Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 8,000
- 16,414
Mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Kiluwa ambaye ndiye Mwenyekiti/Mmiliki wa Makampuni ya Kiluwa Group Tanzania ( KG), amesema yupo tayari kuyaleta Jijini Dar es salaam Mabasi ya Abiria ya MAZ kutoka Ulaya kwa ajili ya kubeba Abiria wa ‘Mwendokasi’.
Kiluwa ameyasema haya leo January 19 Jijini Minsk Nchini Belarus baada ya kutembelea Kiwanda kinachotengeneza Mabasi hayo ambayo yanatajwa kuwa imara zaidi kwa mazingira mbalimbali yakiwemo ya Afrika huku yakija na Waranti ya miaka 10 hadi 15 na uwezo wa kubeba Abiria 200 kwa wakati mmoja.
Kiluwa ambaye amesafiri hadi Jijini Minsk kusaini mkataba na muunganiko wa Viwanda Vikubwa Nchini Belarusi, amesema Kiwanda hiki ambacho kinasifika kwa kuuza Mabasi katika Nchi mbalimbali Ulaya ikiwemo Russia (80% ya Mabasi yao yanatoka MAZ), Lithuania, Serbia, Poland, Bulgaria, Latvia, Hungary na kwa Afrika ni Egypt na Togo kipo tayari kutengeneza Mabasi imara ya ‘Mwendokasi’ yanayoendana na mazingira ya Tanzania.
Akiongea na AyoTV, Kiluwa amesema MAZ ipo tayari kujenga kiwanda cha Mabasi haya Kisarawe Mkoani Pwani pale ambapo Mabasi haya yatahitajika kwa wingi Nchini
Tanzania. #MillardAyoUPDATES
Source: millard ayo