KERO Foleni ya magari Mwenge, Dar yaendelea kuwa kero kwa wananchi

KERO Foleni ya magari Mwenge, Dar yaendelea kuwa kero kwa wananchi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Barabara ya Mwenge, ambayo ni miongoni mwa makutano makuu na muhimu zaidi jijini Dar es Salaam, inaendelea kushuhudia msongamano mkubwa wa magari, hasa wakati wa asubuhi na jioni. Eneo hili linalounganisha Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Bagamoyo, na Sam Nujoma ni kiungo muhimu sana cha usafiri, lakini limegeuka kuwa mtego wa muda kwa wananchi wanaotoka maeneo ya Tegeta, Kawe, na Bunju kwenda katikati ya mji au Mlimani City na Ubungo.

Ongezeko kubwa la magari pamoja na changamoto za usimamizi wa vituo vya abiria vimefanya msongamano huo kuzidi kuwa sugu siku hadi siku, huku sababu kadhaa zikitajwa ikiwemo ni ucheleweshwaji wa kumalizika kwa matengenezo ya barabara na uzembe wa traffic barabarani.
1788849592368.png


1788849664002.png


1788849709927.png
 
Flyover hata moja imewashinda kujenga, wanasubiri warabu wawajengee
 
Flyover hata moja imewashinda kujenga, wanasubiri warabu wawajengee
Hilo eneo kwenye master plan yake kuna flyover, bahati mbaya sana aliyejenga flyover zote zilizopo na ambazo zilikuwa kwenye mpango hayupo tena..
 
Leo nilikwama hapo asubuhi, kichwa kiliwaka moto.
 
Tunaotokeaga ubungo kwenda mbezi beach hatuna la kusema. Kwanza pale mliman tunapigwa stop lisaa kungoja misafara ya kwenda na kutoka makongo juu
 
Back
Top Bottom