Filamu ya wwz na mipango ya kupunguza idadi ya watu

Filamu ya wwz na mipango ya kupunguza idadi ya watu

Joined
Feb 28, 2014
Posts
69
Reaction score
87
a39ac0afc23209664b8aa1222eb8d12d.jpg
Jana usiku (juzi)niliipata filamu inayo kwenda kwa jina la ‘WORLD WAR Z’, jina WORLD WAR ndilo lililo nivutia kuitazama filamu yake, hasa nikitaka kujua ‘Z’ inasimama badala ya nini kwenye jina hilo. Baada ya kuimaliza kuitizama nilikuwa na machache ya kushea na wasomaji wa jamii forum kuhusiana na filamu yenyewe.

Lakini kwanza kabisa kabla ya kupena mawili matu ya filamu hii, kwanza tutambue nafasi na kazi ya Hollywood kwenye soko la filamu.
4cc7b70e695c883aaaa729320cd9ea46.jpg

Tangu Hollywood ianzishe sehemu kubwa ya zake imekuwa ni kuwarubuni mawazo ya watu, kutengeneza mawazo ya watu kukubaliana na kile wanacho kitaka.

Mathalani hakuna ushahidi wowote wenye mashiko unaothibitisha kuwa kuna viumbe wengine ‘huru’ kwenye uso wa dunia au nje ya dunia mbali na binadam na majini, lakini Hollywood wameweza kuurubuni watu kiasi kwamba kwa sasa inaaminika kuwa kuna viumbe wengine kutoka nje ya sayari hii, na kunayo uwezekano wa kuvamiwa na viumbe hao, lakini tunajua huu ni moja ya mipango kamambe ya Illuminanti ambao.

Duniani hatuna tatizo la ‘UGAIDI’ kwa maana ya UGAIDI, Lakini kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na Hollywood leo dunia nzima imekubali kuwa kuna tatizo la ugaidi na kama hatua za msingi hazitochukuliwa basi tatizo hilo litaiangamiza dunia (Hatua za msingi si nyingine bali sheria zilizo na utata na zilizo juu ya katiba ya nchi na zinazo pora uhuru na haki za msingi za wananchi)

cb14321ef1d500179ea759c8d625503f.jpg

Hivyo basi Hollywood hutumika kurubuni na kuandaa maamuzi na fikra za jamii kukubaliana na jambo fulani wanalo taka kulifanya, mara kadhaa imethibitika kwa Hollywood kutengeneza filamu zenye maudhui ya jambo fulani walilopanga kulifanya
01440258301b8096c329fd7ffdeec917.jpg

Mwaka 1954 kitabu kilicho kwenda kwa jina la ‘I Am Legend’ kilizinduliwa. Matukio katika kitabu hicho ni baina ya mwaka 1976 – 1979. Mwaka 1957 janga la mafua likaimeza dunia na chanjo ya polio ikaanza kutumika rasmi. Kipindi ambacho kimetumika kama muda wa maudhi ya kitabu yaani miaka minne ndicho kipindi kilicho chukua kuibuka kwa janga la mafua tangu kitabu hicho kiingie sokoni.

Filamu iliyo kwenda kwa jina la ‘The Last Man on Earth’ ya mwaka 1964, maudhui yake ni matukio yaliyo chezwa kutokea mwaka 1968. Mwaka 1967 baa la mafua liliikumba dunia.

Filamu nyingine ya aina kama hii ni ‘The Omega Man’ filamu hii ni ya mwaka 1971, lakini maudhui yake ni matukio ya mwaka 1977. Mwaka 1976 liliibuka janga la mafua ya nguruwe.

Filamu ya ‘I Am Legend’ ambayo ni ya mwaka 2007, maudhui yake ni baina ya mwaka 2009 – 2012. Dunia ilikumbwa na janga la HIN1.

3d289f350ce34d423fb5260c6317fbf8.jpg

Unaweza kwenda umbali wa ziada na kwakufanya tafiti binafsi, natumai utakuja na majibu mazuri zaidi.

