Kufanya uchaguzi kwa pesa ya ndani, kujenga flyovers, SGR na uboreshaji wa miundombinu unaofanywa na awamu ya 5 ni matokeo ya kubadili matumizi pesa/kipato tu sio kukua kwa uchumi. Mfano, pesa zilizokuwa zinatumika kulipa mishahara kwa watumishi wa umma. Sasa wanastaafu, wengine wanakufa hakuna ajira mpya pesa ndiyo hizo zinakwenda kwenye zoezi la uchaguzi. Nyongeza za mishahara haifanyiki pesa ndizo kwenye maflyover. Wafanyabiashara wananyonywa through kodi pesa ndiyo hizo kwenye madenge.
Kwa manufaa ya bendera fuata upepo natumia mfano mwepesi sana ili hata wale wagumu kuelewa waelewe. Ukiwa na kipato cha 1m Tzs kwa mwezi, kila mwezi tunatumia sehemu ya pesa hiyo laki 5 chakula, laki 2 bia, laki 3 matumizi mengine. Ukiamua kubana matumizi kwenye chakula na bia ukatumia hiyo pesa kujenga nyumba hapo kipato (uchumi) kwenye familia hakijaongezeka ila umebadili matumizi ya pesa. Ingizo la 1m kwa mwezi litabaki palepale.
Hata hivyo, kubadili matumizi kunaweza ongeza pato, mfano kama pesa hiyo ingetumika kujenga viwanda watu wakapata ajira na uzalishaji ukaongezeka. Lakini kujenga daraja na madenge ambapo mwisho wa mwaka kuna hasara uchumi hauwezi kua hata siku moja ni kujidanganya tu tuko kwenye uchumi wa kati.
Nimetumia lugha nyepesi ili wale wenzangu bendera fuata upepo waelewe.