For your EYES ONLY: From Salva to Rostam

For your EYES ONLY: From Salva to Rostam

Hii habari inatakiwa mfikie mama Hawa Ghasia kwanza. Halafu atueleze haya ndiyo anataka iwe siri?
 
Huu sasa ushamba na uropokaji.

Ushamba na urookaji kwa nini? Kwamba watu wanawasema hawa waandishi mahiri wetu kwa kuwa hawawezi kuandika Kiingereza vizuri?

Mimi mpaka napata mashaka kama hii barua ni authentic, lakini kwa standards zetu za uandishi siwezi kushangaa pia kama kweli huyo Salva anaandika kiingereza kilichopinda hivyo.
 
As a result, some board members are willing to go public on these matters, something that would not be in the best interest of HCL, New HCL or anybody associated with the companies.
vitisho
That, refusal to regularize the situation at HCL is an attempt to avoid payment of Tshs. 100 million, as consideration to the old HCL board members, as per contract between HCL and Isenegeja, in the formation of New HCL.
ukicheza na fisadi lazima akufisadi...
And even if this communication does not enlist any kind of action, I can assure you that I definitely will still survive, in fact comfortably.
anatamba ana hela
That everybody of you is comfortable and some few of us are struggling to make ends meet, speaks volumes about our friendships and how we help each other as friends.
kumbe hana hela na analia njaa
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]do not deserve some part of the cake[/FONT][/FONT]?
kumbe TZ ni keki?? na kawaida ya keki usipoalikwa huwezi kuila...
Even if you found the idea of helping us become independent unattractive and costly, you could at least have looked for a way to accommodate us in some positions within the new Government whose struggle to get into power we so painfully supported and for so long.
ukijitegemea utawanyenyekea vipi si utaacha kuwa mtumwa wao
ndio maana wakina makamba kila siku wanarudi kulia njaa kwao halafu wanapewa kiduchu wanaambiwa nenda
salva alimtolea uvivu inaonekana jamaa ni muwoga wa kugombana na watu wanaomjua
 
Last edited:
vitisho
ukicheza na fisadi lazima akufisadi...
anatamba
analia njaa
ukijitegemea utawanyenyekea vipi si utaacha kuwa mtumwa wao
ndio maana wakina makamba kila siku wanarudi kulia njaa kwao halafu wanapewa kiduchu wanaambiwa nenda
salva alimtolea uvivu inaonekana jamaa ni muwoga wa kugombana na watu wanaomjua

Jambo linalonitatiza ni kwa nini RA asingegombea tukampa yeye Urais? Na je, kama JK akiamua kukata kamba sasa hivi na kuwa mtu huru hawezi? Kichwa kinaniuma na natamani kuikimbia nchi hii.
Hivi kweli tumefikia mahali ambapo tunajifanya mbwa koko na kukunjia mikia matakoni mbele ya wageni tena waliotuibia! Hapa bila kuchapana bakola huu unyonge hauishi. Wapo wengine ambao itabidi wavutwe na katapila kutoka mlangoni kwa RA walikokimbia na makopo yao ya Matonya!
 
mbona sijawahi kuona humu mkijadili kuhusu kiswahili kibovu??? acheni kujitia walinzi au viranja wa lugha za wenzenu wakati lugha yenu mnayo.

Kiswahili kibovu kinararuriwa kila siku.Hata kama kingekuwa hakiraruriwi, two wrongs do not make a right.Kosa ni kosa, hata kama likiwa limeachiwa kwingine.Huwezi kuua mtu halafu ukaleta defence ya kusema mbona fulani naye aliua na hajafanywa kitu.That is a really weak argument.

Tetezi kama hizi zinazoletwa na anti-intellectualism apologists wanaowalea hao incompetents, at the same time wakiipeleka nchi vibaya mnapiga kelele.

Kuhoji kiingereza hapa kuna kazi kubwa mbili.

1.Kunaweza kui-expose hii barua kama a fake, kama kweli Salva ni muandishi mzuri, anayejua kiingereza vizuri, na watu wanaweza kujua standard yake ya kiingereza kutoka kwenye articles zake, then tunaweza kulinganisha kiingereza cha Salva katika articles zake na hiki kiingereza hapa tukapata a reasonable picture kwamba hii barua inaweza kuwa imeandikwa na Salva au la.

2.Kuhoji kiingereza kunaonyesha jinsi nchi yetu ilivyo na tatizo la lugha, kwamba mpaka waandiashi wa habari mahiri (au wenzao wanaotaka kuwa impersonate) hawajui kiingereza inaonyesha tatizo ni kubwa kiasi gani.

