BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Je umeshawahi kukutana na mtu akakueleza kwamba ''Huyu ni mdogo wangu'', lakini huyo mdogo mtu akaonekana ni mbavu nene na mkubwa kimaumbile kuliko mkubwa mtu? na wakati mwingine hata urefu mdogo mtu humzidi mkubwa mtu.
Wazaliwa wa kwanza hufubaa sana kutokana na majukumu wanayo beba japo wanapata pesa.
Watoto wawili au watatu wanaweza kuzaliwa katika familia moja lakini wanaweza kuwa tofauti sana. Japo watalelewa katika mazingira sawa ya kijamii, chini ya seti sawa ya sheria na mfumo wa thamani wa familia. Pia wanaweza kuwa sawa kimaumbile lakini wanaweza kuwa tofauti sana katika utu, maslahi na mafanikio.
Ingawa wanaweza kuzaliwa katika familia moja na mzazi mmoja lakini ni wazi kuwa wamezaliwa katika vipindi tofauti, yaani wa KWANZA kuzaliwa ni tofauti na WAPILI kuzaliwa.
Madhara ya nafasi ya kuzaliwa wakwanza yana athari kubwa sana kwa mtoto, mwenendo wa familia huwa unaathiri sana ukuaji wa mtoto wa kwanza kwasababu yeye ndio huchukuliwa kama Case study'' yeye ndiye huchukuliwa kama majaribio, kwani wazazi huamini kuanguka kwa mtoto wa kwanza kutaangusha wote wanaofuatia, na kufaulu kwa mtoto wa kwanza itakuwa ni kichocheo cha ufaulu kwa wote wanaofuata.
Hivyo mtoto wa kwanza hupitia kila aina ya mitihani na kila aina ya majaribio, ili iwe funzo kwa mzazi kunako watoto wanaofuata. Mtoto wa kwanza huwa ni darasa la mzazi katika malezi.
Wazaliwa wa kwanza mara nyingi huhamasishwa zaidi kufikia malengo ya mzazi kuliko waliozaliwa baadaye. Asilimia kubwa ya wazaliwa wa kwanza huishia katika taaluma kama vile udaktari na sheria au vikosi vya usalama.
Nadra sana mzaliwa wa kwanza kumkuta anafanya biashara, labda awe amerithi kutoka kwa mzazi. Lakini walio wengi nguvu huelekeza kwenye taaluma.
Hii ni kwasababu ya magumu na majaribu waliopitia kutoka kwa wazazi wao, Wazaliwa wa kwanza, hutumia nguvu sana za kiakili kuhakikisha kwamba wadogo zao hawawazidi kiakili au kimafanikio, hivyo hutumia umakini wa hali ya juu na nidhamu ili kuthaminiwa na wazazi.
Wazaliwa wa kwanza huzaliwa katika nafasi iliyoshinikizwa. Kawaida ni vitu vya furaha kubwa katika familia - kwasababu wao ni wa kwanza. Wazazi na babu mara nyingi huongeza kila kitu cha msaada na furaha kwa wazaliwa wa kwanza.
Huwa kuna hamasa ya matarajio kwamba atakuja tu, hata kabla ya kuzaliwa kwake. Wazaliwa wa kwanza wengi hupewa majina wakati wa ujauzito, Majina huchaguliwa nusu ya ujauzito na albamu za picha za utoto hujazwa na kutunzwa.
Mtoto wa kwanza huchukuliwa tahadhari zote kutoka kwa wazazi kwasababu mawindo ya shetani huwa ni kumuwinda mtoto wa kwanza na kumvuruga. (Chunguzeni watoto wa kwanza ambao hawako vizuri kiakili na kimaisha huenda walivurugwa na kuangukia sehemu mbaya na wakawa hivyo walivyo sasa)
Wazaliwa wa kwanza huwa wanafunzwa, wanasukumwa kufanya maonyesho. Hivyo matarajio ni makubwa kwa wazaliwa wa kwanza, haswa wavulana wazaliwa wa kwanza, kwa hivyo misukosuko ya shinikizo ni kitu ambacho wanajua kabisa tangu utotoni mwao.
Wanaume wazaliwa wa kwanza huwa wana nafasi ndogo ya kufeli kuliko wazaliwa wakwanza wasichana, au wale walio katika nafasi nyingine za kuzaliwa. Wavulana wazaliwa wa kwanza wanaogopa sana kushindwa hivyo mara nyingi huepuka maeneo ambayo hawawezi kufanya vyema.
Wazaliwa wa kwanza wanaweza kutoroka nyumbani ikiwa mazingira hayako vizuri, wanapoelekea huamini wanakwenda kufanya kazi nzuri zaidi kwasababu wanaogopa sana kuharibu mazingira.
Wazazi huwa wagumu zaidi na wakali kwa wazaliwa wao wa kwanza katika suala la nidhamu, na hulegea kadri wanavyosonga mbele zaidi katika familia. Wazaliwa wa kwanza kwa kawaida hawaitikii vizuri kwa kuwasili kwa mzaliwa wa pili.
Kwa mzaliwa wa kwanza, kuwasili kwa mtoto mwingine kunamaanisha jambo moja tu "Mfalme apoteza taji yake." Mtoto mzaliwa wa kwanza hufanya kila awezalo ili kushika nafasi ya kwanza iliyopendelewa. Ataonyesha mapungufu ya mzaliwa wa pili kwa wazazi wake.
Kuna aina mbili za wazaliwa wa kwanza.
Wa kwanza ni walezi na wanaotii.
Watoto hawa wanapenda kufurahisha na pia wanapenda kufanya vyema shuleni kwani wanahitaji sana idhini ya mama au baba. Pia wanapenda kuwatunza watoto wengine. Walezi hawa wanaotii wana uwezekano mkubwa wa kuwa wasichana. Wazazi mara nyingi huwategemea sana wazaliwa wao wa kwanza ambao ni wasichana huwaacha wachukue majukumu mengi nyumbani ikiwemo kuwatunza wadogo zao. Ni nadra sana mtoto wa kiume wakwanza kuachiwa wadogo zake awalinde, jukumu hili huwa ni la mzaliwa wa kwanza wakike
Aina ya pili ya wazaliwa wa kwanza ni wahamaji na watikisaji wa fujo.
Watoto hawa wana uthubutu, wenye mwelekeo wa kufanikiwa na wenye nia thabiti. Mara nyingi ni wavulana ambao wana mihemko, lakini hawana ujuzi, hisia zao ziko sana nje kuliko ndani, wanaamini sana kutoka kuliko kukaa ndani, hivyo wazazi huwa hawaachi majukumu ya malezi kwa watoto wa namna hii. Haswa pale wanapokuwa wadogo.
Tuwaonee huruma watoto wetu wa kwanza, kuna mengi magumu wanapitia na wataendelea kupitia, sisi kama wazazi watoto wetu wa kwanza ndio huwa darasa letu la malezi.
Kama mwanao wa kwanza anakusumbua jitahidi kutumia kila mbinu kumrejesha katika mstari, watoto hawa wanashida nyingi sana zinazoonekana na zisizoonekana. Usikate tamaa katika malezi ya mwanao.