Msaada tafadhali nahisi kufakufaKuna jamaa yangu alipona ivyo vidonda tena mtoa dawa anakupa na kukuambia ukipona ndo uje kulipa kama shukrani kwanza kwa mola then kwake!
Ukiona dawa yoyote inatangazwa sana ujue ina walakini
Mara ya kwanza kwenda pale kwa huyu mganga wa kienyeji Rahabu ilikuwa mwaka 2006, kuna jamaa angu alikuwa mgonjwa sana wa vidonda vya tumbo. Kwa kipindi hcho pia nilikuwa na ulcers ila nilikuwa nazichukulia poa kwa kuzituliza na "omeprazole".
Baada ya mda jamaa angu aliniambia amepona ila alikuwa amekwisha sana kama muathirika vile, sababu ya masharti ya vyakula!
Jamani ni kuna masharti ya vyakula balaa...
Mwaka 2007 mwishoni pia vidonda vilinichachamalia sana,
ikabidi niende pale kuanza dumu la 1... Baada ya wiki mbili tayari nlkuwa hoi kwa masharti ya vyakula, nilipomaliza dozi ya madumu 4 nkawa bado sijapona na nkazidi kukondeana.
Familia yangu ikaingilia kati, Baba akaenda kumtupia madumu yake huyo bibi Rahabu.
Tukampata Msukuma mmoja hvi alinipa dawa ya kuchanganya Maziwa fresh, Samri, Asali na kuna mitishamba flani hv(hapo ndo sijui miti gani ningewatajia). Hiyo dawa ilikuwa nzuri sana kwanza haina masharti ya vyakula isipokuwa pilipili tu,
mkuu tupe contact zake uyo jamaa,
Vidonda vya tumbo vinatibika hata hospitali lakini ni kati ya wagonjwa 7 miongoni mwa 10
tatizo ni 'adherance to treatment' kufuata maelekezo ya dawa na lishe katika kipindi cha matibabu.
Changamoto:
1:dawa nzuri ni za garama na mara nyingi wanaougua hawana kipato kizuri
2:soko huria limeingia hadi kwenye dawa ziko kibao feki na huwezi kuzitambua
3:madaktari wengi hawana ozoefu wa jinsi ya kutibu ki matendo,wanarubuniwa na matangazo ya dawa kutoka kwa promota
4:hamna utafiti endelevu wa jinsi ya kushughulikia hili tatizo
kama kuna mtu anatatizo kama hili ntamuuelekeza vipimo vya kufanya na baada ya majibu ntamuelekeza dawa za kununua na masharti yake ila inahitaji hela
Kuna jamaa yangu alipona ivyo vidonda tena mtoa dawa anakupa na kukuambia ukipona ndo uje kulipa kama shukrani kwanza kwa mola then kwake!
Ukiona dawa yoyote inatangazwa sana ujue ina walakini
Vidonda vya tumbo vinatibika hata hospitali lakini ni kati ya wagonjwa 7 miongoni mwa 10
tatizo ni 'adherance to treatment' kufuata maelekezo ya dawa na lishe katika kipindi cha matibabu.
Changamoto:
1:dawa nzuri ni za garama na mara nyingi wanaougua hawana kipato kizuri
2:soko huria limeingia hadi kwenye dawa ziko kibao feki na huwezi kuzitambua
3:madaktari wengi hawana ozoefu wa jinsi ya kutibu ki matendo,wanarubuniwa na matangazo ya dawa kutoka kwa promota
4:hamna utafiti endelevu wa jinsi ya kushughulikia hili tatizo
kama kuna mtu anatatizo kama hili ntamuuelekeza vipimo vya kufanya na baada ya majibu ntamuelekeza dawa za kununua na masharti yake ila inahitaji hela
jamani kwa wale mnaojua au mliowahi kutumia dawa ya huyu binti Dr rahabu ambayo inasemekana kutibu vidonda vya tumbo.jamani ni kweli hii dawa inatibu?
kuna concept fulani tunaitumia katika medical sociology kuwa dawa au matibabu hayatangazwi kama bidhaa. sijui sheria za nchi zinasemaje? sijawahi kusikia tangazo kuwa hospitali bora ni muhimbiri au kcmc, bugando n.k wagonjwa tunajipeleka au tukuwa refered kule. sasa hawa watu wa altenative medicine kwa nini wanafanya an ethical practice na wanaachiwa?
Mkuu unasumbuliwa na vidonda vya tumbo?
Nimewahi kusumbuliwa na vidonda vya tumbo na vilifikia hatua mbaya kiasi cha kushindwa hata kula chakula chenye chumvi au nyanya. Na wakati mwingine nikila chakula cha usiku kesho yake natapika kikiwa hakijameng'enywa hata kidogo. Nimewahi kulazwa mara 3! Huu ugonjwa usikie tu usikupate!
Nilipewa dozi na jamaa mmoja bure, japo ilikuwa ngumu kuamini lakini nilipona na sisumbuliwi tena tangu mwaka 2001. Kwa kuwa nilipewa bure nami natoa bure na watu wengi wamepona.
Mahitaji:
1. Kuku mtetea (sijui sababu)
2. Maziwa "fresh" lita 4 (yasichakachuliwe i.e. yasichanganywe na maji)
Maandalizi:
1. Muandae kuku kwa ajili ya kupika (mkatekate vipande)
2. Mpike kuku kwa kutumia maziwa, usiweke kitu chochote zaidi ya maziwa hadi aive. Utabakiwa na lita kama 2 hivi. Toa vipande vya kuku bakiza mchuzi tu (hiyo ndo dawa yenyewe).
Dozi:
Kunywa nusu bilauri (glass) mara tatu kutwa kwa muda wa siku tatu. Unaweza kuhifadhi kwenye friji mchanganyiko huu. Mi nilikunywa siku mbili tu.
Ile nyama ya kuku inaweza kuwekwa viungo na kuliwa kama kawaida. Kilichokuwa kinahitajika ni mchuzi.
Kila la kheri.