Foleni ya Buguruni ni janga la kimkoa, serikali mko wapi?

Hili suala la Buguruni foleni naona serikali imeamua kufumbia macho kabisa.

Hapa nazungumza nimekaa kwenye gari karibia masaa mawili kiasi cha kutamani kushuka niiache gari yangu nichukue bodaboda lakini sina chaguo.

Haya mateso hadi lini? Gharama za mafuta kipengele, traffic wanavyotukata faini kipengele, na foleni nayo kipengele hakuna kitu kigumu nchi hii kama kumiliki gari ni mateso tu.

Turudi kwenye mada hili suala la Buguruni kwanini serikali imelikalia kimya? Kwanini ni buguruni tu ndo pamekua sugu namna hiyo?

Pale Tazara hamna tatizo ijapo ilitakiwa kuwe na flyover mbili juu badala ya hiyo moja lakini ndugu zangu hapa Buguruni pameshindikana kabisa sijui solution ninini na serikali imekaa kimya tu.

Siku hizi imefika mahali mtu ukiwaza kupita njia ya buguruni ukiikumbuka foleni ya pale unahisi kuchoka kabisa
Nunua ndege au "hedikopta"!Acha kulalama ustaadh!😝😝😝😝
 
Buguruni hapafai kabisa.. kuna siku mpka nakuja kuvuka Tazara masaa mawili yalipita. Kiukweli hiyo barabara siku hizi huwa natafuta alternative tu, haifai.
 
Gari lenyewe vitisi??
Sisi wenye fankago hatuongei
 
Hili suala la Buguruni foleni naona serikali imeamua kufumbia macho kabisa.

Hapa nazungumza nimekaa kwenye gari karibia masaa mawili kiasi cha kutamani kushuka niiache gari yangu nichukue bodaboda lakini sina chaguo.

Haya mateso hadi lini? Gharama za mafuta kipengele, traffic wanavyotukata faini kipengele, na foleni nayo kipengele hakuna kitu kigumu nchi hii kama kumiliki gari ni mateso tu.

Turudi kwenye mada hili suala la Buguruni kwanini serikali imelikalia kimya? Kwanini ni buguruni tu ndo pamekua sugu namna hiyo?

Pale Tazara hamna tatizo ijapo ilitakiwa kuwe na flyover mbili juu badala ya hiyo moja lakini ndugu zangu hapa Buguruni pameshindikana kabisa sijui solution ninini na serikali imekaa kimya tu.

Siku hizi imefika mahali mtu ukiwaza kupita njia ya buguruni ukiikumbuka foleni ya pale unahisi kuchoka kabisa
Acha gari panda boda
 
Ikishafika mida ya kuanzia saa kumi jioni, hiyo kamba haitamaniki....suluhu ni kuzuia malori yanayotoka bandarini yapite kuanzia saa 12 jioni....
 
Inaweza saidia kweli nadhan wangejenga na njia za mchepuo kuna njia moja inatokea buguruni sokon ni njia ya mtaan ile ingewekwa vizuri ingeasaidia sn
Moja ingechepukia pale kwenye ma hardware ukitokea Matumbi ikatokee Rozana nyingine itokee CUF ikatokezee relini kabla ya flyover
 
Maoni mengi,ila mimi kwa mfano halisi wa ubungo roundbout wakati wa kujenga ile fry over tuliona.
Wazo la kuiweka roundbout naona wengi wana shauri basi TANROAD waangalie wafanye hata kwa kuiua shell ya buguruni tatizo liishe.
Mawazo yangu.
 
Daraja la mfugale halikuwa na umuhimu kama ring road za Tabata dampo na buguruni.. Lakini hizo hazikujengwa tukaenda kujenga kivuko cha waenda kwa miguu buguruni utadhani wao ndio wanasababisha foleni
 
Abiria wa daladala Wana haki ya kulalamikia foleni kwasababu daladala zimepangiwa njia lkn mtu mwenye gari binafsi? Aidha huijui Dar es Salaam vizuri ama una hamu tu ya kukaa kwenye foleni.
 
Sio mkoa tu kumbuka kuna gari nyingi zinaingia na kutoka via hiyo njia kwenda mikoani
 
Hili suala la Buguruni foleni naona serikali imeamua kufumbia macho kabisa.

Hapa nazungumza nimekaa kwenye gari karibia masaa mawili kiasi cha kutamani kushuka niiache gari yangu nichukue bodaboda lakini sina chaguo.

Haya mateso hadi lini? Gharama za mafuta kipengele, traffic wanavyotukata faini kipengele, na foleni nayo kipengele hakuna kitu kigumu nchi hii kama kumiliki gari ni mateso tu.

Turudi kwenye mada hili suala la Buguruni kwanini serikali imelikalia kimya? Kwanini ni buguruni tu ndo pamekua sugu namna hiyo?

Pale Tazara hamna tatizo ijapo ilitakiwa kuwe na flyover mbili juu badala ya hiyo moja lakini ndugu zangu hapa Buguruni pameshindikana kabisa sijui solution ninini na serikali imekaa kimya tu.

Siku hizi imefika mahali mtu ukiwaza kupita njia ya buguruni ukiikumbuka foleni ya pale unahisi kuchoka kabisa
Watatenga bajeti mwaka wa fedha ujao kujenga hilo eneo hapo.
 
Back
Top Bottom