FITNESS: Kisingizio Chako Ni Nini?

FITNESS: Kisingizio Chako Ni Nini?

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Kuna mwaka nilitaka kua full time boxer nikaenda kwenye klabu moja ya ngumi Mabibo, huku nikiwa na sare za shule, nikakutana na kocha wa pale baada ya kumueleza shida yangu akaniambia.

"Ingia ulingoni, nataka kuona unavyopigana"

Akachaguliwa mpinzani wangu, hakukua na safety gears zaidi ya gloves tu, mpinzani alionekana mtoto zaidi yangu hivyo nikawa na confidence kua "Sasa hivi namaliza show"

Tukaingia ulingoni, nimevua suruali ya shule nimebaki na bukta nimevua shati nipo kifua wazi chini nilivaa raba siku hiyo. Kwa ambao kupigana siyo sehemu ya maisha yetu hua tukipigwa ngumi tunasizi kama sekunde nne hivi, hiyo ni ngumi moja.
Wazia zikiwa zaidi ya moja, na ndani ya sekunde sita mtu ana uwezo wa kurusha ngumi mpaka 18. Kama ana nguvu ngumi ile ile moja inatosha kukuangusha na usinyanyuke.

Hivyo sikumpata hata na ngumi moja na niliumbuka. Kocha akaniambia "Hauna stamina, skills na bado una hofu na ulingo, katafute pumzi na stamina kisha rudi baada ya mwezi"
Nikaanza kukimbia, nilikua natoka Mwananyamala Kwa Kopa mpaka Magomeni Mikumi, kisha kila asubuhi na usiku napiga push ups mia mia.

Baba akajua nia yangu akaniweka chini akaniambia michezo haijawa njia ya ukombozi kiuchumi kwa Tanzania, kama unahisi upo tayari kutupa masomo uwe bondia mi sina neno.
Ubondia ukaishia pale, lakini mwili ulishakua step fulani mbele kimazoezi nifanye nini sasa? Nikaendelea kukimbia lakini spark niliyokua nayo ikawa imekata, sijisikii tena naona sina goal na kama sina goal kwanini niendelee? Nikaacha.

Kisha nikiwa internet nikakutana na mlemavu wa mguu, Joshua Sundquist, akiwa na miaka 9 jamaa alikatwa mguu na akawa anaishi goalless mpaka alipoamua kuanza bodybuilding. More searching nikakutana na picha yake ya before and after bodybuilding.
images.jpg

I was motivated.

Right until nilipomjua Zachary Ruhl
images%281%29.jpg

Nikaona sina kisingizio kuna mtu hana mguu kuna mtu hana miguu ila hawafanyi hiko kama kisingizio cha kutofanya mazoezi.

Nikaanza kwenda gym, ngumu sana mwanzoni unahisi kila mtu anakuangalia akucheke, unamuona anayekusahihisha anajifanya mjuaji lakini baada ya mwezi kila kitu kikawa kwenye mstari.

Gym nyingi hasa za uswazi hua wanabandika mapicha ya bodybuilders wengine nikiwa gym Kigamboni inaitwa Home Ghym (ndivyo alivyoandika labda abadilishe) nikakuta picha yenye kichwa cha habari 'Bill Pearl at 60' ikimuonyesha mzee wa miaka 60 akiendelea na bodybuilding....
images%285%29.jpg

Niliitazama picha kwa muda. Lilikua ni kama tusi mzee wa miaka 60 ana physique nzuri inatazamika na mimi nilikua kijana ila nilikua na mwili wa kawaida tu kuonyesha nafanya mazoezi. Nikaamua kudouble struggle the hustle nikawa natrain kwa kujichallenge mwenyewe na kuhakikisha nafocus kwenye kuyajua mazoezi siyo matokeo ya mazoezi.
I became big and cut, definition kila mahali so big mpaka kuna binti chuo akanikataa kisa hicho.

Nimeacha mazoezi kwa muda, ila jana usiku nikiwa bodybuilding forum nikakutana na story ya Dr. Jeffrey Life, mzee wa miaka 80 ambaye anafanya bodybuilding.
images%283%29.jpg

Ikanikumbusha safari yangu ya kuamua kusukuma weight na watu walioniinspire njiani.

Narudi zizini wakuu, mwenzangu "Kisingizio chako ni nini?"
 
Wengi muda unawabana sana mkuu japo wanatamani sana kujoin Mazoezi...
Kuna mazoezi mbalimbali mengine unayamodify tu yaendane na hitaji lako la kutunza muda.
 
Uzito wako ni kiasi gani na unataka kufika kiasi gani?

Binafsi mazoezi kwangu ni sehemu ya afya yaani nafanya mazoezi ili kuepuka magonjwa ni kama kinga, na nikiwa naanza kuyafanya mazoezi kwangu yanakuwa kama starehe au burudani. Huwa nafanya mazoezi huku nayafurahia sitegemei kuona matokeo ndani ya muda mfupi. Hiyo ndo hunipa stamina ya kufanya mazoezi kuwa endelevu bila kuchoka.
 