5c6752cf2d1d4c233f8d7ab9026b5bbc.jpg

Hadithi ya ‘Worl War Z’ na matukio kwenye filamu hiyo yanaonesha kwamba Illuminanti wanayo aina fulani ya mpango mbaya dhidi yetu. Kama ‘Z’ kwenye filamu hiyo imesimama badala ya neno ZOMBIE, Hapana shaka hivyo ndivyo tunavyo onekana kwenye macho ya Illuminanti, kwamba ni watu duni, wabaya, tusio na bongo salama, na ambao inabidi tuangamizwe kwa namna yeyote ile inayo wezekana na kwa zana yeyote ile inayo patikana kukidhi lengo hilo kwa kiwango cha kidunia, ‘globaly’ na hapo ndipo unapo pata maana ya WWZ.
ea9d8bc2e59bae7a2b6c184d8a2b585f.jpg

Kwenye filamu hiyo zaidi ya watu bilioni 4, ‘wameathirika’ kutokana na virusi wabaya wanao badilisha maumbile ya binadamu na kama wanyama. Tetesi zipo na maandishi yapo kuwa Illuminanti wanao mpango wa kufuta asilimia 90 ya watu wote duniani, pekua mwenyewe utaona. WWZ inaonesha zaidi ya asilimia 80 ya binadamu wote wameathirika na hakuna kinga hivyo wanauwawa wote kwa namna yeyote ile iwezekanayo.

2aaec8e4a960411c9fb991b184842599.jpg

Nyota wa filamu hii ni Brad Pitt, ambaye amesha shiriki filamu zingine zenye jumbe mahususi za kimasonia kwa wanamasonia, na pia anatarajiwa kuowana na Angelina Joel ambaye ni mwanachama wa asasi ya siri ya CFR, asasi ambayo pia inamuandaa Brad Pitt kuwa mwanachama. Katika filamu Brad Pitt kama mtu aliyepata kuwa muajiriwa wa UN, anachukua nafasi ya kutafuta njia ya kuwaangamiza ‘zombi’ (kwenye neno zombi badilisha na weka neno ‘walimwengu’).

Kutakuwa na kambi ambazo zombi itabidi waingizwe kama mahala pa salama wakati tiba yao inaendelea kutafutwa, lakini itakuwa ndiyo machinjio yao, watakuwa wanauwawa humo.

Israel itaonekana kuwa ndiyo nchi inayo weza kupambana na zahama hilo kwa kuweka ukuta mkubwa ambao utawazuia zombi wasiingie, ambao wengi ni wapalestina na mamilioni wanaonekana kuuwawa wanapo upanda ukuta huo.

bc8ec59ef3d8e41ec540b1ca182fefe8.jpg

Kila kona kuna miili ya binadamu iliyo lundikana baada ya kuuwawa ilipogundulika ni waathirika.

Pakistani na Iran zinamalizana zenyewe kwa silaha zao za nyuklia, baada ya Iran kuzuia kwa kuwauwa wakimbizi ambao ni zombi wasiingie Iran kutokea Pakistan, hapa kwa maneno mengine tunaambiwa kuwa Iran wanazo sila za nyuklia.

Ni kama filamu hii, inatabiri yale yatakayo kuja kwenye kila kinacho fahamika saa za mwisho, na pia inawiana na mpango wa Illuminanti, hasa linapo kuja anguko la uchumi la kidunia, ambalo nalo litakuwa ni la kupangwa, na mabilioni ya watu kumwagika mitaani wakiwa hawana kitu nyumbani wala mifukoni, kwa vile Illuminanti kupitia mabenki yao wamewapora utajiri wao, watu hawa watakuwa ni shida mitaani, sheria za kutotembea mtaani zitapitishwa kama inavyo onekana mwanzoni kabisa kwenye filamu hii, lakini hilo halitasaidia na nguvu za kijeshi ndipo zitakapo tumika, nayo itakuwa ni mauwaji ya halaki kama inavyo onekana kwenye filamu ya WWZ.
d651111b06109dc2a717f7b132e0637d.jpg

Baada ya miaka 10 ya vita, dunia imebadilika, tiba ya zombi hakupatikana zaidi ya vifo vya halaiki na walimwengu wamebakia wateule wachache.

Filamu hii ni moja ya filamu zilizo tengenezwa kwa gharama kubwa mno, lakini kikubwa ikionesha burudani ya mabilioni ya watu wakiuwawa kwa halaiki. Ni kweli suala la kuuwa watu, mabilioni ya watu ni kitu cha kukihesabu kama aina ya burudani?

