Food For Thought: Kuna tofauti gani kati ya Mamlaka, Tume pamoja na Bodi?

Food For Thought: Kuna tofauti gani kati ya Mamlaka, Tume pamoja na Bodi?

MFUMO WA WIZARA UKO HIVI:
WIZARA>VITENGO > IDARA >TAASISI,MAMLAKA,BODI, WAKALA e.t.c
NB:
Cha ajabu hao wa chini ndio wenye maslahi mazuri kuliko wa juu.
Kwa hiyo NIDA wapo juu kuzidi Uhamiaji kulingana na huu mlolongo wako?
 
Mamlaka. Hii inaundwa na vizee vyenye roho mbaya hasa wafanyakazi wa serikali.
Tume. Hii inaundwa na wapigaji ambao huteuliwa kishkaji na mhuni mwenzao. Kwa mfano tume inaweza kuudwa kushuhhulikia upotevu wa shilingi milioni tatu lakini yenyewe ikatumia milioni mia tatu. Tume huundwa na watu wenye longo longo.
Bodi.
Hii inahusu utamu zaidi. Bodi huundwa na mijimama yenye minyama nyama. Bodi Mara nyingi huongelea umbea tu lakini umbea na wanalipwa.
 
MFUMO WA WIZARA UKO HIVI:
WIZARA>VITENGO > IDARA >TAASISI,MAMLAKA,BODI, WAKALA e.t.c
NB:
Cha ajabu hao wa chini ndio wenye maslahi mazuri kuliko wa juu.

... nadhani ni majina tu; yoyote ingeweza kuitwa vyovyote. La msingi ni sheria inayoipa nguvu taasisi husika; naming isn't important, I think. Kwa mfano TANROADS ni agency yenye mamlaka kisheria kuhusiana na masuala ya barabara; HESLB vivyo hivyo kwa masuala ya mikopo ya wananfunzi.

Hata Polisi jina rasmi ni Idara ya Polisi (Police Department) vivyo hivyo Idara ya Mkemia Mkuu; TBS (bureau), n.k. wana sheria na mamlaka zao kiutendaji.

Anyway, mtazamo wa mjinga.

Wakuu, nyie wote wawili ndio mnazidi kunichanganya hapa aisee. I'm in a state of total confussion.
 
Hao walikuwa wanatumiwa na Mabeberu sasa Mabeberu yamewaingiza king baada ya kukubali uzalendo wa Rais Magufuli.
 
Ujue una maswali fikirishi bwana mdogo ila dhumuni lako linashindwa ku meet requirement yangu ya ku dedicate time yangu kujibu hoja yako. ngoja tuone mpaka tamati itakuwaje na wadau wengine watajinasibu vipi,... huenda nikapata wasaa wa kujibu hili.


Huu ndio wasaa, jibu please.
 
MFUMO WA WIZARA UKO HIVI:
WIZARA>VITENGO > IDARA >TAASISI,MAMLAKA,
Mkuu, kwa mtitiriko huu wako Mamlaka kama ile ya mapato (TRA) ina-report kwa mkuu wa Taasisi ama mkuu wa Wizara?
 
Magufuli aliposema yeye ni kiongozi anayewajali sana wanyonge na watu wa chini ulidhani anatania?
 
Hizo zote TUME, TAASISI, MAMLAKA, WAKALA zipo chini ya wizara husika ambapo mtendaji mkuu ni katibu mkuu.
Sawa mkuu. Asante kwa ufafanuzi.

Sasa kwanini zina majina yanayo tofautiana (TUME, TAASISI, MAMLAKA, WAKALA) ilhali zote zipo chini ya mtu mmoja ambaye ni waziri?
 
Ambaye angemsumbua Rais Magufuli kwenye Uchaguzi labda yule mama wa ujerumani tu.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu Watanzania eti;

Kuna tofauti gani kati ya Mamlaka (Authority), Tume (Commission) na Bodi (Board)?

(1) Kwanini zamani ilikuwa Income Tax Department ila ikabadilishwa na kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na sio Tume au Bodi?

(2) Kwanini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haikuundwa ikaitwa Authority, Board au Department?

(3) Kwanini Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) sio Mamlaka (Authority), Tume (Commission) au Department (Idara)?

(4) Kwanini moja inaitwa Idara ya uhamiaji (Immigration Department), nyingine inaitwa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ya tatu inaitwa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya (DCEA) ilhali zote zipo chini ya wizara moja ya mambo ya ndani ya nchi? Kwanini zote zisiitwe Mamlaka au Idara kwa maana zipo chini ya wizara moja?

(5) Kwanini ile inaitwa ni idara ya usalama wa Taifa na hii inaitwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)? Kwanini zote zisiitwe idara au taasisi (idara ya kupamnana na rushwa au taasisi ya usalama wa taifa) kwa maana zipo chini ya wizara moja?

Kuna tofauti gani hapa wakuu?

NJE KIDOGO YA MADA: Kama una rafiki yako ambaye ni mwanasiasa wa CCM, CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa hapa Tanzania muulize swali hili;

"Kama Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 kisha ikawa Jamuhuri mwaka 1962, kuna tofauti gani kati ya nchi kupata uhuru na kuja Jamuhuri?"

Ila kuwa makini kwa maana urafiki wenu unaweza ukafa hapo hapo. Jioni njema...!!!!!

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Swali zuri sana, na likijibiwa litatusaidia wengi mno!
 
... nadhani ni majina tu; yoyote ingeweza kuitwa vyovyote. La msingi ni sheria inayoipa nguvu taasisi husika; naming isn't important, I think. Kwa mfano TANROADS ni agency yenye mamlaka kisheria kuhusiana na masuala ya barabara; HESLB vivyo hivyo kwa masuala ya mikopo ya wananfunzi.

Hata Polisi jina rasmi ni Idara ya Polisi (Police Department) vivyo hivyo Idara ya Mkemia Mkuu; TBS (bureau), n.k. wana sheria na mamlaka zao kiutendaji.

Anyway, mtazamo wa mjinga.

hapana mkuu
 
Back
Top Bottom