Floyd Mayweather ampiku Muhammad Ally

Floyd Mayweather ampiku Muhammad Ally

Sijawahi kumpenda lenox Lewis ila kipindi chake aliwadunda hao kina evander na wenzake mpaka akastaafu kwa kukosa mpinzani..sasa kwenye list simuoni sasa huo kama sio ubwege kitu gani
 
Nakubaliana na wewe, mimi Ally hawajawahi kunivutia, sijaona kama alikua special kwenye Ngumi. Media attention na ile uanaharakati ndio uliompa jina ila hakua mzuri kabisa. Enzi zake kulikua na watu wazuri sana kina Smoking Joe, Joe Frazier nk. Labda ubora wa kukwepa makonde.

Mimi kwangu Tyson angekua namba moja. Money nae hana kitu zaidi ya media attention ila sio mbaya.
Umezaliwa 2000 Ali atakuvutia vipi?
 
Sijawahi kumpenda lenox Lewis ila kipindi chake aliwadunda hao kina evander na wenzake mpaka akastaafu kwa kukosa mpinzani..sasa kwenye list simuoni sasa huo kama sio ubwege kitu gani
Unaposema kukosa upinzani unamaanisha nini?
Binafsi Lennox Lewis alikuwa njema sana lkn alishawahi kupata joto la jiwe toka kwa Hasim Rahman na Oliver McCall.
Hata mie nashangaa kutomuona ktk list hii!
 
M. ally anamzidi Mayweather kuandika na kusoma. Kusema hakuna kitu Ally anamkalisha May ni uongo!!
 
Ngumi za enzi hizo ndio zilikuwa burudani haswa.. sio za miaka hii

Ally bado atazidikuwa juu ya wote kwa wengine na sie
 
List hyo ni fake inaweka hw na lw kwa pamoja haiwezekani, KWANZA KABISA KAMA MIKE HAYUPO HIYO NI RUBISH KABISA, Mike Iron Tyson is the greatest boxer to ever happen, on his prime No one on that list could ever defeat him...OVA
 
Mkinisaidia ukokotozi wa hzo point kulingana na mapambano (W-L-D) nafikr hapo tunaweza kuanza kuwajadili.
 
Eti ???
Kwanza Floyd anapigana Middle weight wakati Ali alikuwa anapigana Heavy Weight huoni kama anafanya comparison ya vitu visivyoendana,
Angefanya comparison ya Mike Tyson na Mohamed Ali tungemuelewa kidogo sababu hao wote walikuwa wanazipiga ndondi za uzito wa juu
Cha kushangaza Mike Tyson hayupo kwenye hiyo list
Unapozungumzia boxing usipowataja Tyson na Mohamed Ali ni sawa unapozungumzia boli bila ya Pele na Maradona
Mkuu hii list yake ni Fake kabisa
 
Bondia asiyepigika Floyd Sinclair Joy Money Mayweather Junior azidi kupaa tu kila kukicha japo ma haters nao hawakosekani.

Kwa muda mrefu Muhammad Ally ndiye alikuwa akipewa title ya GOT kwenye boxing lakini binafsi nilikuwa sikubaliani kabisa na hiyo title kupewa Muhammad Ally badala yake hiyo title nilikuwa naona kabisa inamfaa Floyd bila kupepesa macho au kumumunya maneno maana hakuna chochote alichokuwa nacho Ally kumzidi Floyd zaidi ya upendeleo tu.

Sasa hatimaye watafiti wamekaa chini na kuchambua vilivyo mabondia na kuja na listi hii inayoonesha mabondia bora wa muda wote na nafasi ya kwanza imeshikiliwa na Floyd Mayweather na kuwaacha mbali wapinzani wake akiwemo Canelo Alvarez ambaye hayumo hata 50 bora.

View attachment 1180301
Huwezi kuchanganya light weight na heavy weight, licha ya hayo Mike Tyson anakosekanaje hata top 20.
 
Wanalinganisha watu waliokuwa wakicheza round 15 na hawa round 12,Mohamed Ali fundi yule jamaa,katafute pambano la Thrila in Manila alilopigana na Joe Fraizer au lile alilopigana na George Foreman Kinshasha hapo.
hili pambano nilipolitazama nilibadili msimamo wangu na kumuweka ali juuya tyson,ali anapigana vizuri mpaka raha
 
Bondia asiyepigika Floyd Sinclair Joy Money Mayweather Junior azidi kupaa tu kila kukicha japo ma haters nao hawakosekani.
Kwa muda mrefu Muhammad Ally ndiye alikuwa akipewa title ya GOT kwenye boxing lakini binafsi nilikuwa sikubaliani kabisa na hiyo title kupewa Muhammad Ally badala yake hiyo title nilikuwa naona kabisa inamfaa Floyd bila kupepesa macho au kumumunya maneno maana hakuna chochote alichokuwa nacho Ally kumzidi Floyd zaidi ya upendeleo tu.
Sasa hatimaye watafiti wamekaa chini na kuchambua vilivyo mabondia na kuja na listi hii inayoonesha mabondia bora wa muda wote na nafasi ya kwanza imeshikiliwa na Floyd Mayweather na kuwaacha mbali wapinzani wake akiwemo Canelo Alvarez ambaye hayumo hata 50 bora.
View attachment 1180301

Lile jamaa la kuitwa wilder halipo kwenye list..lile lijamaa lina roho mbaya balaa sijui wanaopigana nalo wanajiamini nini kudadeki
 
Back
Top Bottom