Ndugu zangu wa MMU,
Leo nimeamua kufunguka rasmi
Nimekutana na thread zilizopita zikanipa na mimi munkari zaidi,mara nyingi naandikaga lakini nafutilia mbali ila leo nimeamua kumwaga wino kabisa.
Nimefikia hatua ambayo nafikiri itakuwa vyema kama nikiwa na girlfriend,ila nisingependa tuanze tu "paap" kwamba tunakuwa kwenye uhusiano,ningefurahi sana kama tungeanza kama marafiki ndipo we can move forward.
Kuhusu mimi:
Kwa sasa nina umri wa miaka 23,University graduate,pia ni mfanyakazi.Napenda sana kutumia computers na internet,Photography,Kuogelea,Kutembea,Occassional Drinker,Napenda kusoma na kusafiri
ni mwaminifu.Nina ratiba ndefu kila siku na ningependelea kupata mtu aliye busy pia,mtu wa kubadilishana nae mawazo na kushauriana kila nipatapo nafasi.
Najua kazi nyingi za nyumbani (naweza kupika vizuri,pia najua ukulima na ufugaji),I can fix things vikiharibika,napenda utani na napenda kujifunza kila nipatapo nafasi.
Mimi ni mkristo, ninaufahamu uislam na nimejifunza kuhusu madhehebu mengine.Naheshimu sheria na taratibu za dini zote
.dini sio kigezo kwangu.
Nimeishi sehemu tofauti hapahapa Tanzania ila kwa sasa napatikana Mkoa wa Kilimanjaro(Moshi) ambapo nipo kikazi.
Sifa za nitayependa awe rafiki yangu wa kike:
Natafuta msichana aliye mwaminifu,mcha Mungu,msikivu,anayejiheshimu,aliyeelimika,awe anajitambua na kujua ndoto za maisha yake,awe anapenda kujiendeleza.ambaye tutaendana interests itakuwa vyema zaidi.
Age 18-22(naamini wapo humu JF).Ningependelea zaidi kama atakuwa na account ya facebook/myspace,awe ananitumia text na kuongea na mimi kwenye simu daily.good personality na ambaye atakuwa interested na mimi.
Awe anaishi karibu na mimi(sitapendelea awe anaishi mbali sana na mimi)
Mengineyo:
I am too young kuwa mume kwa sasa.tutaanza kama marafiki,na kama wote tuta-qualify kwa pande zote mbili,we can move on kwenye hatua zingine.
Referrees wanaonifahamu in person
😡roulette ,
Puppy Mwali na matwi
Mawasiliano terms:tutawasiliana zaidi kwa JF pamoja na skype.Baada ya kufahamiana tutabadilishana namba za simu.Tutafahamiana zaidi kadri Muda uendavyo..(Kwa sasa ni PM za JF tu!)
Niko very serious
.ONLY those who are serious should contact me.
Cc:Familia yangu ya JF
watu8 MadameX Chimbuvu nitonye Pipi lara 1 Amoeba Judgement Zinduna MziziMkavu AshaDii neggirl C6 Arushaone Bigirita Bishanga Bujibuji figganigga madameb
sweetlady St. Paka Mweusi Nicas Mtei