Castr
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 35,012
- 70,201
Kuna mwaka nilitaka kua full time boxer nikaenda kwenye klabu moja ya ngumi Mabibo, huku nikiwa na sare za shule, nikakutana na kocha wa pale baada ya kumueleza shida yangu akaniambia.
"Ingia ulingoni, nataka kuona unavyopigana"
Akachaguliwa mpinzani wangu, hakukua na safety gears zaidi ya gloves tu, mpinzani alionekana mtoto zaidi yangu hivyo nikawa na confidence kua "Sasa hivi namaliza show"
Tukaingia ulingoni, nimevua suruali ya shule nimebaki na bukta nimevua shati nipo kifua wazi chini nilivaa raba siku hiyo. Kwa ambao kupigana siyo sehemu ya maisha yetu hua tukipigwa ngumi tunasizi kama sekunde nne hivi, hiyo ni ngumi moja.
Wazia zikiwa zaidi ya moja, na ndani ya sekunde sita mtu ana uwezo wa kurusha ngumi mpaka 18. Kama ana nguvu ngumi ile ile moja inatosha kukuangusha na usinyanyuke.
Hivyo sikumpata hata na ngumi moja na niliumbuka. Kocha akaniambia "Hauna stamina, skills na bado una hofu na ulingo, katafute pumzi na stamina kisha rudi baada ya mwezi"
Nikaanza kukimbia, nilikua natoka Mwananyamala Kwa Kopa mpaka Magomeni Mikumi, kisha kila asubuhi na usiku napiga push ups mia mia.
Baba akajua nia yangu akaniweka chini akaniambia michezo haijawa njia ya ukombozi kiuchumi kwa Tanzania, kama unahisi upo tayari kutupa masomo uwe bondia mi sina neno.
Ubondia ukaishia pale, lakini mwili ulishakua step fulani mbele kimazoezi nifanye nini sasa? Nikaendelea kukimbia lakini spark niliyokua nayo ikawa imekata, sijisikii tena naona sina goal na kama sina goal kwanini niendelee? Nikaacha.
Kisha nikiwa internet nikakutana na mlemavu wa mguu, Joshua Sundquist, akiwa na miaka 9 jamaa alikatwa mguu na akawa anaishi goalless mpaka alipoamua kuanza bodybuilding. More searching nikakutana na picha yake ya before and after bodybuilding.
I was motivated.
Right until nilipomjua Zachary Ruhl
Nikaona sina kisingizio kuna mtu hana mguu kuna mtu hana miguu ila hawafanyi hiko kama kisingizio cha kutofanya mazoezi.
Nikaanza kwenda gym, ngumu sana mwanzoni unahisi kila mtu anakuangalia akucheke, unamuona anayekusahihisha anajifanya mjuaji lakini baada ya mwezi kila kitu kikawa kwenye mstari.
Gym nyingi hasa za uswazi hua wanabandika mapicha ya bodybuilders wengine nikiwa gym Kigamboni inaitwa Home Ghym (ndivyo alivyoandika labda abadilishe) nikakuta picha yenye kichwa cha habari 'Bill Pearl at 60' ikimuonyesha mzee wa miaka 60 akiendelea na bodybuilding....
Niliitazama picha kwa muda. Lilikua ni kama tusi mzee wa miaka 60 ana physique nzuri inatazamika na mimi nilikua kijana ila nilikua na mwili wa kawaida tu kuonyesha nafanya mazoezi. Nikaamua kudouble struggle the hustle nikawa natrain kwa kujichallenge mwenyewe na kuhakikisha nafocus kwenye kuyajua mazoezi siyo matokeo ya mazoezi.
I became big and cut, definition kila mahali so big mpaka kuna binti chuo akanikataa kisa hicho.
Nimeacha mazoezi kwa muda, ila jana usiku nikiwa bodybuilding forum nikakutana na story ya Dr. Jeffrey Life, mzee wa miaka 80 ambaye anafanya bodybuilding.
Ikanikumbusha safari yangu ya kuamua kusukuma weight na watu walioniinspire njiani.
Narudi zizini wakuu, mwenzangu "Kisingizio chako ni nini?"