Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Nimeangalia michezo ya AFCON ilyochezwa na nchi za Afrika ya mashariki za Kenya, Tanzania, Uganda na Burundi, halafu nikaongezea na DRC ambayo bado haijaingia EAC. Vile vile nimeangalia michezo yote ya 2019 Women FIFA World Cup iliyochezwa na nchi zote zilizoshiriki. Huenda maono yangu siyo sahihi ila ni wazi kuwa timu za wanawake za USA, France, Sweden, Spain na Netherlands zinacheza mpira mzuri na wa uhakika sana kuliko nchi hizo za Afrika ya Mashariki na Kati nilizotaja hapo juu. Tofauti inatoka wapi ? Timu hizo za wanawke zikiwekwa ligi moja na timu za Taifa za Afrika ya Mashariki na ya kati, utashangaa wakati wa Quarter Final kutakuwa na timu hizo za wanawake tu.