Proceed with extreme caution. Tukumbushane yaliyowakuta walio-invest DECI. Nao walikuja na gia hizi hizi, wakasema wamesajiriwa, na wakafanya publicity stunts nyingi tu ili kuwakamata watu wengi haraka haraka. Cha kujiuliza kuhusu hawa FIC Football Investment, je iwapo wanahusika na Investment, wamesajiriwa CMSA (Capital Markets And Securities Authority (CMSA)? Iwapo ni wahusika wa michezo ya kubashiri je wamesajiriwa GBT (Gaming Board of Tanzania)? Ila hata logically, are you ready to invest kwenye project ambayo iko based on kukisia. Si heri uende kununua hisa DSA (Dar es Salaam Stock Exchange) kama una appetite ya risky ventures? Hawa jamaa so far nimeona wamejitambulisha kuwa wamesajiriwa Brela tu, sasa hata hiyo is very basic, nadhani hata baadhi yetu hapa tayari tuna business ventures tumesajiri uko pia. Let's proceed with caution. Tukumbushane pia yaliyotutokea hivi karibuni from Bwana Maguruwe a.k.a bwana vanilla village.