Five killed in Barrick Tanzanian mine attack

Five killed in Barrick Tanzanian mine attack

Vithaaaaaa ni vithaaa thuu muraaaaaa! Jamani wakurya si kabila la kuchezea,kwao kucharangana mapanga na kulengana mishale ni jambo la kawaida tu. Nafikiri mheshimiwa mbunge alilisahau hilo, morrri wa kimasai na mzuka wa kikurrrya hautofautiani sana. Vithaaa ni vithhaaaa thuuu murrrr - rrrrraaaaaaa.unapokwenda kusuluhisha ugomvi kati ya mkurya na mkurya sharti nawe uwe na panga mkononi,kwakuwa lolote laweza tokea, na jambo hili wakurya wote wanalifahamu.
 
Naishangaa serikali kujibaraguza kugharimia mazishi,kumbe mlishaandaa bajeti ya mazishi? kabla hamjatuma askari wakawaue watanzania wenzetu ambao walikuwa wakipigania rasilimali yao,shame on you the weakest gvt.............................
 
nikitendo cha kinyama hata kama walikuwa na mapanga kwanini hawakuwapiga kwy miguu
hata IGP aliulizwa ana nini la kusema juu ya vifo hivyo muda mdogo baada ya tukio
na hakuweza kutoa jibu. ilikuwa kwy kikao cha alert juzi
 
icon1.png
Re: Hali si shwari wilayani tarime


Safi sana, nguvu ya umma itaamua siku moja. Badala ya kuvaa nguo nyeusi kwa ajili ya maombolezo wao wanajivalia kijani, huyu Nyangwine pamoja na kuandika vitabu vyote hajaelimika tu. CCM mtatafunwa na dhambi ya kuua raia wasio na hatia kwa kutumia vyombo vya dola visivyojua wajibu wao wa kulinda usalama wa raia.

Huwa haandiki, anaandikiwa. Yeye ni bosi wa kampuni, hutumia mawazo ya wasomi wenzie kutoa vitabu.
 
Walishapanga waue ndio maana wakaanda na bajeti ya mazishi,wanapata wapi hela hizo wakati mishahara tazara hawajalipwa?mantiki bajeti ya mauaji hayo ilishandaliwa.
 
Wakurya ni watu wastarabu sana sema wako kwenye nchi iliyojaa ubabaishaji na uongo sasa wao wasiopenda hayo mambo ya hovyo wanaonekana wabaya na wakorofi...hivi ndugu yako akipigwa risasi akafa unaklichukuliaje hilo?!! watu wanasema tu mana hayajawafika!!
 
Mimi sina la kusema kwa kuwa Serikali imediriki kusema hawa ni wahalifu na adhabu yao ni risasi na si kuwa mahakamani kupata haki .Very sad Nchi hii inatafuta laanaya dola kumwaga damu .Iko siku na haya yataisha .
 
kila siku nasema hawa wanaoibeba serikali ya ccm watakosa pa kukimbilia siku moja, ngoja nchi ipate uhuru kwa mara ya pili tuone wataenda wapi.
 
Hapo ndipo hii sirikali inaponiacha na maswali mengi bila majibu!
 
Kama Pesa zote badala ya kuwasaidia Wakazi zinaenda Dar serikali itakuwa na matatizo tu. Ni rahisi suluhisho chukueni kiasi kidogo cha pesa mnachopata na jengeni barabara, wekeni shule, hospitali, maji safi na watu hawatakuwa na matatizo.
 
Anadai watu wanayachukulia mauaji hayo kama mtaji wa kisiasa...YEYE kaenda na sare za chama je ule ni mkutano au msiba wa chama cha mapinduzi??? Pili gari la matangazo na vipaza sauti vya nini msibani? Wao wakivaa sare na kufanya siasa misibani na kwenye sherehe za kitaifa ni sawa ila wengine wanavunja sheria. Kunya anye kuku akinya bata kaharisha
 
Lakini waliwaambia wananchi "wakija huko wazomeeni". Kibao kimewageukia wao wenyewe, sasa si wanazomewa tu kama walivyotaka wenzao wazomewe, na mawe wanapigwa pia..:biggrin1:na bado...
 
