"Fix" nyingi za Viongozi wetu mbeleni zinaenda kuua Taifa. Tuwafundishe Historia ya kweli vijana wetu

"Fix" nyingi za Viongozi wetu mbeleni zinaenda kuua Taifa. Tuwafundishe Historia ya kweli vijana wetu

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,153
Reaction score
3,800
1. Madarasa, madawati, hospitali, maji ya Samia. Vya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli havisemwi, kana kwamba hawakufanya lolote.

2. Viongozi wengi Uchaguzi 2020 walipitishwa tuu kwa nguvu nguvu, uwongo unatamalaki, vijana wetu wanaona, kesho na wao watadanganya vivyo hivyo.

3. Kiongozi anahamasisha kukopa hata vinavyowezekana kufanywa na Taifa, mfano kujenga madarasa, madawati nk. Vijana wanafumdishwa ulemavu wa kukaa na kusubiri kuletewa tu.

4.Wawekezaji wanasombwa kuingia nchini kwa kigezo vijana wetu hawana mitaji. Au kufungua Nchi. Aliyeifunga na kivipi hawaambiwi. Hawashirikishwi kujipanga kupata mitaji au kuamua ni nani aje au asije, Wachache walio ndugu na Viongozi ndo wanufaika.

5. Teuzi zimeegama mirengo fulani ambayo ni sumu kwa Umoja wa Kitaifa huko mbeleni. Wanaoona na kujaribu kukemea, wana pewa ofa ya kuwa nje ya nchi au kuitwa "Magaidi"

6. Wengi walipo madarakani Kesho hawatakuwepo, na aina ya sera za uongozi wao siyo zile za Watangulizi wao. Kila anayeingia anaingia na yake. Huu ndiyo uthinitisho tosha wa hoja hii.
 
Sisi hatuwezi kupiga hatua mzee zaidi ya porojo tu,watu wamezaliwa katika nchi masikini na watakufa bado nchi ikiwa ni masikini...hatuwezi kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo abadani abadaaani...
 
Wenzetu wameshaanza kufundisha coding na robotics 🤖 kuanzia ngazi ya primary school sisi bado tunafundishana kuhusu kilimo cha mahindi iringa!
 
Back
Top Bottom