Unakumbuka kazi ya Hollywood? Filamu hii inaandaa akili za jamii na mawazo yao kusukumwa na nguvu hasi za kiukatili na mauwaji zaidi, kutuandaa kukubaliana na mipango ya Illuminanti hata kama itakuwa ni kuuwa mabilioni ya watu kwa sababu yeyote ile watakayo itaja kwenye vyombo vya habari.

Wakati wa utawala wa Rome, jamii ulidanganywa na mambo ya kipuuzi, kulikuwa na michezo mibovu na mibaya kwa jamii lakini yenye baraka za kiserikali, michezo hiyo ni kama ‘GLADIETOR’ Ambapo wafungwa waliingizwa kwenye ulingo wakapambana na kupigana mpaka kifo na wananchi walikaa majukwaani wakishangilia damu zikitiririka, Hollywood naona wanaturudishia utamaduni huo na ulimwengu umeonekana kuupenda sana.
ebfd4975b23b2cd64ca5cf56aa92254c.jpg

Leo hii tunatizama LIVE kwenye luninga taifa moja likimwaga damu za watu wasio na hatia za watu wa taifa jingine na tunaona yote hayo ni sawa tu.

Mauwaji ya halaiki tangu lini yakawa ni burudani kwa jamii?
 
Kupitia Hollywood umma umeaminishwa kwamba Uislamu ni dini mbaya ya kigaidi, kishetani, waumini wake wana roho mbaya, wakatili na wauaji wabaya kama wao hakuna, lakini hadithi ni tofauti kabisa na Waislamu wenyewe namna walivyo.

Hivyo basi Hollywood hutumika kurubuni na kuandaa maamuzi na fikra za umma kukubaliana na jambo fulani wanalo taka kulifanya, mara kadhaa imethibitika kwa Hollywood kutengeneza filamu zenye maudhui ya jambo fulani walilopanga kulifanya

[http://2]

Mwaka 1954 kitabu kilicho kwenda kwa jina la ‘I Am Legend’ kilizinduliwa. Matukio katika kitabu hicho ni baina ya mwaka 1976 – 1979. Mwaka 1957 janga la mafua likaimeza dunia na chanjo ya polio ikaanza kutumika rasmi. Kipindi ambacho kimetumika kama muda wa maudhi ya kitabu yaani miaka minne ndicho kipindi kilicho chukua kuibuka kwa janga la mafua tangu kitabu hicho kiingie sokoni.

Filamu iliyo kwenda kwa jina la ‘The Last Man on Earth’ ya mwaka 1964, maudhui yake ni matukio yaliyo chezwa kutokea mwaka 1968. Mwaka 1967 baa la mafua liliikumba dunia.

Filamu nyingine ya aina kama hii ni ‘The Omega Man’ filamu hii ni ya mwaka 1971, lakini maudhui yake ni matukio ya mwaka 1977. Mwaka 1976 liliibuka janga la mafua ya nguruwe.

Filamu ya ‘I Am Legend’ ambayo ni ya mwaka 2007, maudhui yake ni baina ya mwaka 2009 – 2012. Dunia ilikumbwa na janga la HIN1.

[http://4]

Unaweza kwenda umbali wa ziada na kwakufanya tafiti binafsi, natumai utakuja na majibu mazuri zaidi.

[http://1]

Hadithi ya ‘Worl War Z’ na matukio kwenye filamu hiyo yanaonesha kwamba Illuminanti wanayo aina fulani ya mpango mbaya dhidi yetu. Kama ‘Z’ kwenye filamu hiyo imesimama badala ya neno ZOMBIE, Hapana shaka hivyo ndivyo tunavyo onekana kwenye macho ya Illuminanti, kwamba ni watu duni, wabaya, tusio na bongo salama, na ambao inabidi tuangamizwe kwa namna yeyote ile inayo wezekana na kwa zana yeyote ile inayo patikana kukidhi lengo hilo kwa kiwango cha kidunia, ‘globaly’ na hapo ndipo unapo pata maana ya WWZ.

