Filikunjombe ni jembe

Filikunjombe ni jembe

Deo Filikunjombe ni sawa na wabunge 900 wa CCM na ni sawa na wabunge 11,900 wa CCM wenye vichwa kama vya Lusinde au Komba.
 
Filikujombe, Kangi Lugola na Esther Bulaya ni majembe yaliyopo ccm kwa bahati mbaya
 
Filikujombe, Kangi Lugola na Esther Bulaya ni majembe yaliyopo ccm kwa bahati mbaya

Naamini mambo mengine yanayofanywa na hao wanaojiita WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA yanabeba maudhui yasiyotambuliwa wala kueleweka mbele ya jamii nzima ya Watanzania. Kubwa kwa walio wengi ndani ya bunge hilo ni kuhakikisha wanapata posho kubwa kwa namna yoyote iwayo kwa faida na masilahi ya watawala wachache na marafiki zao.

Katika hali kama hiyo nachelea kusema siku za usoni tutashuhudia watu wachache waliojenga heshima kubwa mbele ya jamii wakidharauliwa, kupuuzwa na kuonekana watu wasio na maana yoyote mbele ya jamii kwa kuingizwa kwao kama wajumbe wa bunge hilo ambalo limenajisiwa na kukosa uhalali wa kuitwa BUNGE MAALUM LA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Kwa hali halisi ilivyo sasa na kwa wale wanaopenda heshima yao iendelee kutamalaki mbele ya umma wa Watanzania ni kujiondoa mapema kutoka kwenye huo mchakato dhalili ili siku za usoni wasije wakasutwa na kudhihakiwa kuwa kwao WALIONA POSHO NI MUHIMU ZAIDI YA MUSTAKABALI MWEMA KWA UMMA WA WATANZANIA.

Niseme tu kuwa ndani ya bunge hilo kuna wanazuoni waadilifu, viongozi wa dini, wanasiasa na wanaharakati waliojijengea heshima kubwa kwa umma wa Watanzania na kwa hali inayojionesha sasa ndani ya bunge hilo heshima yao itapotea ghafla kama mwanga wa mshumaa kama wao wataendelea kuwa washiriki wa hicho kinachoonekana wazi kunajisiwa na wachache.

Ni vyema wakatumia hekima na busara zao na kujiondoa mapema na kueleza umma sababu za wao kujitoa; sababu ambazo mpaka sasa ziko wazi na hawatahitaji nguvu kubwa kueleza umma juu ya hilo.
 
Wazee mnasemaje kuhusu Mrema? Huyu mzee wa kiraracha?
 
Jembe ndani ya green vesti ya kijani sahau 🙂 wamelaniwa hao chama cha magamba au mafisadi.
 
Mkuu Pasco nimemsikia Edward Lowassa nae akisema ndiyoooo, kumbe nae ni imbecile, insane. Bado utaendelea kutushawishi tumpe kura yetu
Mkuu Kapoloto, kuna kitu kinaitwa pseudo insanity kinachosababishwa na group mentality, ambapo mtu anapata insanity ya muda kutokana na group influence hivyo kuwa kichaa kwa muda tuu, mfano watu wapompiga mwizi wa kuku hadi kumuua binadamu mwenzao, kisa kaiba kuku tuu wa TZS.10,000/=!, au kummwagia mafuta na kumchoma moto binadamu mwenzao for whatever reason, watu hao wanakuwa ni vichaa wa muda!.

Wote waliopiga kura ya ndio kwa upuuzi ule ni Vichaa!.Wawe ni madaktari, maprofesa, wawe ni mawaziri, wawe ni wenye nywele nyeupe, au nyeusi, vichaa ni vichaa tuu bila kujali jina la mtu, hadhi ya mtu, ukubwa wa mtu wala umaarufu wa mtu!, kichaa ni kichaa tuu, uamuzi ule ni uendawazimu!.

Pasco
 
This is the first time in history, Bunge letu Maalum la Katiba linapiga kura kwa aina mbili kuunga mkono kanuni kituko cha mwaka kuliruhusu bunge hilo kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja!. Hiki sio tuu ni kioja cha mwaka bali pia ni kituko cha karne na kubwa kulio kumbe Wabunge Wasio Timamu kwenye Bunge hilo Maalum la Katiba Ni Wengi Kuliko Hata nilivyowadhania mwanzo!.

Mtu mzima mwenye akili zako timamu, unawezaje kupiga kura ya ndio kuusupport upuuzi huo?!. Angalau Deo Filikunjombe sii mmoja wa hawa wasio Timamu!

Kiukweli Mhe, Samuel Sitta amenidisapoint hakuna mfano!.I had very high hopes on him with great expectations, now, the Great man is hopeless and a total failure!.
Wote mliokuwa na matumaini ya kupatikana "Katiba Bora", subirieni "Bora Katiba!".

Uliona wapi kura ya siri mtu akatajwa jina?!.

NB. Kutokuwa Timamu, hakumaanishi ni vichaa au wana wazimu,insanity pia imo, imbecile pia imo, na sio vichaa wote ni mpaka waokote makopo!.
Pasco

Ni hakika, wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana, nimeumizwa na msiba huu!.

RIP Deo Filikunjombe!.

Pasco
 
1607109_744799005625801_8378169153150820722_n.jpg
 
Habari zimeenea kuwa jamaa alikuwa na vimada kibao na alikuwa anampiga sana mkewe kiasi cha kutaka kukimbia ndoa hiyo. Pale NBC makao makuu alikuwa na vimada wawili na wengineo. Duh, mtu akiondoka watu ndo wanaanza kuneneza habari za mtu, mbayaaaa!
 
Habari zimeenea kuwa jamaa alikuwa na vimada kibao na alikuwa anampiga sana mkewe kiasi cha kutaka kukimbia ndoa hiyo. Pale NBC makao makuu alikuwa na vimada wawili na wengineo. Duh, mtu akiondoka watu ndo wanaanza kuneneza habari za mtu, mbayaaaa!
hubby Asprin uje uniambie kama na wewe una vimada NbC nisepe zangu mie!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom