Fixed account za benki na utajiri wa haraka haraka

Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’

Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki

‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi

‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika

Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini

Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie

Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali

Signed

Oedipus
Hiyo fixed account mimi naitaka.

Nataka kufungua niweke kiasi cha pesa kila mwezi baada ya miezi 12 ndo nataka kuitoa.

Je hakuna pesa ambayo nitakatwa kama malipo ya kuwalipa kunitunzia pesa ?

Je ikitokea kuna tatizo nikahitaji kutoa pesa kwa muda usiokuwa nimeandika inakuwaje ?

Na je inawezekana nikawaambia benki husika wanikate kwenye mshahara moja kwa moja pale unapoingia uende kwenye fixed account ?

Nijibu hayo niendelee maana ninaitaka hyo fixed account.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba current acc unaweza kutoa pesa zaidi ya uliyonayo, kivipi sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanawake bhana kwa kupenda hela...

Hizo Mara nyingi wanapewaga makampuni mbali mbali ya biashara au ya ujenzi,

Na si kwamba unaruhusiwa tu kujitolea no kuna kuwa na kiwango husika mfano mwisho milioni mia sita,na pia unaweka dhamana mfano gari lenye thamani ya zaidi ya million mia mbili,viwanja na nyumba.

Pia ni kwa kipindi cha mwaka mmoja tu,baada ya hapo unaenda kurenew kiuhasibu inaitwa bank overdraft
 
Ahaa kwahiyo ndo maana Mo Dewji kaweka fedha zinazotumiwa na Klabu ya Simba kwa sasa kwenye hiyo Fixed Account yake kwa msaada wa maelezo ya Haji Manara leo Wasafi.....

Na mimi ni miongoni mwa waliotaka kujua kiundani hiyo fixed account...
Sasa nimeelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’

Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki

‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi

‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika

Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini

Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie

Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali

Signed

Oedipus
Je, kuna muda wa ukomo wa kuweka pesa zangu katika akaunti hii ya fixed? Au naweza kuweka na kuacha zikae kwa muda wowote nipendavyo?
 
Ahaa kwahiyo ndo maana Mo Dewji kaweka fedha zinazotumiwa na Klabu ya Simba kwa sasa kwenye hiyo Fixed Account yake kwa msaada wa maelezo ya Haji Manara leo Wasafi.....

Na mimi ni miongoni mwa waliotaka kujua kiundani hiyo fixed account...
Sasa nimeelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii fixed acc hata serikalini kuna watu wanapiga mpunga mrefu sana kwa kuweka fedha za serikali kwenye accounts binafsi halafu zikishatema faida wanarudisha cha serikali na wao wanabaki na faida.
 
Je, kuna muda wa ukomo wa kuweka pesa zangu katika akaunti hii ya fixed? Au naweza kuweka na kuacha zikae kwa muda wowote nipendavyo?
Mara nyingi zinaanzia miezi mitatu, ila kama ikitokea unataka kuweka zaidi, siku ukienda kuvuna unaweka tena
 
Inakuwa kama umekopa benki bila makubaliano, unairudisha baada ya muda fulani, hiyo ni kwa current accounts tu
Hiyo fixed account mimi naitaka.

Nataka kufungua niweke kiasi cha pesa kila mwezi baada ya miezi 12 ndo nataka kuitoa.

Je hakuna pesa ambayo nitakatwa kama malipo ya kuwalipa kunitunzia pesa ?

Je ikitokea kuna tatizo nikahitaji kutoa pesa kwa muda usiokuwa nimeandika inakuwaje ?

Na je inawezekana nikawaambia benki husika wanikate kwenye mshahara moja kwa moja pale unapoingia uende kwenye fixed account ?

Nijibu hayo niendelee maana ninaitaka hyo fixed account.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea na benki, na kiwango cha riba wanayotoa! riba nyingi najua hazizidi 10%
Hiyo fixed account mimi naitaka.

Nataka kufungua niweke kiasi cha pesa kila mwezi baada ya miezi 12 ndo nataka kuitoa.

Je hakuna pesa ambayo nitakatwa kama malipo ya kuwalipa kunitunzia pesa ?

Je ikitokea kuna tatizo nikahitaji kutoa pesa kwa muda usiokuwa nimeandika inakuwaje ?

Na je inawezekana nikawaambia benki husika wanikate kwenye mshahara moja kwa moja pale unapoingia uende kwenye fixed account ?

Nijibu hayo niendelee maana ninaitaka hyo fixed account.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Benki nyingi zinaanzia laki 5

Back
Top Bottom