Fixed account za benki na utajiri wa haraka haraka

Niliwahi kusoma humu JF kuwa kwenye saccos ukiweka 2.5m baada ya miezi mitatu wanakukopesha 10m. Hii naona imekaa vizuri zaidi kuliko fixed account. Naomba wenye uelewa na hii issue watudadavulie kwa niaba ya wote.
Kuna ukweli mkuu,ila sio utoe million 2.5 then upate millioni 10 labda, ngoja nitoe mfano, kwa mfano ngoja niwape somo kwenye hii saccos,kuna kkkt dayosisi ya kaskazini saccos, hawa ni saccos ambayo ilinivutia utendaji na uwekezaji wake, wame invest sana kwa mfano wana mashamba mbalimbali eg la miti nk na wana bank yao binafsi wana mifugo nk, wao wana masharti simple sana, kujiunga yani kufanya registration ni laki 250000TSH na fomu ni Tsh 50 elfu tu hapo unakuwa mwanachama utafungua account chini wa umiliki wako,

baada ya usajili utakuwa mwanachama na ukikaa miezi mitatu unaruhusiwa kuomba mkopo kwa sharti dogo kabisa kumuomba mwanachama mwenzako wa hiyo hiyo saccos ili akudhamini ukopaji ule na utakopeshwa kulingana na account yako ina kiasi gani lakini wata double mkopo kutokana account yako inasoma kiasi gani, mfano kama una million 5 kwenye account yako basi utapewa MKOPO wa MILION 10 ,kama kwenye account yako una MILION 10 basi utapewa MKOPO wa MILLION 20 kama una MILLION 30 basi utapewa MILLION 60 na riba ni ndogo sanaaa kwa kuwa ni mwana chama, halafu kila vikao mtakavyo kaa kujadili miradi ya saccos na shughuli nyingine basi huwa mnalipwa sitting allowance, pia huwa kuna gawio la faida la mwaka yani kila mwisho wa mwaka dividend inatolewa according to what is read in your account...
 
Nimejifunza vitu hapa nilitaka nikafungue hiyo akaunti ya principle ya 10m kumbe haina faida
 
Think Big brother. 8.4 millions per year ni hela kidogo sana. Hiyo unatakiwa uipate ndani ya mwezi mmoja au chini ya hapo.
 
dah! sio kweli, kila mtu angeziweka benki maana tunavyoogopa risks za biashara ndo mambo yangekuwa murua huko
 
Una biashara gani?
 
Embu nieleweshe Treasury bill ni kitu gan wadau
 
mkuu mbona mi hesabu nimepata 150,000 badala ya 600,000 ?
 

Mkuu unafanyeje hesabu without considering period of time?
 
Mkuu utajiri wa haraka haraka uonaoutaka hauuwezi kupatikana kwa njia ya kuhifadhi Fedha kwenye akaunti za muda maalum bali akaunti ya muda maalum inaweza kukusaidia kutunza fedha kwa muda ili kufikia malengo yako, kwa mfano umepokea malipo ya nyumba yenu ya ukoo mliyoiuza na ww hautaki kuzitawanya fedha zako kwa anasa mara moja basi unaweza kuzihifadhi kwenye akaunti ya muda maalum ukitafakari nini cha kufanya.
Kwa sasa Benki ambayo inatoa riba kubwa kwenye akaunti za muda maalum ni Access Bank wao kwa kiwango cha hiyo Tshs 10,000,000/= kwa miezi 6 wanatoa 9.5%, na hesabu zinakuwa kama ifuatavyo:
Mtaji wako ni Mill 10 na faida ni 9.5% kwa miezi 6
Fanya hivi 9.5% ÷ 100 = 0.095
Kwa kuwa faida inapatikana kwa miezi 6, kinachofuata ni
Miezi 6 ÷ miezi 12= 0.5 hichi ulichokipata
0.5 × 0.095 = 0.0475 sasa hii ni factor utakayoizidisha kwa Tshs Mill 10 ili kujua utapata Tshs ngapi?
0.0475 × 10,000,000 = Tshs 475,000/= hii fedha hauichukui yote kuna kodi ya Serikali inaitwa "with holding tax" yaaani kodi ya zuio ambayo ni 10% ya Hiyo faida utakayo pata, hivyo basi
Tshs 475,000 × 0.1 = 47,500/= kiwango halisi cha kwako ni
Tshs 475,000 - 47,500 = 427,500 hizo ndo fedha zako ww.

