Floyd Mayweather ajipongeza kwa ushindi

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Hatimaye bondia machachari na mwenye pesa, alieweka rekodi ya kutopigwa kwa mapambano ya ngumi 50, amejipongeza kwa kushinda pambano lake la mwisho na McGregor ambae ni bingwa wa UFC, kwa kununua jumba la kifahari huko Beverly Hills nchini Marekani..pambano hilo lilimuingizia Mayweather zaidi ya hela ya kitanzania Bilioni 225, na hakupoteza muda kuitumia hela yake hio aliyopata kwa kujipongeza.

Jumba hilo amelinunua kwa shilingi Bilioni 60 za kitanzania. Mayweather pia ametumia zaidi ya Bilioni 1 za kitanzania kufanya tu furnishing ndani ya nyumba yake hio mpya.

Jumba hilo lina ukumbi mkubwa wa kuangalia sinema, vyumba vya wageni, na sehemu nzuri ya kustarehe nje ikiwemo sehemu nzuri ya kuogelea.

Hii ni kwa ufupi tu, unaweza kuangalia zaidi picha hapo chini.

Everything is possible if you put your mind on it.


















 
Hapa ndipo sometimes uwa ninahisi kuna maisha mara nyingine, yani ukifa unazaliwa kwingine na maisha mengine.
Haimake sense juma anaishi Tanzania ana maisha magumu ni kibaka ana madhambi tele, halafu mayweather yuko states ana maela mengi na anafanya kufuru na uzinzi naye ana madhambi pia halafu eti wote wakifa waende motoni wakati mmoja duniani alikula raha mwingine aliishi kwa tabu.
 
Hayo ni matokeo ya bidii na kujituma.
Zaidi ya hapo mtaishia kulalamika na mtakufa mkingali mafukara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…