Vitabu vimeshawekwa humu vitafute uvipakue dukani ukatafute nini tena?Mkuu hivyo vitabu vya Forex for dummies and Naked Forex naweza vipata duka gani kwa wewe mzoefu?
acha uvivu soma hii thread yote ina vtu vng sana vya muhimMkuu hivyo vitabu vya Forex for dummies and Naked Forex naweza vipata duka gani kwa wewe mzoefu?
Around june 15thkila siku nimekuwa nikipitia huu uzi nikitegemea kutangazwa kwa siku ya kuanza kwa mafunzo
Mkuu mwanambugulu naomba unipatie link ya kitabu cha Naked TradingNaendelea kupata maarifa hapa namalizia kitabu cha 2 (naked trading )ila nimepitia pia kijarida kinaitwa 7 winning strategies by Grace Cheng
Aisee hii kitu inahitaji uamakini wa hali ya juu pamoja na kusoma ila pia hakuna jinsi lazima Uwe na mentor wa kukuongoza
Tuendelee kujifunza na punde darasa likianza basi iwe rahisi kwa mkuu kuendelea na vitu vigumu sio ndio kwanza unaanza kuuliza"what is forex " kwa kweli haita pendeza ila cha ziada tusome vitabu
Thanks all
Mkuu mwanambugulu naomba unipatie link ya kitabu cha Naked Trading
God bless you brotherUpdate ya kwanza
Kwanza kabisa niseme mimi na team yangu tumekuwa tukipambana sana kuhakikisha operation inaanza ASAP, lakini kiukweli mambo ni mengi sana, tofauti na nilivyotegemea.
Mpaka sasa naeza sema tupo almost half way katika kupata documents za kiserikali, vikwazo ni vingi sana sana, kila mtu anakwambia hiki, lkn tangu J5 tumekutana na watu wa ndani zaidi wa CMSA, hivyo nategemea week ijayo itakuwa smooth-tunaweza kukamilisha japo 90% ama kila kitu.
Kuhusu office yani hapa kichwa cha motooo si mchezo. Bajeti ya awali na hali halisi ni tofauti kabisa, kila unachogusa bei utakayotajiwa unatamani uwatukane wauzaji. But mwisho wa siku kwasababu maji tumeshayavulia nguo lazima tuyaoge.Reception kwajili ya maulizo nk
1 ya office za mentors
Pia niseme nimesikitishwa sana na baadhi ya watu either kwa kutokua na uelewa wa forex ama kwa maksudi kuanzisha thread za kunichafua mimi pa1 na hii programme. Kwanini mtu asije kuniattack hapa, ananiattack kwenye uzi ambayo siwezi kuuona ama naweza kuuona baada ya siku kadhaa. Kama mtu ana strong argument aje kwa huu uzi, sio kusambaza chuki kwenye nyuzi ambazo siwezi kutoa clarification. Nimeona wanavyonizungumzia in negativities, sijataka kuwajibu hata neno - kwasababu binafsi naamini muda ndio hakimu makini zaidi. Nataka results za wanafunzi wangu ndio ziongee si maneno yangu, tayari nimeongea sana.
Zaidi ya yote, niwaombe tuwe wavumilivu... vitu vizuri havihitaji haraka. Nahisi Mungu akijalia tunaweza kuanza kabla ya tarehe 15 June - mambo si marahisi kama nilivyotegemea, but nusu mwezi utatosha. Na ninapromise, this is gonna be a financial breakthrough kwa wale waliodhamiria, naongea kwa kile ninachokifahamu, kamwe katika maisha yako hautajilaumu kuifahamu forex.
Pia, baada ya kufanya tathmini kwa kina pamoja na team yangu nimegundua kua watu 300 ni wengi mno. Darasa litakuwa na watu 50 tu, ili interaction kati ya mwanafunzi na mwalimu iwe ya juu zaidi, pamoja na kuongeza concentration. Kutakuwa na maximum 3 sessions kwa siku. Hivyo nitaanza na watu 150 maximum. Kwa wale ambao hamtabahatika kua katika hawa 150 msiwe na presha, mtapata hii fursa mbeleni bila upendeleo, though charges may apply.