Kuna sababu chache za kutetea incompetency hii.

1.Mtetezi hajui makosa yaliyofanyika na kwa hiyo hana jinsi ya kuelewa umuhimu wa makosa haya, na pengine baya kuliko yote hana udadisi wa kutaka kujua, anaona wanaofuatilia lugha ni vifimbocheza wasio na mada.Zaidi ya yote anaweza kuwa hapendi ukosoaji lugha kwa sababu ana udhaifu katika lugha, na mtu yeyote anayekosoa lugha anakuwa kama anamnyooshea kidole yeye na kumkosoa yeye pia. "Kama siwezi kuona makosa haya ina maana mimi na muandishi huyu tuko sawa na anachokosolewa na mimi naweza kuwa nacho".Tukubali kukosolewa, ndiyo kujifunza.

2.Mtetezi ana uzalendo wa kijinga na reverse inferiority compex, anaona kukosoa kiingereza ni kutaka kujifanya muingereza au kutukuza uingereza, kwa hiyo hataki kuzungumza kuhusu kuboresha kiingereza.

3.Hoja potofu kwamba lugha si muhimu, almuradi mtu anaeleweka.Hoja hii ni potofu kwa sababu ili kueleweka kwa uhakika tunahitaji kutumia lugha sahihi.

Kwa ujumla, kusema "acheni kujitia walinzi au viranja wa lugha za wenzenu wakati lugha yenu mnayo" kunaonyesha huyu muandishi asivyoelewa sehemu ya lugha katika mawasiliano. Hatukuchagua Salva aandike Kiingereza, Salva amechagua hivyo, hatukutafsiri maandishi ya Salva yaliyoandikwa kiswahili kwenda kiingereza na kukirarua kiingereza hicho, Salva mwenyewe kaandika kiingereza kilichopinda ambacho kiko chini ya standards zinazotakiwa
 
splendid!
 
RA anawaweka watu wengi sana hapo mjini...huyu ni kama Osama, kichwa chao. Pengine bila kichwa....

kweli mpaka rais wako!!!!!

Kila siku nasema tatizo sio RA ni JK, watu wanabisha, unafikiri Nyerere angefanya hivi???
 
Ni katika kutaka kujua tu .Je hii nyaraka za Srikali ama siri zao ambazo wamezipigia kelele kule jumbani kwenye baridi ?
 
What a shame!!! Yaani huu ni umbea au ni kujikomba na kujidhalilisha njaa!!!! Toba Rabi, kumbe Salva hana maana, nafasi yenyewe kaipata kwa kupachikwaaaaaaa. Hawa Ghasia uko wapi?? Ila nahofu hata kwa Hawa Ghasia kuwa utumishi ni dili maana ni shemejiye JK na hawezi mwangusha katika dili za kupatia washikaji zake kazi serikalini, bila kusahau vimada.

Kulaleki, nilishasema nchi inaongozwa na RA na EL!!!! EL yuko Benji lakini bado ana power kubwa sana kwa JK!!!!!

Wakuu wa BRELA vipi, tujuzeni kama hiyo New Habari imeshasajiliwa na kwa majina gani?? Kama bado haijasaljiliwa theni tuanze kuwasha moto katika jukwaa letu na waandishi wa habari waipate?? Hiv This Day, Kulikoni, Taifa letu, Nipashe, hawajaipata hii??

Yaani nchi yetu inafananishwa na cake?? RA wa Irani ameshakula half of the cake!!!! Salva naye anataka!!!! Yesu wangu wee!!! Watoto wangu na wajukuu wataambulia nini katika keki hiyo??

Watanzania tuamke sasa, ikibidi tuanzishe vita vya kuwang'oa mafisadi wote. Hivi hatuwezi?? Tuanzie tu kwa kuanza kuchoma maviwanda yao, na mabiashara yao tuwaingizie hasara kwanza mmoja baada ya mwingine. Please, give me a hand grinade (check spelling). Tunahitaji wazalendo wanaojitoa mhanga!! Upinzani umeshashindwa so we need others, tujaribu hiyo tunaweza kufaulu.

Kule Uganda Idd Amin aliwafukuza wale jamaa, hadi leo wanaikoma Uganda. Na sisi tuamke, tuwatafue vijana wanaofanya kazi katika mashirika na makampuni hayo tuwape fedha nooooooono, wafanye vitu vyao.

Nimesikia hasira.
 
Dilungaaa
........Unakumbuka Kagoda?

