we Ruta, mbona unaandikla kama AK? au Rutashubanyuma =Akili Kichwani?
halafu sio kweli kuiwa mwanaume ni dhaifu anapokaribia ejaculation, na kwa wasichana na wanawake, nawaonya mapema, mkifuata ushauri wa Ruta basi mtaonekana mnatumia tendo lenu hilo kama silaha. utakuwa ni utapeli.
hata kama hiyo nadharia ingekuwa sawa, bado ina mapungufu manake inaeleza wakati mzuri wa mwananmke kuomba msamaha lakini haielezi wakati mzuri wa mwaume kuomba msamaha. hata kama umetahadharisha mada isomwe na ladies tu, bado hata hao ladies wanapenda kujua wakati mzuri wa kuombwa msamaha na wanaume.
msamaha wa kweli si ule utokanao na hadaa au "timing" fulani hivi. ni vyema kama mnakosana na wenzenu muwaombe msamaha mkiwa katika hali ya kawaida na msihusuishe kabisa tendo lile na ombi la msamaha. msamaha wa kweli ni ule utokao moyoni na sio utokanao na udhaifu wa mwanaume
mbarikiwe sana wapendwa
Glory to God!