Floyd Mayweather anunua jumba la thamani ya billion 46.14

Floyd Mayweather anunua jumba la thamani ya billion 46.14

Mzee makoti

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Posts
3,482
Reaction score
4,673

masumbipicc

Mayweather, ambaye ni promota wa ngumi na bondia wa zamani, amenunua jumba hilo katika kisiwa cha Palm Island na lina vyumba tisa vya kulala na mabafu 10.

Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather, ambaye amejipachika jina la "Money (fedha)", amenunua jumba la kifahari lililoko kisiwa cha Palm, likiwa na vyumba tisa vya kulala na mabafu kumi, magazeti ya Marekani yameripoti.

Miongoni mwa vitu vingine vilivyoko katika jengo hilo la Mayweather, 44, ambaye amestaafu ngumi, ni ukumbi wa sinema, gym, bwawa la kuogelea na bei yake ilikuwa dola 19.9 milioni za Kimarekani (sawa na Sh46.14 bilioni za Kitanzania.

Jumba hilo liko katika eneo la ukubwa wa futi 10,853 za mraba,

"Baada ya uporaji benji uliohalalishwa, Floyd Mayweather anunua jumba kubwa Miami Beach," limeandika gazeti la Miami Herald, wakati tovuti ya realtor.com imeripoti habari hiyo ikisema "Floyd Mayweather amelipiga knockout jumba la Miami Beach kwa dola 18 milioni" na tovuti ya New York Post (nypost.com) imeandika "Floyd Mayweather aongeza jumba la dola 18 milioni Miami Beach katika orodha ya nyumba zake nyingi".

Miongoni mwa mali anazomiliki ni jumba la thamani ya dola 26 milioni lililoko California likiwa na ukuta wa mvinyo na jumba jingine lililoko Las Vegas la thamani ya dola 10 milioni, tovuti ya nypost.com imeripoti.

Katikati ya mwaka, Mayweather aliripotiwa kukusanya takriban dola 10 milioni kwa kushiriki pambano lake la maonyesho dhidi ya nyota wa YouTube, Logan Paul kwenye uwanja wa Hard Rock. Pambano hilo liliisha bila ya mshindi, ingawa Mayweather alizawadiwa malipo mazuri kwa kushiriki.

“Naamini katika kufanya kazi kwa uangalifu, si kwa juhudi. Kwa hiyo kama kitu ni rahisi, kama uporaji benki uliohalalishwa, nitaufanya, lazima niufanye,” alisema Mayweather katika kipindi cha Showtime cha “Inside Mayweather vs. Paul".

Mayweather alinunua jumba hilo kwa kutumia kampuni ya Fojoso LLC.

Jumba hilo lina ghorofa tatu likiwa na paa la ukubwa wa futi 5,000 za mraba.
 
FIoyd money myweather hate or love him, utafikiri kazaliwa kwetu Mbagra Chambre kwa sifa.
Kununua majumba ya kifahari kama hayo sio kupoteza hela,hayo majumba na ardhi yake baada ya miaka 5 yanapanda bei zadi ya aliyonunulia,kwahiyo bado anajitahidi kuwekeza,ila hela ya ngumi ni ngumu sana,unapata pesa kwa kupigwa hii ni hatari sana,pamoja na kuwa anashinda lakini kuna ngumi ambazo zinampata na hata kumhatarishia maisha yake,cha kujifunza ni kuwa hakuna pesa rahisi...
 
Sure, hakuna pesa rahisi
 
Wapi nimesema kapoteza pesa?
 
Back
Top Bottom