Ogah, nakumbuka Kagoda, ndio, lakini hii inadhihirisha mengi ya Rostam kuliko Kagoda. Kwenye Kagoda hakutumia nguvu, alichora mchoro, akatunga majina John Kyomuhendo and Francis William, akashirikiana na kina Jeetu Patel wakatafuta insiders wa kuzima light switch na security alarm, zigo likatoka benki kuu. Hii hapa ni kwamba Rostam anapiga simu Ikulu kumuombea mtu kazi ya u-spokesperson wa Ikulu. It's beyond the pale.

Kikwete atakuwa amejifunza mawili matatu. Miaka miwili ya mwanzo alikuwa analipa fadhila, anasema "liwa ule," nikune mgongo nikukune wa kwako. Kunana-kunana hizi sometimes mikono inaenda beyond migongo n.k., ndio yanatokea ma skandali ya billioni 133, na hizi aibu za kuombeana kazi Ikulu kama ki-gang cha Sicily.

I wish angekuwepo prosecutor mwenye ujasiri wa ku subpoena rekodi za haya ma conversation ya Rais na fisadi tusikilize Rostam anavyotongoza watu kwenye simu za Ikulu.
 
HATARI KUBWA!tunekoelekea sio kuzuri kabisa
 
Dilunga,

Ni vibaya kwamba Kikwete anakwenda kwa falsafa hii. Kibaya zaidi ni kwamba, maneno hayo uliyosema, si kwamba umemsemea maneno ambayo hajayasema kulingana na falsafa yake inavyoonekana, ni maneno ambayo Kikwete mwenyewe ameyasema wazi mbele ya kadamnasi!

Yaani hata kama "kula na kipofu" this is too much, sio tu wanamgusa mkono kipofu, wanamtukana na kumfunga mikono asile kitu, atafanya nini nan yeye kipofu?
 
Mie sishangai kabisa. Huyu Salva ni opportunist na juzi juzi baada ya kufanikiwa kupewa kazi na Rostam hapo Ikulu alikuwa anahaha kumsaidia rafiki yake Gideon Shoo ili awe mkurugenzi wa habari MAELEZO. Lakini bahati nzuri safari hii watu wa usalama wa taifa walifanya kazi yao vizuri wakampiga chini. Kazi ya MAELEZO sasa kapewa Clement Mshana wa TBC.
 
Ahsante sana ushauri huu "You really need to read the document maana its more than "kuvuja siri za serikali " "- , ndo maana nikasema hili bandiko linasema mengi zaidi ya jinsi tunavyochangia humu.

Nimetumia maneno ya siri za serikali lakini katika mabano kuonyesha kuwa kila mtu aliye karibu na system, siri zake zinachukuliwa kama siri za serikali, kumbuka sakata la Masha na vitambulisho vya Taifa, sakata la Kubenea kutoa namba za accounts za watu waliojihusisha na EPA n.k, kumbuka sakata la Zitto na mikataba ya madini, kumbuka TICTS, sakata la Mkapa na machimbo ya Kiwira n.k na n.k naweza taja mengi, haya yote yanapoguswa vitisho hujitokeza na hata kutishwa kuwa nchi haitatawalika kama watu hao kugusa. Au kutolewa maneno ya kejeli eti kuna wanatafuta cheap populality.

Nakubaliana na wewe kuwa "inaonyesha kuwa kuna watu very poweful nje ya serikali lakini wenye nguvu kama au kuliko serikali.Hawa wanatisha maana ndiyo vinara wa ku steer mambo mengi yanayoiyumbisha serikali na kuwafanya wananchi kuishia na hali duni." Unategemea nini kama rais alipolihutubia bunge alisema "kubali kuliwa ili na wewe ule" hii ina maana kuwa kuna watu wameruhusiwa kutula bila hata ya ridhaa yetu. Hawa wanaotula wanalindwa kwa kila hali na serikali, ukiwagusa aidha nchi haitatawalika au unaambiwa siri za serikali zinavujishwa na atakayekutwa nazo kiama chaja. Haya ndo niliyomanisha, ndo mana nikasema tutatokaje katika usingizi huu? Tunaliwa hatushituki, tukishituka tunajipiga kofi mithili ya mtu aliyeumwa na mbu kisha tunaendelea kulala na hata kutega sehemu nyingine ili tuendelee kuliwa zaidi.

Asubuhi itafika lini ili tuamke kuhesabu makovu tuliyopata? Nani atuamshe kutoka usingizi huu tutambue kuwa mbu hafukuzwi kwa kujipiga kofi bali ni kwa neti au dawa e.g Rungu?

Tafakari.
 
