A
Anonymous
Guest
Napenda kuchukua fursa hii kuwaandikia barua hii kama Mwananchi mzaliwa na mkazi wa Mkoa wa Arusha, nikiwa na dhamira ya dhati ya kuchangia mawazo na maoni yatakayosaidia maendeleo ya mji wetu.
Kwa muda mrefu sasa, Mkoa wa Arusha umekumbwa na tatizo sugu la ongezeko kubwa la foleni ya magari, hali ambayo imegeuka kuwa kero kubwa kwa wakazi na wageni wa jiji letu.
Tatizo hili limeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi, matumizi ya muda wa wananchi pamoja na ustawi wa kijamii kwa ujumla.
Kwa sasa, mji mzima wa Arusha umeonekana kuchafuka kutokana na foleni zisizo na mpangilio pamoja na tabia ya baadhi ya madereva kushindwa kujiongoza na kuheshimu sheria za usalama barabarani.
Bajaji, magari madogo (Toyo), pamoja na watembea kwa miguu, kila mmoja anaonekana kutaka kuonyesha kuwa yeye ndiye mwenye haraka zaidi kuliko mwenzake. Hali hii imesababisha msongamano mkubwa wa magari, vurugu barabarani na kuongezeka kwa hatari ya matukio ya ajali.
Napenda kulielekeza pia suala hili mahsusi katika eneo la Friends Corner, ambapo kuwepo kwa Bajaji zinazosimama na kufanya shughuli zao katika eneo hilo kumechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa foleni. Kwa uhalisia, uwepo wa bajaji hao unaongeza msongamano wa magari kwa kiwango kikubwa sana.
Ni maoni yangu kuwa kuondolewa au kupangiwa eneo maalum kwa bajaji hao kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni katika eneo hilo.
Aidha, hali ya usimamizi wa usalama barabarani nayo imeendelea kuwa changamoto. Inaonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi wa Usalama Barabarani linakabiliwa na ugumu katika kusimamia na kuongoza magari ipasavyo.
Vilevile, kutokuzingatiwa kwa taa za kuongozea magari kumezidisha tatizo la msongamano na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.
Ni vema hatua zikachukuliwa kutafuta utatuzi, kuacha kama hivi kunamaanisha ni kama Viongozi wote wa Mkoa kuanzia chini hadi juu wameshindwa, tunakoelekea hali itazidi kuwa mbaya kama hakuna mpangilio wa maana utakaofanyika kutafuta solution.
Pia soma ~ RC Makala aagiza TARURA, TANROADS na Polisi kuondoa foleni Arusha, TARURA yatangaza kufuta 'stendi bubu'