Mimi kubeba vyuma kwangu,ni sawa na kufanya kazi nzito bila ya kutokumfahamu tajiri yako ataekulipa hio hela baada ya kumaliza kubeba vitu vizito[emoji1321]
 
I hate dem akiwa na manyama uzembe[emoji13]
Hususan pale anapovua sidiria halaf minyama ya ubavuni imeshuka kama droo za jikoni[emoji13][emoji13]
No sijafika huko nasitafika manyama ya pembeni yanakuwa kama kitabu oghhhh! yanaharibu mwonekano sana .kitumbo cha kujifungua kipo kwa mbali nataka kujua namna ya kupambana nacho.mbona mazoezi ya kukimbia hayakimalizi jamani
 
Nutrition? Unakula vipi?

Kama unafanya mazoezi ili tu viungo vya ndani viwe poa, na stamina na pumzi viwepo then nutrition sio big deal. La kama nia yako ji kubadilisha outward appearance yako basi angalia kwa makini sana nini unakula na namna unavyokula.
 
asubuhi mara nyingi uji oats,dona ,mchele its depends kikombe kimoja tuu mchana ugali size ya ngumi na mamboga mengi jioni kama ni wali nala kabla ya saa mbili sijui huu ni ulaji mbaya ISO M.CodD
 
ISO M.CodD habari ya soda,Chips na vikaangwa nimeachana navyo kabisa au ni mu=augali nnayo kula mkuu?
 
asubuhi mara nyingi uji oats,dona ,mchele its depends kikombe kimoja tuu mchana ugali size ya ngumi na mamboga mengi jioni kama ni wali nala kabla ya saa mbili sijui huu ni ulaji mbaya ISO M.CodD
Honestly mimi sio nutritionist, nimekupa kama challenge tu ufanye research.

Lakini nadhani wali, ugali, dona ni wanga mwingi sana na una energy (calories) nyingi kuliko mahitaji yako. Hivyo either ongeza mazoezi ya kuchoma calories mf. aerobic na bodyweight training au punguza calories even more. Pia kula kidogo kidogo mara kadhaa kwa siku rather than milo mitatu straight ya kushiba.
 
Shukrani
 
ISO M.CodD habari ya soda,Chips na vikaangwa nimeachana navyo kabisa au ni mu=augali nnayo kula mkuu?
Hivyo vyote ulivyoviacha ni kweli havifai kutokana kuwa na sukari / fats nyingi na hivyo kuwa na calories nyingi.

Lakini at the end of the day it is a calories game. Na genetics kidogo. Ukitumia more than you take in, the body will use its reserves na ukitake in more than you use the body will replenish its reserves. Where in the body does it choose to store/take the reserves is left to genetics ndio maana hakuna zoezi litakalopunguza mafuta eneo moja tu na kuacha maeneo mengine untouched.
 
Mleta mada unaonekana ni mtu usiyejiamini na huna msimamo thabiti!

Mada yako inajieleza kabisa,mara ushike hiki kisha uache and then unapata mtu anakuinspire kisha unarudi tena halafu unaacha tena mara unarudi tena!!

Kua na msimamo na muamuzi ni wewe usikubali mtu akupangie cha kufanya au kucontroll ur life..

Samahani lakini mkuu.
 
Mimi kubeba vyuma kwangu,ni sawa na kufanya kazi nzito bila ya kutokumfahamu tajiri yako ataekulipa hio hela baada ya kumaliza kubeba vitu vizito[emoji1321]
Mazoezi siyo vyuma tu chief, kuna watu wanakimbia, kuna watu wanacheza ngumi, kuna wacheza mpira, kuna kila unachoweza kufanya kama mazoezi hata kusukuma tairi la gari ni mazoezi.
 
I hate dem akiwa na manyama uzembe[emoji13]
Hususan pale anapovua sidiria halaf minyama ya ubavuni imeshuka kama droo za jikoni[emoji13][emoji13]
Sasa ndiyo umpe moyo muanze kujogg
 
Uzito wako ni kiasi gani na unataka kufika kiasi gani?

Binafsi mazoezi kwangu ni sehemu ya afya yaani nafanya mazoezi ili kuepuka magonjwa ni kama kinga, na nikiwa naanza kuyafanya mazoezi kwangu yanakuwa kama starehe au burudani. Huwa nafanya mazoezi huku nayafurahia sitegemei kuona matokeo ndani ya muda mfupi. Hiyo ndo hunipa stamina ya kufanya mazoezi kuwa endelevu bila kuchoka.
Speechless.

Wengi hutamani matokeo ndani ya muda mfupi, husababisha kuhisi unachelewa
 
Back
Top Bottom