[http://1]

Kwenye filamu hiyo zaidi ya watu bilioni 4, ‘wameathirika’ kutokana na virusi wabaya wanao badilisha maumbile ya binadamu na kama wanyama. Tetesi zipo na maandishi yapo kuwa Illuminanti wanao mpango wa kufuta asilimia 90 ya watu wote duniani, pekua mwenyewe utaona. WWZ inaonesha zaidi ya asilimia 80 ya binadamu wote wameathirika na hakuna kinga hivyo wanauwawa wote kwa namna yeyote ile iwezekanayo.

[http://4]

Nyota wa filamu hii ni Brad Pitt, ambaye amesha shiriki filamu zingine zenye jumbe mahususi za kimasonia kwa wanamasonia, na pia anatarajiwa kuowana na Angelina Joel ambaye ni mwanachama wa asasi ya siri ya CFR, asasi ambayo pia inamuandaa Brad Pitt kuwa mwanachama. Katika filamu Brad Pitt kama mtu aliyepata kuwa muajiriwa wa UN, anachukua nafasi ya kutafuta njia ya kuwaangamiza ‘zombi’ (kwenye neno zombi badilisha na weka neno ‘walimwengu’).

Kutakuwa na kambi ambazo zombi itabidi waingizwe kama mahala pa salama wakati tiba yao inaendelea kutafutwa, lakini itakuwa ndiyo machinjio yao, watakuwa wanauwawa humo.

Israel itaonekana kuwa ndiyo nchi inayo weza kupambana na zahama hilo kwa kuweka ukuta mkubwa ambao utawazuia zombi wasiingie, ambao wengi ni wapalestina na mamilioni wanaonekana kuuwawa wanapo upanda ukuta huo.

[http://3]

Kila kona kuna miili ya binadamu iliyo lundikana baada ya kuuwawa ilipogundulika ni waathirika.

Pakistani na Iran zinamalizana zenyewe kwa silaha zao za nyuklia, baada ya Iran kuzuia kwa kuwauwa wakimbizi ambao ni zombi wasiingie Iran kutokea Pakistan, hapa kwa maneno mengine tunaambiwa kuwa Iran wanazo sila za nyuklia.

Ni kama filamu hii, inatabiri yale yatakayo kuja kwenye kila kinacho fahamika saa za mwisho, na pia inawiana na mpango wa Illuminanti, hasa linapo kuja anguko la uchumi la kidunia, ambalo nalo litakuwa ni la kupangwa, na mabilioni ya watu kumwagika mitaani wakiwa hawana kitu nyumbani wala mifukoni, kwa vile Illuminanti kupitia mabenki yao wamewapora utajiri wao, watu hawa watakuwa ni shida mitaani, sheria za kutotembea mtaani zitapitishwa kama inavyo onekana mwanzoni kabisa kwenye filamu hii, lakini hilo halitasaidia na nguvu za kijeshi ndipo zitakapo tumika, nayo itakuwa ni mauwaji ya halaki kama inavyo onekana kwenye filamu ya WWZ.

[http://1]

Baada ya miaka 10 ya vita, dunia imebadilika, tiba ya zombi hakupatikana zaidi ya vifo vya halaiki na walimwengu wamebakia wateule wachache.

Filamu hii ni moja ya filamu zilizo tengenezwa kwa gharama kubwa mno, lakini kikubwa ikionesha burudani ya mabilioni ya watu wakiuwawa kwa halaiki. Ni kweli suala la kuuwa watu, mabilioni ya watu ni kitu cha kukihesabu kama aina ya burudani?

Unakumbuka kazi ya Hollywood? Filamu hii inaandaa akili za umma na mawazo yao kusukumwa na nguvu hasi za kiukatili na mauwaji zaidi, kutuandaa kukubaliana na mipango ya Illuminanti hata kama itakuwa ni kuuwa mabilioni ya watu kwa sababu yeyote ile watakayo itaja kwenye vyombo vya habari.

Wakati wa utawala wa Rome, umma ulidanganywa na mambo ya kipuuzi, kulikuwa na michezo mibovu na mibaya kwa umma lakini yenye baraka za kiserikali, michezo hiyo ni kama ‘GLADIETOR’ Ambapo wafungwa waliingizwa kwenye ulingo wakapambana na kupigana mpaka kifo na wananchi walikaa majukwaani wakishangilia damu zikitiririka, Hollywood naona wanaturudishia utamaduni huo na ulimwengu umeonekana kuupenda sana.

