safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Hiyo fixed account mimi naitaka.Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’
Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki
‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi
‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika
Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini
Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie
Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali
Signed
Oedipus
Nataka kufungua niweke kiasi cha pesa kila mwezi baada ya miezi 12 ndo nataka kuitoa.
Je hakuna pesa ambayo nitakatwa kama malipo ya kuwalipa kunitunzia pesa ?
Je ikitokea kuna tatizo nikahitaji kutoa pesa kwa muda usiokuwa nimeandika inakuwaje ?
Na je inawezekana nikawaambia benki husika wanikate kwenye mshahara moja kwa moja pale unapoingia uende kwenye fixed account ?
Nijibu hayo niendelee maana ninaitaka hyo fixed account.
Sent using Jamii Forums mobile app