For Teamo and Co: Baadhi ya imani potofu kuhusu uzazi na watoto

na pia kuna kamtindo nilishawahi kuona kondakta wa basi moja kabla ya kuondoka anarusha vimawe ndani ya basi nikauliza sababu ni nini nikaambiwa eti kuna wanawake wako kwenye siku zao wataleta mkosi barabarani.....kwa kweli huu ni uonevu
 
Hii ngoja tusubiri kuiongeza kwa sababu imekaa vibaya sana. Ila kweli, kuna imani kuwa mwanamke akiwa kwenye period chanzo cha mikosi. Nashani kuna makabila ambayo inabidi hata kutengana kitanda na mume wake. Ngoja tusubiri kwanza wadau watupe maoni yao.
 
preta umenikumbusha nyengine

mwanamke akiwa kwenye siku zake asitengeneze mkate wa mayai .....................hauta 'umuka'. yaani utakuwa bumunda! heheh
 
Hii naiongeza moja kwa moja. Unachungulia lakini orodha yetu inavyokua?

Nitamtafuta jamaa yangu (medical anthropologist) ili aangalie uwezekano wa kuyatafit baadhi ya mambo. Na especially maana yake kwa wigo mpana (broad perspective).
 
hii mikwaraq ilikuwa na malengo yake. nitatoa maelezo machache

preta umenikumbusha nyengine

mwanamke akiwa kwenye siku zake asitengeneze mkate wa mayai .....................hauta 'umuka'. yaani utakuwa bumunda! heheh

my dear wanawake tunanyanyaswa sana....sijawahi kusikia wanaume wao wana mikosi gani ni wanawake tu.....na hii yote ni wao ndio husema
 
Sasa jamani, utamjuaje?

Hii naona imekuja siku hizi (it is contemporary) kwa sababu huko nyuma hao mashetani hawakuwepo.

nakataa hii mkuu

mashoga wamekuja sambamba na lugha ya kiswahili. Kwa hiyo kwenye maeneo ya pwani mashoga wako tokea zamani japo hawakuwa wakijinadi namna hii tunayoiona sasa.
 
Hii naiongeza moja kwa moja. Unachungulia lakini orodha yetu inavyokua?

Nitamtafuta jamaa yangu (medical anthropologist) ili aangalie uwezekano wa kuyatafit baadhi ya mambo. Na especially maana yake kwa wigo mpana (broad perspective).

hiyo list naiyona inavyorefuka! Maisha yetu yamezungukwa na vitu tusivyojua maana 🙂
 
Godii,

Umenikuna sana kwa maelezo yako.

Hilo la kuepusha ndugu wa karibu kuona ni kweli kisayansi kwa sababu kuna kitu kinaitwa inbreeding. Yaani watu ndugu au wanyama kuzaa pamoja. Inasababisha kuendeleza magojwa ya kurithisha lakini pia inapunguza kitu kinaitwa "genetic variability" ambayo huaongeza fitness ya viumbe hai. Hata wanyama wa porini wana strategies za kuzuia inbreeding.
 
my dear wanawake tunanyanyaswa sana....sijawahi kusikia wanaume wao wana mikosi gani ni wanawake tu.....na hii yote ni wao ndio husema

Ni kweli kabisa. Ni jambo la kusikitika kwamba myths nyingi zimekaa kimtego mtego kwa ajili ya kuwakandamiza wanawake. Ila kitu kinachokera, wanawake wenyewe wanakuwa media ya kuzieneza. Nadhani tuendelee kujadili labda hawa vijana wetu akina Teamo and Co wengine wanaweza kuambulia moja au mawili ya kuwafaa. Mfano kama hilo la marufuku wakati wa terminal pregnancy!!!

nakataa hii mkuu

mashoga wamekuja sambamba na lugha ya kiswahili. Kwa hiyo kwenye maeneo ya pwani mashoga wako tokea zamani japo hawakuwa wakijinadi namna hii tunayoiona sasa.

Inawezekana. Wenzio tumekuja pwani juzi juzi tu.
 
mwana mwari haruhusiwi kujitia manukato akanukia au atakumbwa na jini
 
Which means what?

Kwamba jini linaweza kuwa "popobawa" au?

Nitaiongeza pia ukinipa ufafanuzi kidogo zaidi.
 
nafikiri ni kutaka tu mtoto wa kike ambae hajaolewa asijipambe sana wala kunukia sana kuepusha kuleta vishawishi huko mitaani.

Ndio wakamtisha kwa kumwambia ukifanya hivyo utapata jini ( na utakosa nafasi za kupata binaadamu mwenzio wa kuishi nae)
 
Haaaaaaaaa,

Hapo umenikumbusha. Nilishawahi kusikia yule mjinga Shekh Yahaya akisema kuwa majini yanaoa. Kwa hiyo nimekupata. Ngoja niiongeze kwenye list yetu.
 
Mkuu umesahau kale kadesturi ketu ka kuwafunga watoto kabangi mkononi ili kumlinda na wachawi,naona mijini siku hizi kametoweka.Hivi kale kabangi uondolewa mtoto akifikia umri gani.
 
baadhi ya hizi mila ziko across the whole africa, kama mnakumbuka vizuri kwenye kitabu cha things fall apart cha chinua achebe kile cha enzi zile sio hiki kilichoeditiwa, kuna stori za nwoye na wadogo zake kina ezinma wakikatazwa kupiga uluzi usiku kwani wataita wachawi na pia nyoka usiku alikuwa naitwa uzi /kamba kitu ambacho ni the same huku east africa, so naamini hizi mila zilikuwa zinacut across subsaharan africa yote
 
na pia kuna kamtindo nilishawahi kuona kondakta wa basi moja kabla ya kuondoka anarusha vimawe ndani ya basi nikauliza sababu ni nini nikaambiwa eti kuna wanawake wako kwenye siku zao wataleta mkosi barabarani.....kwa kweli huu ni uonevu

Hii pia mimi nimeiona nilimbamba taxi driver mmoja asubuhi akiokota vijiwe saba na kuvitupa ndani ya buti nilipomuuliza akasema ni kinga huwa wanapakia wanawake wakila aina na vijiwe vilivokuwepo kwenye buti kabla vilitupwa na muosha gari kwahiyo anaweka vingine kabla ya kuanza kazi.
 
Mkuu umesahau kale kadesturi ketu ka kuwafunga watoto kabangi mkononi ili kumlinda na wachawi,naona mijini siku hizi kametoweka.Hivi kale kabangi uondolewa mtoto akifikia umri gani.

na wachawi ndo wanaogopa bangi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…