[http://3]

Leo hii tunatizama LIVE kwenye luninga taifa moja likimwaga damu za watu wasio na hatia za watu wa taifa jingine na tunaona yote hayo ni sawa tu.

Mauwaji ya halaiki tangu lini yakawa ni burudani kwa uma?

[http://3]
Mm naomba unajua misimamo na Sheria za dini ya Kiislamu..?
Ilienezwaje...?
Adhabu zake..?
Je yale yanayotendeka kule Saudia ni uongo (rejea uzi wa The bold kuhusu kuchinjana)
Bokko haram je wale mabinti 200 ni uongo..?
Al shabab somalia west gate tunadanganywaa..?

Aksante..
 
Kwa namna yoyote uwezikuwa na ushirikiano na majini usiwe gaidi kwa namna moja au nyingine,
na auwezi kusema ugaidi haupo kama wewe si gaidi.
 
kama si mchonozi wa mambo fulani fulani yanayoendelea duniani, kamwe hutajua kipi kinaendelea. Mfano hata muvi za matrix kuna ujumbe uko ndani yake, series za katuni za 'the simpson' kuna mambo mengi ni kama yalitabiliwa na yametokea na mengine bado yanatabiliwa na huenda yakatokea. mfano. nenda 'youtube' andika 'the things the simpsons predicted' kisha search, jibu utalipata

M
 
Kuna movie inaitwa looper ya bluce wills, niliiangalia kwa umakin ile movie nkagundua ina malengo maalumu. Et kuna watu wachache matajir wanamilik umri wa watu, yaan unapozaliwa unapewa miaka walau 18 ya kuish, then mingne inabdi ufight na kununua kwa hao matajir. Ni kupambana tu ili kupata miaka il uish, watu wanauziana kama njugu sekunde, dk, masaa, siku. wiki na miakag. Kuna mitambo maalumu na kifaa unafungwa mkonon ndo unatumia kununua umri wa kuish. Na umr wako ukiisha unakauka kau, maskn wamehustle sana mule ndan
 
Mm naomba unajua misimamo na Sheria za dini ya Kiislamu..?
Ilienezwaje...?
Adhabu zake..?
Je yale yanayotendeka kule Saudia ni uongo (rejea uzi wa The bold kuhusu kuchinjana)
Bokko haram je wale mabinti 200 ni uongo..?
Al shabab somalia west gate tunadanganywaa..?

Aksante..

kwanza tambua SAUDI ARABIA si dora ya kiisram bali ni dora ya kifalme
hivyo sheria zinazosimamiwa ni za kifalme fahamu hilo kwanza
Dora ya kiisram ni nini ?
ni mfumo kamiri wa maisha ya MUISLAM tangu tumboni kwa mama yake mpaka siku ya mwisho ya uhai wake ambapo huongozwa namna ya kuishi kwa SHARIA na TARATIBU za kiislam kwa kufuata QURANI na SUNNA za Mtume na naswahaba wake

piri kuhusu boko kharamu na alshababu
labda ujue kwa undani JIHAD ni nini katika UISRAM
unaposema JIHAD unamaana kujituma zaidi au kujitolea
na unapozungumzia JIHADI katika UISLAM inamaaka kujituma zaidi na kujitolea zaidi kwa ajiri ya DINI malipo ikiwa ni kwa MUNGU
hivyo JIHADI ya kwanza kabisa inaanza nafsi mwako ukiweza kushida JIHAD ya nafsi yako basi inafatia wanaokuzunguka famiria yako na ndugu zako

Ili uweze kupigana JIHADI kama hivyo wanayojinasibu hao Boko khalamu na alshabab Shart uwe MJAHIDINA
sasa ni nini JIHAD na nani MUJAHIDINA ?
ni muumini anayefanya juhudi(JIHAD) katika njia ya Allah, kwa mali yake nafsi yake na muda wake

Jihad inapigwana wapi na kina nani na wakati gani ?

