SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,889
Habari zenu.
Nimekuwa nikijiuliza sana juu ya mahusiano kati ya mke na mume ndani ya ndoa kuna vitu nimeshinmdwa kabisa kuvipatia majibu. Naombeni mnisaidie ndugu zangu.
Eti for how long tunatakiwa kusamehe na kusahau kwa kosa ambalo ni la kulirudia? Namaanisha kwamba kama wewe unachukia mpenzi wako kufanya kitu flani na ukamwambia jinsi unavyoumia akifanya kitu hicho, kwa hali ya kawaida mimi nilikuwa ninafikiri kuwa ukishamwambia kikukeracho atajitahidi juu chini katikati pembeni ili asikifanye tena..... kumbe lah kuna ambao wao huwa ni kawaida
Mf. mtu mwenye tabia ya kuchelewa kurudi majumbani bila kutoa taarifa au tabia yake ya kutoka kwenda saluni bila kukuaga wala kutoa taarifa!
unatakiwa kusamehe kila anapolifanya kosa hilo au ?
Na je anapolirudia huiwa anamaanisha nini?
wewe mwenzi wako akiwa anakufanyia hayo utajisikiaje na utaamua kitu gani?
Tafadhali nisaidieni.
Ni kweli inakera pale mwenza anaporudia kosa hilo hilo mara kwa mara. Inapotokea hali ya 'kosa' kujirudia rudia mara kwa mara, then kuna kila sababu ya kuwa makini zaidi na kujichunguza wewe binafsi kama sehemu ya ndoa na kisha mwenza wako (Ili usijikute unataka kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati kwako kuna boriti!).
Usipokuwa makini unaweza kuwa unaaddress dalili za tatizo badala ya kuaddress tatizo lenyewe.Hivyo ni vema kufanya uchunguzi (positively) wa kutosha kabla ya kufikia conclusion ya either kuvunja mahusiano, kutoa 'adhabu' au kulipiza kisasi.
Kwenye ndoa kuna mambo mengi ambayo yanachangia wanandoa kubehave namna hii au ile. Kwa mtu wa nje si rahisi kujua mambo yanayoendelea ndani bali tunaona tu dalili kwa nje. Njia nzuri ya kuweza kujua kiini hasa cha tatizo ni kuongea na wanandoa (au kama ni wanandoa wenyewe kukaa chini na kureview mahusiano yao).
Hivyo MJ1, kama unataka (na unauwezo wa) kusaidia ndoa ya dadako, ni vema kwanza ukawa na neutral position na kujaribu kuongea na wote wawili kwa nyakati tofauti. Hii itakuwezesha kujua grivances za kila mmoja against mwenzake. Trust me hiyo tabia ya shemeji yako kuchelewa kurudi, kuna uwezakano mkubwa ni reaction towards tabia za dadayako!