Fitina na Uhuni behind draw za CAF, tukomae tu

Fitina na Uhuni behind draw za CAF, tukomae tu

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Hizi draw za CAF Huwa tayari zinakuwa zishapangwa huko nje, hapo wanakuja kutimiza ratiba.

Michuano hii huwaga na fitina nyingi sana, kuanzia Kwa marefa, mapokezi, uchezeshaji wa draw na fitina ya kuhonga timu pinzani Ili wakubwa wapite kirahisi.

Sasa ni wakati wa watanzania kujikomaza kisaikolojia, wametupangia hivyo makusudi Ili tutoke , wametuona sisi ni dhaifu, nasema sisi watanzania sio dhaifu , lazma tukabiliane na mishale yote dhidi yetu.

Sasa kwenye Madam Kuu, Hawa jamaa wa CAF Huwa tayari washapanga nani akutane na nani, pale utaona mipira yote katika vyungu tengwa inafanana Kila kitu ukiangalia Kwa macho lakini sio kweli mipira haifanani, nikujulishe kumekuwa na uvujaji wa taarifa juu ya kinachofanyika kwenye draw za michuano mkubwa kama hii.

Sasa unaweza ukaona Kwa mbali ama kwa karibu mipira minne ya chungu kimoja inafanana kwa Kila kitu yaani rangi na size, ila kiukweli hilo halipo na ndomaana nasema draw inapangwa nje, pale unaweza kuona mipira imefanana rangi lakini anaebeba mpira anajua kabisa nabeba timu gani kwasababu wahuni wale huwa katika mipira iliyofanana ndani yake utakuta kuna mpira wa moto yaani unajoto labda huyu yanga, kuna mpira wa baridi huyu labda simba, kuna mpira mzito kuliko mingine huu utajua ni mamelod, na kuna mpira kama una upele huyu ni asec.

Hivyo kuzani kwamba draw inachezeshwa fair ninkujidanganya, all in all mpira utabaki kuwa na maajabu yake , watu wanaweza wakafanya Kila kitu ila mpira ukaja na matokeo yake ya kipekee
 
Leo asubuhi mapema tu nimekuta micky jnr amepost kaandika draw test halafu kaweka draw hii hii iliyopangwa na CAF. yaani niliona kama anatabiri tu ile asubuhi ila kuona kila kitu kimefanana kwakweli nikaingiwa na mashaka. Nikaingia kwenye post zake baada ya kutoka kwa draw nikaona kafuta ile post. Kwa waliona post ya Micky Jnr watakuwa mashahidi kwa hiki nachosema
 
Yanga tusiogope, mashabiki wengi hawana Imani ya kusonga mbele hivo itafanya wachezaji kucheza wakiwa hawana stress sana tofauti na mamelodi....

Hata tukitoka tunaendelea kujikomaza, Rome wasn't built in a day
 
wametuona sisi ni dhaifu, nasema sisi watanzania sio dhaifu , lazma tukabiliane na mishale yote dhidi yetu.
Hofu zako tu. Wanatuona dhaifu au tishio? Tumeingiza timu 2 robo useme wanatuona dhaifu? Sio kwel..

Na kama hii ni mipango, bas ni dhahir wanajaribu kufikir tutatoka mapema kudhirisha hofu walionayo
 
Mwaka Jana alilikosa Kwa uzembe tu...draw ya 2-2 nyumbani...basi...
Halafu ni bingwa WA super league...

Haogopwi bure ..

Super league ni bonanza tu ni mashindano ya timu 8 kwa kualikwa .

Caf champions league ni mashindano yanayoshirikisha timu zaidi ya 50 za nchi zote africa.

Ndio maana bingwa wa CL ndie anaeitwa bingwa wa africa na ndie anaenda kushiriki Fifa club world cup.
 
Back
Top Bottom