Alisema walikataa kutoa kibali hicho kwa sababu maandamano yaliyopangwa kufanywa, yanahatarisha amani.
"Tunakiri kwamba hawa ni wahalifu lakini bado ni Watanzania wenzetu ndiyo maana kama serikali tumeamua kutoa msaada wa mazishi," alisisitiza
..... Kagesheki hapa umepotoka ingekuwa ni nchi za watu wewe unatakiwa kujiuzuru...... Mahakama peke yake ndo zinajukumu la kusema nani ni mharifu na kutoa adhabu. Je adhabu ya kufa kwa risasi hayo watanzania ilitolewa na mahakama gani?
 
Watu hawataki kabisa kuona sare za kijani siku hizi! Kwa upande wa CCM ni wenyewe hasa waliotaka kugeuza mauaji hayo kuwa mtaji wa kisiasa maana walivamia mkutano na mijisare yao bila kualikwa!
Kweli kabisa.
 
Mimi nawashangaa sana wakuu wa JF na maoni yao humu jamvini. Pamoja na kwamba siungi mkono vitendo vyovyote vya ukandamizaji vinavyofanywa na dola au/na vyombo vyake, siwachi kujiuliza, mlikuwa wapi Wazanzibari walipokuwa wakipigwa, kuuliwa, kunajisiwa na kadhalika ndani ya nchi yao?

Kuweni fair.


haya tena basi jamani 2.jpg


haya tena basi jamani.jpg
 
Serikali imefikia mahali pabaya,inafikia hatua ya kuua raia wake,napinga kwa nguvu zote mauaji haya yaliyofanywa na jeshi la polisi huko mji mdogo wa Nyamongo wilayani Tarime.
 
Makaimati acha ubinafsi,
wakati mauaji ya zanzibar yanafanyika JF haikuwepo hivyo **** huu haukuwepo wakati huo pia.
lazima unasumbuliwa na ama uzanzibar au uccm.

Unaweza kutuonyesha thread uliyoanzisha juu ya mauaji hayo na watu wakaipotezea au
kutoa kauli za kuyaunga mkono, Mnafiki mkubwa wewe
 
Hiyo BIFU wanayoisuka CCM dhidi ya Wa-Tanzania wa Mkoa wa Mara hivi kweli watauwezaaaaaaaaaaaaaaa?????????????????????

Maana kama majeshi ni wao, polisi hawajiungi isipokua FFU, bunduki ni wao, ngumi kavu kavu ni wao, vita vya mawe ni wao, siasa za chuki ni wao, vinara vya mageuzi ya kweli nchini ni wao na sasa usomi pia umeanza kuwa ni wao ...

Mama yangu, CCM mbona huruma hivi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wana jf naomba niseme siungi mkono watu kuvamia mgodini,lakini serikali ya ccm iltegemea nini inapowafanya wanatarime kuwa watumwa kwenye ardhi yao?haijifunzi migogoro mingi africa inatokana na unyonyaji wanaofanyiwa wazawa ilipo rasilimali kama vile madini yaliyopo tarime?hivi watu wanapoona wanaumizwa wanahitaji kuhamasishwa na nani kama sio ugumu wa maisha ndio umewafikisha hapo?nataka serakali ya ccm ijifunze kuwa migogoro mingi inakuja kwa sababu ukisikia kuna waasi ujue kuna dhuluma inafanyika,wanatarime wameona mgodi huo hauna faida zaidi ya kuwafanya watumwa kwenye nchi yao, kwanza nimesikitishwa kauli ya kagasheki kuwa wananchi wale wamehamasishwa na wanasiasa wa chama fulani cha upinzani,sio kweli hawanufaiki na mgodi na wamekata tamaa,"can't u imagine mtu anakwenda kupambana na mtu mwenye silaha ya moto akiwa amebeba panga?"hamuoni kuwa wamechoshwa?leo mmeu tarime mkimaliza hapo mtaenda wapi tunaomba ratiba,lakini hii hali itaendelea kama watu wanaozungukwa na rasilimali muhimu hawanufaiki "mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu ambao walikuwa wakipigana kupinga utumwa kwenye ardhi yao lakini wakauwawa kama wanyang'anyi" naamini ndio kwanza wamepanda mbegu ya ukombozi katika ardhi yao kwa kuwawa kwa risasi za serikali ya ccm .
 
ni heri kuwa maskini kwa kulinda utu wako kuliko kuwa kuwa na shibe inayodhalilisha utu wako.
 
Back
Top Bottom