Foleni ya Buguruni ni janga la kimkoa, serikali mko wapi?

Situmekubaliana serikali imehamia dodoma ama? mbona mnalalamika inamaana bado mji huo una foleni? aisee basi sawa, jiwe oyee, aliwaaminisha anahamisha serikali kuondoa foleni etc. apumzike kwa amani shujaa wa chattle
[emoji23]
 
Hiyo foleni inatengenezwa makusudi na trafik mkoa wa ilala ili magari yatanue wakupige fine .wanamake sana hela hao na ushahidi upo
Mpaka saa nne usiku unakuta traffic anaongoza magari wameshafanya mrija wao was kuchukua pesa
 
na wewe kwanini unakaa Buguruni? huko hata mkuu wa mkoa hajawahi kufikiria kutembelea
 
Tatizo hakuna kiongozi mkubwa anaekaa mitaa hiyo... miaka nenda rudi tazara ni tatizo kubwa na hakuna ufumbuzi... wamejichimbia zao masaki wanakula upepo wa bahari..
Wanajenga daraja pale salendar tena wakati huku buguruni foleni kichefuchefu haswaaa!!
 
Hapo kuna haja ya flying over,kutoka Buguruni mataa,hadi kule mbele ya Tazara,la sivyo watu watakaa kwenye foleni hadi mtaomba Mungu sana
Kuna flyover ya tren pale kati sijui watadesign vipi
 
Ile flyover hata haisaidii,pitia pale ukitokea ubungo mida ya saa nne usiki hiyo foleni ya malori ni balaa
 
Pale kuna shida kubwa mbili:--
1/. Malori mengi mno yanayoenda na kutoka bandarini yanasababisha msongamano. Yangewekewa utaratibu wa kuingia bandarini usiku tuu.
2/. Traffic police wanasimamisha magari muda mrefu mno ili watu wachoke kusota kny foleni watanue, halafu wao wanavuna tu mkwanja wa rushwa toka kwa watanuaji kilainiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…