Fisadi anataka kukimbia na kutoroka Nchini

Fisadi anataka kukimbia na kutoroka Nchini

Hapa naona hoja ya Mtikila inaanza kupata "mashiko" kuwa huyu RA sio mwenzetu .
 
Kuna taarifa kuwa lile sakata la mkataba tata baina ya Serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond limechukua sura mpya baada ya baadhi ya vigogo maarufu kuanza kuliwa mingo ili wadakwe kabla ya kuchukua hatua zozote za kutimkia nje ya nchi. Hivi kuliwa mingo kama alasiri wanavyosema ni kukua kwa kiswahili ama?
 
Mi nakwambia mambo yanawataiti hao mafisadi watu wanasema sijui nachosema.
Haya kama hawaoni hayo mimi basi niko radhi kuitwa kichaa.
Cha muhimu na wazuiliwe hadi JK arudi.
 
Kuna taarifa kuwa lile sakata la mkataba tata baina ya Serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond limechukua sura mpya baada ya baadhi ya vigogo maarufu kuanza kuliwa mingo ili wadakwe kabla ya kuchukua hatua zozote za kutimkia nje ya nchi. Hivi kuliwa mingo kama alasiri wanavyosema ni kukua kwa kiswahili ama?

Mkuu kuliwa mingo ni kuhakikisha hawatoki nje ya rada.
 
Baadhi ya waliotajwa katika ripoti hiyo ya Dk. Mwakyembe, kwamba wanahusika na Richmond kwa namna mbalimbali ni pamoja na Mbunge wa Igunga (CCM), Mhe. Rostam Aziz, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Johnson Mwanyika na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa , Dk. Edward Hosea.

ROSTAM AZIZI ALIENDA KUWASHITAKI MWANAHALISI MAHAKAMANI KUWA WALISEMA YEYE ALIHUSISHWA KWENYE RICHMOND SASA ALASIRI WAMESEMA NGOJA TUONE KAMA ATAENDA MAHAKAMANI KUPAMBANA NA MENGI AU ALIKUWA ANAMWONEA KUBENEA .
 
Roast the mizizi ... huyo ... atalindwa mpaka atakuwa salama tu ... maana watanzania hatuna kelele za kuendelea .. baada siku chache tutanyamaza mambo yataendelea kama kawa ... maana si yeye wa kwanza kutajwa na hapajakuwa na adhabu ... ama hatuna pa kushitaki ... ndiyo najiuliza tufanye nini ... teundeleze kelele tu au?
 
Back
Top Bottom