Ukiwa na fedha nyingi kwa mfano Billioni 5 akaunti ya muda maalum inaweza kukupa fedha angalau lakini si kwa fedha kiduchu kama hizo ulizokuwa nazo.


Nawasilisha.
 
Kwa wenzetu wenye pesa ya Ukweli wanapata faida mfano umeweka Mil 50
Kwa mwaka unapata faida ya Mil 4.
Aisee lakini ni kwa sababu tu wengi hatujaona fursa..ila kweli niweke ml50 kwa mwaka mzima nipate faida ml4 tuu???nitakua namkosea mungu
 
Aisee lakini ni kwa sababu tu wengi hatujaona fursa..ila kweli niweke ml50 kwa mwaka mzima nipate faida ml4 tuu???nitakua namkosea mungu
Unajua bank [emoji542] nyingi zinaletwa kwa ajili ya watu tofauti tofauti kama mtu ana uwezo wa kufanya biashara ndio anaweka katika fixed deposit. Izi bank account [emoji542] na zenyewe zinafanya biashara. Watu wengi tunakosa elimu ya biashara ndio maana tunalalamika na hata kama unaenda bank unatakiwa kuuliza sana maana wanaweza wanakudanganya ukaweka mkwanja wako kwa muda mwingi kwa faida kidunchu
 
Ndio maana mfanyabiashara kuweka pesa katika fixed deposit uwezi kumkuta anaweka huko kwa sababu anayo elimu ya pesa ni bora akanunua hisa katika soko la hisa (mitaji) la DSE kuliko kuweka katika bank account [emoji542]
 
The only way utakapofaidi fixed account ni kama una bulk money meaning 50m+ but if u have lower than that nenda kanunue hisa DSM stock exchange.
 
The only way utakapofaidi fixed account ni kama una bulk money meaning 50m+ but if u have lower than that nenda kanunue hisa DSM stock exchange.
Ni kweli kabisa mkuu
Sema tatizo lililopo mkuu watu wengi wanachambua kisiasa siasa tuuu. Sisi watanzania tunajua sana siasa kuliko mambo ya siasa. Angalia Uzi kama huu unakuta unachangiwa na watu wachache sana
 

Nenda CRDB Bank wana akaunti ya Thamani na Dhahabu ambazo zinatoa riba kubwa ya 13% ukiwa na Thamani au 10% ukiwa na Dhahabu pia unauwezo wakupata makopo hadi asilimia 80% ya amana zako.

Wasiliana nao upate maelezo zaidi.
 
Nenda CRDB Bank wana akaunti ya Thamani na Dhahabu ambazo zinatoa riba kubwa ya 13% ukiwa na Thamani au 10% ukiwa na Dhahabu pia unauwezo wakupata makopo hadi asilimia 80% ya amana zako.

Wasiliana nao upate maelezo zaidi.
Ni kweli mkuu kuna FD nzuri tu kwa uwekezaji ambao hautokuumiza kichwa kwa riba hiyo ya 13% crdb ukiweka 20ml kila mwezi unakunja 216,000 kama riba yako na unawekewa moja kwa moja katika ac yako ya kawaida
 
Nikiweka milioni 21 NMB Kwa miezi 3 nitapata riba Tsh. Ngapi?
 
Kwa wenzetu wenye pesa ya Ukweli wanapata faida mfano umeweka Mil 50
Kwa mwaka unapata faida ya Mil 4.
Huu ni uvivu wa hali ya juu, uweke bank milioni 50 kwa mwaka faida ya milion 4, wakati unauwezo wa kuweka kwenye biashara milion 5 ukapata kila mwezi milioni 1 sehe ambayo hata haijachangamka, kweli tuna mawazo tofauti, mimi leo unipe milion 20 baada ya mwaka utanishangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…