anataka watu wa system wale ili 2025 waone yeye bora abakie kuliko kuleta mtu wasiyemjua. Kiufupi anahonga kwa kutengeneza expenditures.
 
Tunaambiwa kwamba filamu ya Royal Tour yenye kupromote Utalii imegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni tisa. (9).

Leo tunaambiwa Rais ana safari ya kikazi yeye na delegation yake marekani na moja wapo ya mambo atayoyafanya ni kuzindua filamu ya Roya Tour.

Kwakua hizo kazi nyingine atazofanya hatujaambiwa ni zipi hivyo main task inakuwa ni Kuzindua filamu yake.

Ukiachana na matumizi ya Bilioni Tisa kwenye maandalizi ya filamu bado tunatumia tena mapesa mengine kwenye Uzinduzi na badala ya kuufanya hapa nyumbani tunaufanyia Marekani.

Matumizi ya mapesa haya yanafanyika kipindi tukiwa kwenye wave ya Corona maana tumeambiwa ipo na Vita Vya Ukraine.

Ukiachana na uwepo wa korona na vita ya Ukraine , Uchumi wetu umekumbwa na pigo la kupanda kwa bei za bidhaa muhimu jambo linaloongeza ukali wa Maisha kwa wananchi wa kawaida.

Inaleta ukakasi wa matumizi ya aina hii ya mapesa wakati Taifa likipitia kipindi kigumu namna hii.

Sijui viongozi wetu wanafikiria nini ila haipendezi kuzindua Filamu huko ughaibuni kwa mapesa mengi wakati kuna mtanzania hapa hata mlo wake tu unakua wa kuvizia na wakati juzi tu hapa Waziri Ummy anatuletea takwimu kwamba bado kuna idadi ya watanzania wanaojisaidia maporini(hawana vyoo)

Ningeiomba tu Serikali ijaribu kubana matumizi hasa kipindi hiki badala ya kuendelea kutumia fedha ambazo hatuna kwa mambo ambayo yanaonekana kabisa yasingefaa kufanyika kwa kipindi hiki.

Vile vile timing ya uzinduzi nayo sio nzuri maana jumuia za kimataifa zinahangaika na vita vya Urusi na Ukraine hivyo mwamko wa filamu hiyo utakua mdogo.

Wangesubiri mambo yatulie kidogo kama kweli tunataka kuipromote hiyo video.

Asanteni.

On top of that,

Uzinduzi unafanyika Marekani kuvutia watalii wakati Taifa la Marekani limekataza Raia wake kuja Tanzania kutokana na uwepo wa Korona.

View attachment 2186609
Naam, ingezinduliwa kwenye kitovu cha utalii, Chato.
 
Back
Top Bottom