Iceberg9
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 24,893
- 47,768
Kuna ukweli mkuu,ila sio utoe million 2.5 then upate millioni 10 labda, ngoja nitoe mfano, kwa mfano ngoja niwape somo kwenye hii saccos,kuna kkkt dayosisi ya kaskazini saccos, hawa ni saccos ambayo ilinivutia utendaji na uwekezaji wake, wame invest sana kwa mfano wana mashamba mbalimbali eg la miti nk na wana bank yao binafsi wana mifugo nk, wao wana masharti simple sana, kujiunga yani kufanya registration ni laki 250000TSH na fomu ni Tsh 50 elfu tu hapo unakuwa mwanachama utafungua account chini wa umiliki wako,Niliwahi kusoma humu JF kuwa kwenye saccos ukiweka 2.5m baada ya miezi mitatu wanakukopesha 10m. Hii naona imekaa vizuri zaidi kuliko fixed account. Naomba wenye uelewa na hii issue watudadavulie kwa niaba ya wote.
baada ya usajili utakuwa mwanachama na ukikaa miezi mitatu unaruhusiwa kuomba mkopo kwa sharti dogo kabisa kumuomba mwanachama mwenzako wa hiyo hiyo saccos ili akudhamini ukopaji ule na utakopeshwa kulingana na account yako ina kiasi gani lakini wata double mkopo kutokana account yako inasoma kiasi gani, mfano kama una million 5 kwenye account yako basi utapewa MKOPO wa MILION 10 ,kama kwenye account yako una MILION 10 basi utapewa MKOPO wa MILLION 20 kama una MILLION 30 basi utapewa MILLION 60 na riba ni ndogo sanaaa kwa kuwa ni mwana chama, halafu kila vikao mtakavyo kaa kujadili miradi ya saccos na shughuli nyingine basi huwa mnalipwa sitting allowance, pia huwa kuna gawio la faida la mwaka yani kila mwisho wa mwaka dividend inatolewa according to what is read in your account...