kwanza tambua
UISLAMU si dini ya mabavu
Uislamu unajali zaidi hoja na siyo nguvu
Unamtaka mwanadamu atumie akili yake katika kumtambua Muumba wake.
na Ndiyo maana katika Qur’an haimlazimishi mtu kumkubali Mwenyezi Mungu bali inamtaka binadamu atumie akili na kuzingatia
Qur’an inasema:
"Je! Hawatazami ngamia jinsi walivyoumbwa? Na mbingu jinsi zilivyoinuliwa. Na milima jinsi ilivyothubutishwa. Na ardhi jinsi ilivyotandazwa?" (Al- Ghashiyah 88:17-20).

hapa MWENYEZIMUNGU anawataka wanaadamu(wakrsto kwa waislamu) watazame umbo la ngamia, mbingu, majabali na ardhi, kisha watumie akili zao kupima ili waone kama vyote hivyo vimekuja vyenyewe hivi hivi au yuko aliyeviumba?
Kisha MWENYEZIMUNGU akamwambia Mtume wake:
"Basi kumbusha, hakika wewe ni mkumbushaji (tu). Wewe si mwenye kuwatenza nguvu’. (Al-Ghashiyah 88:21-22)

sasa hapo Unaona Uislamu umeilenga zaidi akili ya mwanadamu. Mwanadamu amekuwa ni kiumbe bora kuliko mnyama kwa sababu ya akili aliyo nayo. Binadamu asiye na akili hatofautiani na mnyama. Mwenye akili hupima kila analoambiwa. Akiliona linakubaliana na akili analikubali na akigundua halikubaliani na akili, basi naye hulikataa. Na Uislamu ndivyo ulivyo. Hoja zake zinachuana na akili ya binadamu. Kama akili inakataa kukubali kuwa 1 + 1 + 1 ni 3, kwanini basi akili itaabishwe kwa kupewa jawabu isiyoridhia na ya uwongo?

Na vipi Muislamu atakashifu dini nyingine na wakati Uislamu wenyewe unakataza kufanya hivyo
unaweza ukashangaa unakataza kukashifu je ni vipi wale wanaojinasibu kuchinja watu kwa kigezo cha JIHADI na kuwaita makafiri wakati kumbe hata kukashifu dini nyingne kwa lugha kali UISLAM unakataza !!?
ni some kwa umakini utanielewa

Qur’an Tukufu inasema:
"Wala msiwatukane wale ambao wanaabudu, kinyume cha MWENYEZIMUNGU wasije wakamtukana MWENYEZIMUNGU kwa jeuri zao bila kujua". (Al An-Am 6:108).

Na kutokana na aya hiyo hapo juu MWENYEZIMUNGU alimwagiza
Mtume muhammad kwa kumwambia
"Waite (watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora (siyo kwa kuwatukana wao au kutukana dini zao)". (An Nahl 16:125).

Mtume (saw) akafuata maagizo ya Mola wake. Kwa miaka 13 mfululizo aliwalingania watu wa Makka kwa maneno mema, hekima na busara. Katu hakuwatukana wala kutumia nguvu. Kinyume chake yeye na wafuasi wake ndio waliokuwa wakitukanwa kunyanyaswa na kuteswa.

Na kila mara katika kulingania akijibiwa hovyo au kukashfiwa
MWENYEZIMUNGU alimwambia,
"Basi wasamehe na uwaambie (maneno mazuri) ya salama (labda mwisho wake watatambua). Hivi karibuni watajua". (Az-Zukhruf 43:89).

Na pale alipofanyiwa uovu mkubwa aliambiwa,
"Ondosha mabaya (unayofanyiwa) kwa (kulipa) mema". (Al Muuminun 23:96).

ni kama wewe ulipouliza hapo juu inakuwaje BOKO KHALAM kufanya yale yanayofanya hali kadhalika AL SHABAB kila siku kuua watu wasio na hatia
kisha nije na nahau nilizozipangilia vema kuwa Uislamu ni dini ya amani, na jihadi siyo vita na ilihali Waislamu kila uchao w wanapigana vita vya jihadi?

Vita hupiganwa kwa malengo mawili makuu. Aidha kwa kupigania maslahi ya kidunia, kama kutaka kuziteka na kuzitawala nchi nyingine, kupata mali ghafi au masoko ya kuuzia bidhaa ardh nk
au pia vita vinaweza kupiganwa kwa ajili ya kujilinda na mashambulizi ya adui.

