Fm academia kutua london?

Fm academia kutua london?

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2007
Posts
2,257
Reaction score
363
Chanzo changu cha kuaminika kinanidokeza kuwa- wazee wa mujini, wazee wa bling bling, wazee wa pamba, wazee wa ngwasuma, toka jumatatu wamekuwakuwa wakiingia na kutoka katika ubalozi wa UK bongo katika jitiada zao za kufuatilia visa ili waweze kufanya show ndani ya UK. Kuna tetesi kuwa zoezi la utoaji visa limekuwa gumu kutokana na idadi kubwa ya wakongo wanaounda kundi hili. Kuna hisia kwamba wengi wataingia mitini na kuclaim asylum punde watakapotua hapa kutokana na machafuko ya hali ya kisiasa yanayoendelea nchini kwao.
 
tueleze vizuri bana,wazee a ngwasuma ndio nani?wataonyesha show uk,yaani hawa kama ze-comedy au,by the way your location is 10 dawning street,should it not be 10 downing street-just curious
 
Baada ya hawa jamaa kuja UK nadhani wale wa Zeutamu watakuwa na picha nyingi....kuabisha watu wakijimwaga na Ngwasuma wazee wa Mujini....
 
Baada ya hawa jamaa kuja UK nadhani wale wa Zeutamu watakuwa na picha nyingi....kuabisha watu wakijimwaga na Ngwasuma wazee wa Mujini....

Ndio maana the utamu inaitwa 'mtambo wa kurekebisha tabia', everyone will be at their best behaviour!
 
Hii issue imeshakuwa confirmed, watakuwa Birmingham tarehe 11.04 na Reading watapiga siku inayofuata. Wadau wa UK tutangwasumika kipindi cha pasaka kwa kwenda mbele.
 
Hii issue imeshakuwa confirmed, watakuwa Birmingham tarehe 11.04 na Reading watapiga siku inayofuata. Wadau wa UK tutangwasumika kipindi cha pasaka kwa kwenda mbele.

SASA,kwanini wanaishia birmingham na reading,sasa london ina maana hatutawaona?
 
- Haya wakulu tukutane huko London kwa wazee wa ngwasuma, wazee wa mujini kina Kitokololo, pablo Masai, Jose Mara, na Mkulu Nyoshe El-Sadat "Sauti ya Simba" chini ya Predjshee Mkulu Wangu Martin Kasyanju, Duh! wallahi itakuwa XXL siku hiyo na hawa wazee wa funika bovu.

I will be right there, vipi wakulu mtakuwepo? Tukutane huko jamani I am down.

FMES!
 
FEMES kumbe nawe umo eenh? Mimi show ya reading nitaisafiria, Birmingham is too far from where I live. Nahisi pia kutakuwa na show ya London lakini hawa mapromota hawataki kuitangaza. Tutafutane kwa mtakaokuwa Reading.
 
- Mkuu hawa ndio hasa watu wangu baada ya "kufa" kwa Kamanyola ya Mbuya Makonga, Kassongo na kina Vumbi Kahanga, Dekule na ni mimi ninayewanunulia sana spare za vyombo vyao na hasa studio yao, maana owner Martin ni ndugu yangu, kwa hiyo tupo pamoja mkuu huko, au?

FMES!
 
Mizengwe ya visa inawezekana walikuwa wanataka kujua taarifa zaidi,kwani kuna wimbi la wasaani au mabondia kubeba unga kupeleka ulaya. kuna kizazi kipya tayari waingereza wamemkamata.

tunaharibu wenyewe jina zuri la nchi yetu.hizi ni tamaduni za Africa Magharibi.
 
Mizengwe ya visa inawezekana walikuwa wanataka kujua taarifa zaidi,kwani kuna wimbi la wasaani au mabondia kubeba unga kupeleka ulaya. kuna kizazi ya tayari waingereza wamemkamata.

tunaharibu wenyewe jina zuri la nchi yetu.hizi ni tamaduni za Africa Magharibi.

mkuu,hebu mwaga hizi taarifa za huyu kizazi kipya waingereza waliemkamata..mbona unatuzuia haki yetu ya kikatiba ya kupata taarifa jamaa yangu?
 
Wakifika huko waambieni wafikirie kuvuka Atlantic watue hapa nyumbani kwa Obama.
Mashabiki wa FM tupo.
 
- Mkuu hawa ndio hasa watu wangu baada ya "kufa" kwa Kamanyola ya Mbuya Makonga, Kassongo na kina Vumbi Kahanga, Dekule na ni mimi ninayewanunulia sana spare za vyombo vyao na hasa studio yao, maana owner Martin ni ndugu yangu, kwa hiyo tupo pamoja mkuu huko, au?

FMES!

Tukijaaliwa inshalaah, lakini naona kama tangazo limekuwa rushed kwa Michuzi kwa kuwa naongea na mmoja wa wanamuziki nyota wa kundi hilo na anasema hadi sasa bosi wao hajawaambia chochote kuhusu safari hii, hata wao wanashangaa kuona matangazo tu, anasema pia kwamba passport zao toka zilipopelekwa ubalozini hazijarudi. Jaribio la kwanza la kuomba visa lili fail kwa kuwa kuna mambo sponsors walikuwa hawaja cover.
Martin nduguyo ni yule kibosile wa TANESCO?
 
Jaribio la kwanza la kuomba visa lili fail kwa kuwa kuna mambo sponsors walikuwa hawaja cover.
Martin nduguyo ni yule kibosile wa TANESCO?

- Sawa sawa mkuu, siku hizi hayupo tena kule Tanesco, uanjua yeye ndiye mtu wa kwanza kupinga Netgroup kuingia kule, aliandika paper moja nzito na saafi sana ya kuwakataa, ile pepar ikapelekwa kwa Mkapa akiwa rais, akawapa amri wakuu wa Tanesco kuhakikisha wanamuondoa when the time is right, akasumbuliwa sana na kufukuzwa na kurudishwa, mwisho wakamuhamishia Shinyanga, lakini hayakuisha matatizo kila siku, akaamua kuhachana nao recently na kushika hatamu ya hii bendi yake, ambayo siku zote ilikuwa akisimamiwa na sister wake, kama unakumbuka longtime ago alikuwa anamiliki MK. Group ya kina Kassongo Mpinda, akishirikiana na Papa Msilwa Baraka, baadaye ndio waka-split na Papa akanzisha Twanga ya kina Mkulu Generale Banzastone wazee wa Mwananyamala na Ali Choki. Martin akanzisha FM Academia na sasa Acudo pia.

- Sasa ngoja nimtwangie kujua kama wanakuja au, in 20 minutes nitakuwa na jibu la uhakika toka kwake.

FMES
 
Back
Top Bottom