Mara ya kwanza kwenda pale kwa huyu mganga wa kienyeji Rahabu ilikuwa mwaka 2006, kuna jamaa angu alikuwa mgonjwa sana wa vidonda vya tumbo. Kwa kipindi hcho pia nilikuwa na ulcers ila nilikuwa nazichukulia poa kwa kuzituliza na "omeprazole".
Baada ya mda jamaa angu aliniambia amepona ila alikuwa amekwisha sana kama muathirika vile, sababu ya masharti ya vyakula!
Jamani ni kuna masharti ya vyakula balaa...
Mwaka 2007 mwishoni pia vidonda vilinichachamalia sana,
ikabidi niende pale kuanza dumu la 1... Baada ya wiki mbili tayari nlkuwa hoi kwa masharti ya vyakula, nilipomaliza dozi ya madumu 4 nkawa bado sijapona na nkazidi kukondeana.
Familia yangu ikaingilia kati, Baba akaenda kumtupia madumu yake huyo bibi Rahabu.
Tukampata Msukuma mmoja hvi alinipa dawa ya kuchanganya Maziwa fresh, Samri, Asali na kuna mitishamba flani hv(hapo ndo sijui miti gani ningewatajia). Hiyo dawa ilikuwa nzuri sana kwanza haina masharti ya vyakula isipokuwa pilipili tu,
mkuu tupe contact zake uyo jamaa,