Flora Mbasha, amekimbilia mahakama ya hakimu mkazi Kisutu

Flora Mbasha, amekimbilia mahakama ya hakimu mkazi Kisutu

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Inili, Flora Mbasha, amekimbilia mahakama ya hakimu mkazi kisutu, akiomba kuvunja ndoa kati yake na mumewe, Emmanuel Mbasha. Flora anadai sababu za kuomba kuvunja ndoa hiyo apewe talaka ni kutokana na tabia ya mumewe kumpiga, kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.

Una lipi la kuwaambia wanandoa hawa?

vipi mimba ya Gwajima inaendeleaje? kijusi kinaendelea kukua? ukute anataka kuvunja ndoa ili ahalalishe uchepukaji wake na huyo pastor wake.
 
Kwani hiyo ndio ilifungwa mahakamani? Akimbilie kwa Mungu amuombe kama ataivunja coz alifunga yeye ...
 
Hawana jipya,waendezao huko. Sasa mahakama si dhani kama inavunja ndoa. Bali hutenganisha wanandoa pale panapojitokeza hali ya hatari kati yao. Ndoa ya kikristo haivunjwi isipokuwa kifo pekeee!!!!

Zipo taratibu ukizifuata Mahakama wanaiuvunja NDOA hata km niyakidini lkn Inafuata Sheria za NCH
 
Hawajaomba ushauri ila weye ndo unawaombea ushauri. Ka vip Flora angeomba ushauri kabla kuingia kwa Pilato. Ameshaona haki yake iko huko kwa Pilato. Tuwaache wajiaibishe kwanza. Kwani hawajui kuwa biblia imewanyima kwenda kwa Pilato??
Hawa vip banaa?? Walipokuwa wanapeana kiss by kiss wakivungana kuwa hadi kifo, leo wanaona Pilato ndo kifo cha kuwatenganisha?? Ujinga mwingine si lazima usome vidato. Wazaliwa nao tuu
 
halafu kuna wakati haka kadada kakawa kanafikiria kuingia kwenye siasa eti kagombee ubunge kupitia ccm... ila kwa ccm ni chaguo muafaka kwake akaungane na akina Ghasia maana wote wanaghasia kweli kweli
 
Mkuu kweli GASIA ana GASIA.Unafaa uwe Padri au Sheikh mkuu wa DUNIA.
 
Huyo hajui kuwa hakuna cheti cha ndoa cha dini...vyote ni vya serikali...
Mahakama inavunja tu...hayo maagano mengine ni ya wanandoa na Mungu....watakuwa na kesi nyingine siku ya hukumu mbinguni...

Zipo taratibu ukizifuata Mahakama wanaiuvunja NDOA hata km niyakidini lkn Inafuata Sheria za NCH
 
halafu kuna wakati haka kadada kakawa kanafikiria kuingia kwenye siasa eti kagombee ubunge kupitia ccm... ila kwa ccm ni chaguo muafaka kwake akaungane na akina Ghasia maana wote wanaghasia kweli kweli

Te te te na hiyo ni dalili kwamba kana tamaa...ameona za kwaya hazitoshi ajisogeze kwa wazee wa mjengoni...na ana kila sifa as long as viti maalumu havitafutwa...
 
Huyo hajui kuwa hakuna cheti cha ndoa cha dini...vyote ni vya serikali...
Mahakama inavunja tu...hayo maagano mengine ni ya wanandoa na Mungu....watakuwa na kesi nyingine siku ya hukumu mbinguni...

mkuu upo sawia,ukiisoma vizuri ile sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inatamka wazi kuwa ni mahakama PEKEE ndio ina uwezo wa kutoa talaka baada ya kuwepo sababu kadha wa kadha ambazo mahakama itajiridhisha kuwa haina budi kutenganisha ndoa husika.
 
kumshinda shetani ndani ya ndoa si kazi ndogo na mtumishi halisi wa Mungu ni yule anayeishi kwa kufuata neno la Mungu na kulitendea kazi,"aliyekiunganisha Mungu,mwanadamu asikitenganishe" je Frola anafuata hili andiko na kulitendea kazi? je ni mtumishi halisi kwa hiki anachotaka kukifanya sasa? Tafakari,Chukua hatua.
 
Kwani hiyo ndio ilifungwa mahakamani? Akimbilie kwa Mungu amuombe kama ataivunja coz alifunga yeye ...

Umesahau kuwa ndoa ni mktaba wa kisheria? Kwa kuwa kisheria ni mkataba basi usishangae yeye kuomba kibali cha Mahakama ili kutengua huo Mkataba.

Pili, inaonekana kuna mchanganyiko wa hoja hapa,lkn kama ni kwelu Flora anadai talaka, Kibiblia siamini kama amefanya dhambi ili mradi aishi kama mtu ambaye hajaolewa [ asishiriki mambo ya kindoa].

Vv
 
.........Nafuu adai talaka tu, kitendo walichofanya yeye na mumewe kujianika siri zao nje aibu kuishi pamoja.

Sidhani kama hiyo ndoa itabaki ndoa kweli...........humo ndani kila mtu atamuangaliaje mwenzake?

Ndoa ikashafika hatua kama hii, hapo ndani ya nyumba hakuna amani. Solution ni kuachana tu.
 
Hawawezi kuelewa .......mtu anahubiri alafu mwisho anasema nani ambaye "HAJAOKOKA" anataka "KUOKOKA" .......baada ya hapo anaambiwa sema maneno yafuatayo .........mtu akishasema maneno hayo anaambiwa "AMEOKOKA" .........What a joke? .........kuna wokovu kabla ya kubatizwa? Kimsingi hapo mtu ameamini kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye wokovu.....then anabatizwa kama hatua nyingine kuelekea kwenye wokovu ........baada ya hapo anapaswa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu hata mwisho ili AOKOKE .......huwezi kutumia neno zito kuwa UMEOKOKA alafu kesho unaanguka dhambini .....ukianguka unaokoka tena baada ya kutubu?

Unasikia mhubiri anasema waliookoka tu ndio wataenda mbinguni ........anasahau kuwaambia ukweli kuwa watakaoishi maisha ya kumpendeza Mungu hata mwisho ndio Watakaokoka .........Wokovu ni ushindi wa mwisho wa Mkristu baada ya kushinda dhambi maisha yake yote hapa duniani ..........

Nakubaliana nawe mkuu,watu wengi hawasomi maandiko na kuyaelewa.Baadhi ya viongozi wa dini hasa hawa mitume wetu wa mjini ndo wapotoshaji wakuu wa maandiko.
 
Back
Top Bottom