Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilisikia ni Mkombozi Bank........lakini sina uhakika.......ngoja mshana jr aje.......yeye ni muhasibu..........
Fixed account iko poa,jaribisha NMB wana riba nzuri
Benki zote wapo kwa ajili ya faida tu. Mimi niliweka bonus account ya 50m na wanalipa baada ya miezi mitatu. juzi nilifuatilia kujua riba yangu cha kushangaza kwa muda wa miezi mitatu wamenieleza kuwa riba yangu ni 467,000. Mimi nimeona ni upuuzi nimeamua kuchukua fedha zangu nizifanyie shughuli nyingine.
Hivi mnakosaje kazi za kuzifanyia hizo fedha hadi mzitelekeze bank??
Niliweka somo kuhusu treasury bills na bonds. Kama huna matumizi na pesa zako nenda wekeza kule. Fixed deposit huwa benki haziwaambii ukweli Riba halisi ni ndogo mnoo. Na kama mfano ukiona fixed ya miezi mitatu Riba ni asilimia 4 hapo ujue kama uliweka milioni 50 utachopata sio asilimia 4 ya hiyo pesa.
Bali hiyo asilimia 4 ni Riba ya mwaka mzima ko kupata ya hiyo miezi yako mitatu unachukua hiyo asilimia 4 unagawa kwa nne. Ambayo italeta pesa ndogo sana.
Ndo benki zetu hizo za kitanzania wala hawana mda wa kuelimisha watu the best way to earn more with their money.
Bank za wenzetu wanaoitwa bankers ni watu wa umuhimu sana na wanaheshima kubwa mnoo.
Mambo kama haya mngepaswa kuelezwa.
Kuliko kuweka pesa benki bora ukanunua stocks na kutumia ile certificate kuombea mkopo benki kwa biashara yako.
Ni kweli mkuu Sema ndo hivo bank zetu hazina mda wa kuwashauri watu.