Kwa vyovyote vile vita hivyo viwili havifanani. Vile vya aina ya kwanza ni vya uchokozi na vile vya pili ni vya kujihami
Uislamu unaviita vile vita vya uchokozi "Harbun" na vile vya kujihami "Jihadun

Ilitarajiwa Waislamu wafanye nini baada ya kudhulumiwa uhuru wa kuabudu na kufukuzwa katika nchi yao kuporwa ardhi yao na wengine kuuawa

Bila shaka hiyo ni jeuri iliyopindukia na hakuna atakayeivumilia. Ndipo hapo Mwenyezi Mungu (sw) akawapa Waislamu ruhusa ya kupigana. Ruhusa ya kwanza waliyopewa ilikuwa

"Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa. Na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwasaidia ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki ila kwa sababu wanasema ‘Mola wetu ni Allah’ (Al Hajj 22:39-40)

Huo ukawa ndio mwanzo wa vita vya jihadi. Lakini msisitizo mkubwa waliowekewa ulikuwa wasipigane vita vya uvamizi bali vita vya kujihami. Na shahidi wa haya ni ile kauli ya Allah(sw) inayosema
"Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msipindukie mipaka (mkawapiga wasiowapigeni). Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi warukao mipaka" (Al Baqarah 2:190).

rejea mikasa ya MYNMAR waislamu wa ROHNGYA na PARESTINA wanavyofanyiwa na ISRAEL then linganisha na SYRIA SOMARIA na huko NIGERIA na baadhi ya NCHI nyingne wanavyopigana kwa Chuki USUNNI na USHIA
then tumia akili yako kung'amua lipi ni lipi wapi sahihi wapi UZUSHI

MKUU uislamu ni DINI nzuri sana yenye MUONGOZO thabiti kwa walioamini
na si propaganda za mitaani ukitaka kuujua UBORA na UZURI wa UISRAMU ujifunze kwa undani

mwisho nakuongezea kukufuta mawazo mabaya kuhusu UISLAM kama ulikuwa hujui jua sasa sisi WAISLAM tunampenda YESU na Tunaamini atarudi kama MKOMBOZI kama tulivyobainishiwa
Ila sisi tunamuita NABII ISSA bin MARIAM
 
Ok you might have a point. Ngoja niingie kwenye observation yangu ndogo tu na kung'amua mambo mawili matatu yanayohusu mind tuning kuhusiana na hiyo movie perhaps sikatai kama hollywood hiyo ndo kazi yao
 
Mm naomba unajua misimamo na Sheria za dini ya Kiislamu..?
Ilienezwaje...?
Adhabu zake..?
Je yale yanayotendeka kule Saudia ni uongo (rejea uzi wa The bold kuhusu kuchinjana)
Bokko haram je wale mabinti 200 ni uongo..?
Al shabab somalia west gate tunadanganywaa..?

Aksante..
soma uongeze maarifa rejea kwenye story za bold who's a bold soma vitabu vya dini sio story za kusimuliwa neutral ila unapocoment simulia unachofaham sio unachosikia tuendelee kujifunza
 
Kuna movie inaitwa looper ya bluce wills, niliiangalia kwa umakin ile movie nkagundua ina malengo maalumu. Et kuna watu wachache matajir wanamilik umri wa watu, yaan unapozaliwa unapewa miaka walau 18 ya kuish, then mingne inabdi ufight na kununua kwa hao matajir. Ni kupambana tu ili kupata miaka il uish, watu wanauziana kama njugu sekunde, dk, masaa, siku. wiki na miakag. Kuna mitambo maalumu na kifaa unafungwa mkonon ndo unatumia kununua umri wa kuish. Na umr wako ukiisha unakauka kau, maskn wamehustle sana mule ndan
co time ya Justin timberlake
 
Asante kwa Uzi mzuri mkuuuuuu.

Apa ndo nmepata picha ,,nikwann Màrekan imeanza kufanyia uchunguzi Vina Saba vya warusi.....nakwann Putin ametoa Onyo kwawanchi wake juuu yahuo mchezo!!!!.

Asante sana .
 
Back
Top Bottom