Wacha wee,hawa nishasikia wako vzuri sana, japo sijaelewa je ni lazma kununua vipande au inakua ni unadeposit tu unasubiria riba regardless hali ya soko ilivo
Mana mtindo wa dividends soko likiwa baya inakula kwako
Sijapata doc. ambayo ni current sana but nahisi hii itawapa mwanga.... mengine someni kwenye website yao
MAMBO MUHIMU KUHUSU MFUKO WA KUJIKIMU
• Madhumuni: Mfuko huu ni mpango ulio wazi wenye lengo la kukuza na kutoa gawio kutokana
na mapato ya ziada katika vipindi tofauti na pia kukuza mtaji kwa mwekezaji wa muda mrefu.
• Chaguo la Mpango wa Uwekezaji : Mfuko unatoa fursa mbili za uwekezaji - (a) Mapato ya robo mwaka (b) Mapato ya mwaka yaliyoambatanishwa na ukuaji wa vipande (growth option)
• Nani anaruhusiwa kuwekeza:
Mfuko uko wazi kwa watanzania walio ndani na nje ya nchi, watu binafsi, makampuni/taasisi, mabenki, asasi za kiraia (NGO) n.k. kama inavyoonyeshwa kwenye waraka huu.
• Thamani ya Mwanzo ya Kipande:
Thamani ya mwanzo ya kipande (face value) ni Sh. 100.
• Bei ya Kipande (Issue Price):
Vipande vitauzwa kwa bei ya Sh. 100 kwa kila kipande wakati ya mauzo ya awali (kuanzia 3 Novemba 2008 hadi 29 Novemba, 2008) na baada ya hapo kipande kitauzwa kulingana na thamani halisi.
• Mipango ya mgao wa Mapato:
Mpango wa mapato kila robo mwaka na mpango wa mara moja kwa mwaka wenye gawio na ukuaji.
• Kiwango cha Chini cha Kuwekeza:
Ni Sh. milioni 2 kwa mpango wa mapato ya robo mwaka, na Sh. milioni moja kwa mpango wa gawio kwa mwaka na Sh. 5,000 kwa mpango wa ukuaji wa mtaji kwa mwaka.
• Uwekezaji wa Nyongeza:
Kiwango cha chini cha uwekezaji wa nyongeza/unaofuata
(additional investment) ni Sh.15,000 kwa mpango wowote wa gawio na Sh. 5,000 kwa mpango wa ukuaji wa mtaji kwa mwaka, hakuna ukomo wa kiwango cha kuwekeza
• Ukwasi:
Ununuzi na Uuzaji wa vipande utafanyika kila siku ya kazi kuanzia tarehe 16 Aprili, 2009 yaani miezi minne na nusu baada ya kufungwa kwa kipindi cha mauzo ya awali.
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) itatuma malipo ya mauzo ya vipande ndani ya siku 10 za kazi tangu kuwasilishwa kwa maombi ya mauzo.
• Uwazi:
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) itafanya tathmini na kutangaza thamani halisi ya kwanza ya mfuko (Net Asset Value) katika kipindi kisichozidi siku 60 tangu kufungwa kwa mauzo ya awali na baadaye itatathmini na kutangaza kila siku ya kazi. Hali kadhalika
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) itatoa mgawanyo wa uwekezaji (Investment portfolio) kwa kila robo mwaka.
• Uhamishaji wa Vipande:
Uhamishaji wa vipande kutoka kwenye mfuko mmoja kwenda mwingine kati ya mifuko inayoendeshwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania unaruhusiwa.
Uhamishaji huu utatumia thamani halisi ya kipande kwa wakati huo bila gharama yoyote.
Uhamishaji huo utafanywa kwa mauzo ya vipande kutoka kwenye mfuko mmoja na
kuviwekeza kwa kununua vipande kwenye mfuko mwingine, ilimradi sifa za kuwekeza kwenye mfuko mwingine zimezingatiwa.
• Makato ya Kodi:
Kulingana na sheria za sasa, kodi ya mapato haitotozwa kwenye gawio litokanalo na uwekezaji kwenye mfuko huu.
• Kuorodheshwa:
Kwa sababu ni mfuko uliowazi ambapo manunuzi na mauzo ya vipande yatafanywa wakati wote na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), vipande vya mfuko
havitapendekezwa kuorodheshwa kwenye soko lolote la hisa. Hata hivyo, hapo baadaye
Meneja wa mfuko, baada ya kushauriana na Mwangalizi wa Mfuko na maombi yake kupitishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, ana uwezo wa kuamua kuorodhesha vipande vya mfuko kwenye masoko ya hisa.