Fitina na Uhuni behind draw za CAF, tukomae tu

Fitina na Uhuni behind draw za CAF, tukomae tu

Mamelodi sundown kaleta stress Sana Leo...
Mimi simba hawa utopolo walikuwa wanatusumbua sana,yaan mpaka leo tena mpaka jamaa nikamwambia mkuu unaweza wewe kupangiwa hata na hao Yellow Nation,lakin mwana utopolo alikuwa haambiliki.

Yaan unakuta utopolo linakwambia Simba vs mamerod

Yanga vs assec mpaka unashangaa,ila leo ndio wakome
 
Leo asubuhi mapema tu nimekuta micky jnr amepost kaandika draw test halafu kaweka draw hii hii iliyopangwa na CAF. yaani niliona kama anatabiri tu ile asubuhi ila kuona kila kitu kimefanana kwakweli nikaingiwa na mashaka. Nikaingia kwenye post zake baada ya kutoka kwa draw nikaona kafuta ile post. Kwa waliona post ya Micky Jnr watakuwa mashahidi kwa hiki nachosema
Tena mwamba aliweka mapema sana
 
Hizi draw za CAF Huwa tayari zinakuwa zishapangwa huko nje, hapo wanakuja kutimiza ratiba.

Michuano hii huwaga na fitina nyingi sana, kuanzia Kwa marefa, mapokezi, uchezeshaji wa draw na fitina ya kuhonga timu pinzani Ili wakubwa wapite kirahisi...
Sisi ni wakubwa na tumepangwa na wakubwa wenzetu.
 
Hizi draw za CAF Huwa tayari zinakuwa zishapangwa huko nje, hapo wanakuja kutimiza ratiba.

Michuano hii huwaga na fitina nyingi sana, kuanzia Kwa marefa, mapokezi, uchezeshaji wa draw na fitina ya kuhonga timu pinzani Ili wakubwa wapite kirahisi...
Furgeson aliwahi lalamika kila draw ikipangwa kaangukia Madrid sasa nyinyi wa dar es salaam mna vidaka matonge virefu sana mimi kila mkikomeshwa huwa nasikia raha pambaneni hakuna hujuma wala nini mpira wenu umekua!
 
Katika yote uloandika nadhani la msingi ni hiyo point ya mwisho. Iwe kwa fitna au kwa halali lazima timu zetu kupambana.
 
Ni jambo ambalo lisingewezekana kwa timu kama Al Ahly kukutana na Mamelody kwenye mtoano.

Draw inapangwa kwa kuzingatia vigezo vya nafasi ambazo timu ilimaliza kwenye group stage.

Timu zote zilizomaliza zikiwa kinara zinahesabiwa kama ndio timu bora.

Na kawaida ya mashindano ladha inakuja pale timu bora zinapokutana mwishoni.

Kwa kuliona hilo zikawekwa kanuni ya kufanya timu bora zisiweze kukutana kwenye hatua za mwanzoni.

Kwamba timu ambazo zilimaliza zikiwa namba moja kwenye kundi zitapangwa na timu ambazo zilishika nafasi ya pili.

Timu nyingi zinazoshika nafasi ya pili mara nyingi ndio zile ambazo zinajitafuta japo kuna muda hata timu kubwa zinajikuta zinaangukia kwenye hiyo nafasi.

Sasa kinachofanyika ili kuipata ile ladha ya mpira halisi sheria ikawekwa kuwa hizi timu kubwa zilizovuka makundi zikiwa kinara haziwezi kukutana kwenye hatua ya robo ili huko mbeleni wabaki wababe peke yao.

Isingeweza kuleta ladha halisi ya mashindano kama fainali zinakutana zile timu dhaifu kwasababu wakubwa walitoana wenyewe kwa wenyewe.

Na sheria hiyo ipo hata kwenye preliminary round, timu yenye point nyingi inapangiwa na timu yenye point ndogo.

Na ndio maana huwezi kuona Al Ahly na Mamelody wanakutana kwenye hatua hizo za mwanzoni.

Msimu wa 2020/021 Simba tuliongoza kundi tukapewa kibonde Kaizer Chiefs ambaye alikuwa group moja na Mamelody

Mamelody kwasababu alikuwa ndio kinara kwenye group akapangwa na Al Ahly ambao walikuwa nafasi ya pili nyuma yetu.

Kwa hiyo sio kweli kuwa kuna figisu zinafanyika bali ni kanuni tu, kwasababu tunaona Mamelody alikutana na Al Ahly kwa kigezo hiki hiki kilichotumika leo.
 
Tuache kulia lia, ligi ya mabingwa usitegemee ukutane na mchekea mwanzo mwisho.

Hata kama wamepanga, sie tupambane tu.

Na sidhani kama caf kuna taifa wanalihusudu kwenye uchizi wa usoka baada ya waarabu kama tanzania, sisi tuna vibe, mitandao ya kijamii jambo likiihusu tanzania comments zake sio sawa na taifa jingine.
 
Wakubwa siku zote uwa wanajichagukia timu wanazo zani ni dhaifu ila ukisha watoa nishai Wana kukimbia.

Kwenye mahojiano baada ya makundi kupangwa Engineer Hersi Ali dokeza, wakati Yanga wanacheza mechi ya mwisho dhidi ya Ahly, Mamelodi walikua wametuma wataalamu wao kuja kuangalia mechi Ile.
Maana yake tayari walisha panga kua watakutana na Yanga.

Kinacho hitajika ni Yanga kuwaandalia surprise package ao Mamelodi na ita watisha wakubwa wengine wa soka kwamba nyuki hapigwi busu.
 
Back
Top Bottom