Duuh....jamani nasisitiza kwenye maombi kwa taifa hili. Hizi taarifa kwa kweli zinatisha na kwa mtaji huu ufisadi hautaisha milele. Yaani nchi sasa imekosa uzalendo kabisa ni kula kula tu. Sio siri inauma sana watu tuliowapa madaraka wanaendelea kutulaghai kiasi hiki.

Salva pamoja na kuaminika katika taalum ya habari ndo huyo anashabikia vifo vya uhuru wa mawazo, wako wapi wakongwe ambao tuliwategemea kuwa ndio wakombozi na wenye kupaza sauti za wanyonge, Je tuendelee kuviamini na kuvipa hatma ya nchi vyombo vya habari hapa kwetu??? Jakaya mwana wa Kikwete amka na urejeshe heshima yako na kulinda maslahi ya walalahoi, ni wewe pekee kwa sasa mwenye mamlaka ya kukomesha DHARUA HII.

"Ulisema kwa kauli yako mwenyewe kuwa Urais wako hauna ubia na mtu isipokuwa Makamu wako", Je ni kweli umekuwa mwoga kiasi cha kushindwa kuwaamini wapiga kura wako? Je inawezekana kweli umetia pamba masikio yako na vilio hivi huvisikii? Kama unamikakati mbona muda unaelekea kukutupa mkono. Amka ee bwana na usikilize sauti ya MUNGU kwani manabii walisema sauti ya wengi ni SAUTI YAKE BWANA.

INSHALAH kwa dua na kilio hiki na hasa kama yanayoletwa humu ndani ni ya kweli basi na adhabu yao ianzie hapa hapa kama ilivyowatokea akina A....M...na wngine wanaokosa usingizi kila kukicha.

Amen!
 
Mie sishangai kabisa. Huyu Salva ni opportunist na juzi juzi baada ya kufanikiwa kupewa kazi na Rostam hapo Ikulu alikuwa anahaha kumsaidia rafiki yake Gideon Shoo ili awe mkurugenzi wa habari MAELEZO. Lakini bahati nzuri safari hii watu wa usalama wa taifa walifanya kazi yao vizuri wakampiga chini. Kazi ya MAELEZO sasa kapewa Clement Mshana wa TBC.

Huyo Gideon Shoo alifanya nini cha kuwahusisha Usalama wa Taifa?

Maana tusije kuwa tunasifu-sifu Usalama wa Taifa wakati hawahusiki katika vetting ya mtu kabla ya kuteuliwa.
 
Kama hii barua ni kweli ya Rweyemamu na ilimfikia Rostam ina maana Rostam ana uwezo wa kumuunganishia kazi mtu akawe presidential spokesman, nimekoma na Rostam Aziz.

By the way, to be the devil's lawyer for a minute, kama ungekuwa ni wewe Kikwete halafu kina Rostam na kina Rweyemamu ndio hao waliku propell into power kama Salva anavyosema humo, ungefanya nini wakija wanaomba na kuombeana kazi, ungejifanya huwajui? Sijui kama Kikwete atapokea tena favor ya mtu uchaguzi wa 2010. Labda 2011 Rais Kikwete hatakuwa mfukoni mwa kina Rostam na CCM financiers wengine.

Naona pia Salva kamtukana Johnson Mwambo kwamba ni "ki-mbwa cha J.U." akimaanisha Jenerali Ulimwengu, maana Ulimwengu ndie kibosile pale Raia Mwema. Salva Rweyemamu mwana haramu, kama ni barua yake hii.

Rostam aliwahi kulalamika kuwa kuna watu (presumably wana-mtandao wenzao) wanamlaumu yeye kwa kuwa hawakuteuliwa kwenye madaraka Serikali hii ilipoingia madarakani. Wanamtandao na all informed people wanafahamu nguvu ya RA kwenye Serikali hii. Je na ile info kuwa Edo Low.... aliweka watu wake kwenye the latest appointments za wakuu wa Wilaya? Wakuu tuambieni nani haswa ni kiongozi wetu: RA, EL au ....? au wote watatu wanaongoza kwa ubia na wakiamua wanafanya usanii hadharani kuwa wanatofautiana mambo fulanifulani ili kulaghai watu?
 
Nikiwa kana mmoja kati ya journalists waliowahi kufanya kazi pale HCL hadi miaka ya karibuni, kwanza niseme kwamba hiyo barua ni authentic – author ni Salva 100%. Ule msemo wa Kiswahili alioutoa ndiyo hupendelea sana. Aidha pronunciation ya maneno ni yake, kwani hubadilisha kati ya herufi l na r. Kwa hiyo methali yake nyingine ya Kiiengereza -- “many cooks spoil the blot” ni matamshi yake kabisa.

