Filikunjombe ni jembe

Deo Filikunjombe ni sawa na wabunge 900 wa CCM na ni sawa na wabunge 11,900 wa CCM wenye vichwa kama vya Lusinde au Komba.
 
Filikujombe, Kangi Lugola na Esther Bulaya ni majembe yaliyopo ccm kwa bahati mbaya
 
Filikujombe, Kangi Lugola na Esther Bulaya ni majembe yaliyopo ccm kwa bahati mbaya

Naamini mambo mengine yanayofanywa na hao wanaojiita WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA yanabeba maudhui yasiyotambuliwa wala kueleweka mbele ya jamii nzima ya Watanzania. Kubwa kwa walio wengi ndani ya bunge hilo ni kuhakikisha wanapata posho kubwa kwa namna yoyote iwayo kwa faida na masilahi ya watawala wachache na marafiki zao.

Katika hali kama hiyo nachelea kusema siku za usoni tutashuhudia watu wachache waliojenga heshima kubwa mbele ya jamii wakidharauliwa, kupuuzwa na kuonekana watu wasio na maana yoyote mbele ya jamii kwa kuingizwa kwao kama wajumbe wa bunge hilo ambalo limenajisiwa na kukosa uhalali wa kuitwa BUNGE MAALUM LA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Kwa hali halisi ilivyo sasa na kwa wale wanaopenda heshima yao iendelee kutamalaki mbele ya umma wa Watanzania ni kujiondoa mapema kutoka kwenye huo mchakato dhalili ili siku za usoni wasije wakasutwa na kudhihakiwa kuwa kwao WALIONA POSHO NI MUHIMU ZAIDI YA MUSTAKABALI MWEMA KWA UMMA WA WATANZANIA.

Niseme tu kuwa ndani ya bunge hilo kuna wanazuoni waadilifu, viongozi wa dini, wanasiasa na wanaharakati waliojijengea heshima kubwa kwa umma wa Watanzania na kwa hali inayojionesha sasa ndani ya bunge hilo heshima yao itapotea ghafla kama mwanga wa mshumaa kama wao wataendelea kuwa washiriki wa hicho kinachoonekana wazi kunajisiwa na wachache.

Ni vyema wakatumia hekima na busara zao na kujiondoa mapema na kueleza umma sababu za wao kujitoa; sababu ambazo mpaka sasa ziko wazi na hawatahitaji nguvu kubwa kueleza umma juu ya hilo.
 
Wazee mnasemaje kuhusu Mrema? Huyu mzee wa kiraracha?
 
Jembe ndani ya green vesti ya kijani sahau 🙂 wamelaniwa hao chama cha magamba au mafisadi.
 
Mkuu Pasco nimemsikia Edward Lowassa nae akisema ndiyoooo, kumbe nae ni imbecile, insane. Bado utaendelea kutushawishi tumpe kura yetu
Mkuu Kapoloto, kuna kitu kinaitwa pseudo insanity kinachosababishwa na group mentality, ambapo mtu anapata insanity ya muda kutokana na group influence hivyo kuwa kichaa kwa muda tuu, mfano watu wapompiga mwizi wa kuku hadi kumuua binadamu mwenzao, kisa kaiba kuku tuu wa TZS.10,000/=!, au kummwagia mafuta na kumchoma moto binadamu mwenzao for whatever reason, watu hao wanakuwa ni vichaa wa muda!.

Wote waliopiga kura ya ndio kwa upuuzi ule ni Vichaa!.Wawe ni madaktari, maprofesa, wawe ni mawaziri, wawe ni wenye nywele nyeupe, au nyeusi, vichaa ni vichaa tuu bila kujali jina la mtu, hadhi ya mtu, ukubwa wa mtu wala umaarufu wa mtu!, kichaa ni kichaa tuu, uamuzi ule ni uendawazimu!.

Pasco
 

Ni hakika, wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana, nimeumizwa na msiba huu!.

RIP Deo Filikunjombe!.

Pasco
 
Habari zimeenea kuwa jamaa alikuwa na vimada kibao na alikuwa anampiga sana mkewe kiasi cha kutaka kukimbia ndoa hiyo. Pale NBC makao makuu alikuwa na vimada wawili na wengineo. Duh, mtu akiondoka watu ndo wanaanza kuneneza habari za mtu, mbayaaaa!
 
Habari zimeenea kuwa jamaa alikuwa na vimada kibao na alikuwa anampiga sana mkewe kiasi cha kutaka kukimbia ndoa hiyo. Pale NBC makao makuu alikuwa na vimada wawili na wengineo. Duh, mtu akiondoka watu ndo wanaanza kuneneza habari za mtu, mbayaaaa!
hubby Asprin uje uniambie kama na wewe una vimada NbC nisepe zangu mie!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…