Foleni ya Buguruni ni janga la kimkoa, serikali mko wapi?

Nunua ndege au "hedikopta"!Acha kulalama ustaadh!😝😝😝😝
 
Buguruni hapafai kabisa.. kuna siku mpka nakuja kuvuka Tazara masaa mawili yalipita. Kiukweli hiyo barabara siku hizi huwa natafuta alternative tu, haifai.
 
Gari lenyewe vitisi??
Sisi wenye fankago hatuongei
 
Acha gari panda boda
 
Ikishafika mida ya kuanzia saa kumi jioni, hiyo kamba haitamaniki....suluhu ni kuzuia malori yanayotoka bandarini yapite kuanzia saa 12 jioni....
 
Lianze kunyanyukia mbele ya daraja la treni kuelekea buguruni mataa itasaidia magari kujongea kwa haraka
Tazara pia bado ni shida panatakiwa lingine la juu kama ubungo
 
Inaweza saidia kweli nadhan wangejenga na njia za mchepuo kuna njia moja inatokea buguruni sokon ni njia ya mtaan ile ingewekwa vizuri ingeasaidia sn
Moja ingechepukia pale kwenye ma hardware ukitokea Matumbi ikatokee Rozana nyingine itokee CUF ikatokezee relini kabla ya flyover
 
Maoni mengi,ila mimi kwa mfano halisi wa ubungo roundbout wakati wa kujenga ile fry over tuliona.
Wazo la kuiweka roundbout naona wengi wana shauri basi TANROAD waangalie wafanye hata kwa kuiua shell ya buguruni tatizo liishe.
Mawazo yangu.
 
Acha Uongo office ya mkuu wa mkoa ipo hapo ilala Boma sasa kuna umbali gani na hapo buguruni?
na wewe kwanini unakaa Buguruni? huko hata mkuu wa mkoa hajawahi kufikiria kutembelea
 
Daraja la mfugale halikuwa na umuhimu kama ring road za Tabata dampo na buguruni.. Lakini hizo hazikujengwa tukaenda kujenga kivuko cha waenda kwa miguu buguruni utadhani wao ndio wanasababisha foleni
 
Abiria wa daladala Wana haki ya kulalamikia foleni kwasababu daladala zimepangiwa njia lkn mtu mwenye gari binafsi? Aidha huijui Dar es Salaam vizuri ama una hamu tu ya kukaa kwenye foleni.
 
Sio mkoa tu kumbuka kuna gari nyingi zinaingia na kutoka via hiyo njia kwenda mikoani
 
Watatenga bajeti mwaka wa fedha ujao kujenga hilo eneo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…