Lakini madhumuni hasa ya post hii ni kuomba mniruhusu niseme kwamba sijawahi kuona mtu muongo, mnafiki, haramia na mlambaji miguu ya wakubwa kama Salva.

Yeye na mwenzake -- aliyekuwa anampigia debe apewe kazi na JK -- Gideon Shoo, ndiyo waliifilisi HCL, na hadi wakafikia kumfitini Mwenyekiti wao na main sharehiolder, Jenerali Ulimwengu kupoteza uraia wake kwa muda.

Lengo ilikuwa JU aondoke nchini kwa kutokuwa raia, wao warithi kampuni, wamkabidhi RA kwa lengo la kuitumia kumuingiza JK madarakani mwaka 2005. Kumuondoa JU ilishindikana lakini kuifilisi kampuni walifanikiwa na kumlazimisha JU kuiuza kampuni shingo upande – kwa yule aliyekuwa tayari kuinunua kwa haraka – RA – ambaye wakati huo alikuwa tayari anazo pesa za Kagoda alizoiba.

Inashangaza Salva kusema eti HCL aliyoinunua RA ilikuwa inaendeshwa kinyume cha sheria za kuendesha makampuni huku kabla haijauzwa yeye mwenyewe alikuwa anaiendesha kinyume cha sheria: Alikuwa shareholder, CEO, na chief financial controller all rolled in one.

Hakuna malipo yaliyokuwa yakifanyika, hata ya sh 10,000/- bila yeye kuruhusu. Hakuna. Hii siyo kinyume cha sheria za makampuni, kwani interest za wafanyakazi zilikuwa zinakaa vipi? Yeye na Shoo walikuwa wanajichotea mapesa wanayotaka – walikuwa kila mara wakibuni vi-miradi vya kifisadi vya mamilioni.

Katika extension project ya newsroom, kabla ya kuweka foundation walinunua tani 1,000 za cement na kuiweka store mle mle na ilibidi circulation department wahame ili waweke cement. Hivi siku hizi kuna ulazima wa kuvundika cement? Si iko belele, unaletewa kwenye site siku ya kumwaga zege.

Na wakati cement ilikuwa inateremshwa Dr Shoo ndiyo alikuwa tally clerk – hivyo mntaelewa ufisadi ulikaa vipi katika deal hiyo. Na huo ni mfano mmoja tu katika mingi.

Wafanyakazi walikuwa hawalipwi mishahara hadi miezi mitatu lakini Salva kila mwezi anasafiri kwenda London.

Analalmikia akina Bobby aliyeletwa kama CEO kuwa hawaelewani na wenzie, nadhani sababu ilikuwa katika mambo ya dili. Bobby, na Chidaya (HR Officer) walitimuliwa na CEO mpya, Rosemary Mwakitwange kwa sababu ya wizi. Rosemary aligundua hundi 15 blank zilizokuwa tayari zimesainiwa na Bobby, Chidaya, Salva, Shoo (walikuwa sigantiories hao) -- yaani saini mbili za kati ya hao katika hundi mbali mbali kati ya hizo. Haikujulikana ni fedha ngapi walizowahi kuzitoa.

Hivi sasa Bobby na Chidaya wamerudishwa kwa mshangaio wa wafanyakazi wengi wa New habari.
Si hao tu, Rosemary, akishirikiana na Tagalile (managing editor) aliwatimua Manyerere, Balile, na Muhingo kwa kukosa maadili ya uandishi na kusababisha magazeti ya Kiswahili – hasa Rai na Mtanzania ku-nosedive katika mauzo. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwasiliana direct na RA (wakiwa-bypass Tagalile na Rosemary) na hivyo kuandika story na makala za kutetea mafisadi.

Kufukuzwa kwa hao RA hakulipenda na akakampeni sana kurudishwa kwao – kwa mlango wa nyuma. Walirudi na ndipo Rosemary aliacha kazi kutunza heshima na principles zake. Rosemary aliibadilisha kampuni na kutokea kuwa kipenzi kukibwa cha wafanyakazi kwani alijali sana masilahi yao, kama vile kuhakikisha mishahara kutoka tarehe 26 kila mwezi.

Nadhani hawakukosea waliomuita King Maker, anaweza hata kutengeneza na viking vidogovidogo.
Kudos ka-inzi

Never let a politician (fisadi) grant you a favour/They will always want to Control you forever..

Robert Nesta Marley
 
Back
Top Bottom