Kwasasa mtu anaweza asione umuhimu wa kulipia hii training, lkn nikitoa batch ya kwanza ya wanafunzi wangu, najua kila mtu atapanda dau kwajili ya kupata mafunzo. Moja ya aspect ya msingi kabisa ktk training tutafanya "Live trading" kwa pamoja. Yani tutatrade live kila mtu aone na aelewe nini ni nini, kwa wale ambao watakua na account wataweza kupiga mpunga jicho kwa jicho na mentors wetu. Yani mf kama una $300, pale pale live tutafungua trades tugonge $100 ya chap chap.
Wakati tunasubiri update ya mwisho, naomba tuendelee kusoma kitabu cha Forex for dummies. Baada ya kumaliza hicho kitabu tuanze kitabu kingine kiitwacho Naked Forex - High-Probability Techniques for Trading Without Indicators >>Kimeandikwa na Alex Nekritin. Please soma kuelewa, si kusoma kumaliza pages ama kumfurahisha Ontario. Your knowledge is the best weapon to beat the market.
Ontario.
Mkuu ONTARIO tunashukuru sana kwa darasa. Ila muhimu ukawaambia watu kwamba Forex Trading si biashara ya kila mtu, na kuna faida na hasara. Magwiji wa Forex hujitahidi ku mimimize loss ili kupata faida, ila ukiingia kichwakichwa itakufilisi.
Mbona alisha toa tahadhari hata Na mfano halisi wake mwenyewe jinsi alivyo pata hasara? Au umeanzia kusoma kivivu hivyo unakwepa Za mwanzoni? Fanya walau sampling kabla hujaanza kushiriki kutuandikia.
Na kwa ufupi tu! Hakuna uwekezaji wowote ule unaolipa ambao hauna risk kubwa! Karibu sana.
Mkuu PHES nimemsoma toka mwanzo. Chagua maneno ya staha, maana hiyo comment haikukulenga wewe. Naamini Hutopungukiwa na kitu. Nami nikitumia maneno yasiyo hapa nitakuharibia siku.
Naamini kuna watu wameanza Fx miaka mingi sana. Mimi nimeanza miaka saba sasa. Najua wengi huwa na mihemko wakidhani FXtrading ni utajiri wa haraka. Kichwa cha thread kitafanya watu wasiwe na maamuzi sahihi. Hata ONTARIO pamoja na uzoefu wake, lazima anapata loss; lakini ana minimize loss kwa ku maximize gain/win kisha kuwa na net profit. Lakini onyo honest, Forex si utajiri wa haraka. Na pia si kila raia anapaswa kujiunga na Forex trading.
Umeniwahi kumjibuMbona alisha toa tahadhari hata Na mfano halisi wake mwenyewe jinsi alivyo pata hasara? Au umeanzia kusoma kivivu hivyo unakwepa Za mwanzoni? Fanya walau sampling kabla hujaanza kushiriki kutuandikia.
Na kwa ufupi tu! Hakuna uwekezaji wowote ule unaolipa ambao hauna risk kubwa! Karibu sana.
Mkuu PHES nimemsoma toka mwanzo. Chagua maneno ya staha, maana hiyo comment haikukulenga wewe.
Asante kwa angalizo, nazidi kustaajabu Kama kweli umemsoma vyema toka mwanzo basi ningetarajia kuwa ungeweka mkazo kuonesha risk ilivyo. Lkn sio kumwambia aeleze alicho kwisha kueleza. Pia sijui neno gani uliloona kuwa nimelitumia lisilo la staha ndugu! Usije ukatumia lugha chafu kunijibu halafu tukaja laumiana baadae. Kwani sitarajii kutumia maneno machafu Na sijafanya hivyo. Kama unaleta tafsiri zako binafsi hiyo Ni juu yako.
Tatu, hapa ukichangia hoja haimaanishi Ni kwa ajili ya mtoa Mada tu! Vinginevyo angekuwa anawajibu au kuwaita pm. Hivyo openness ya hapa Ni yetu sote.
Natumaini umenielewa vyema, Asante.
Mkuu naona balance sio ya mchezo.Vip ulianza na kiasi gani?Maendeleo yangu ndani ya wiki moja ya kubahatisha bila kujua sana nachokifanya,thanx Ontario,i owe this 2 u.
€50,000,na less than a week nilikua na €1,000,so hapo nadhani mtaji ulinibeba,ningekua najua nachofanya ningepiga hela ya maana.Mkuu naona balance sio ya mchezo.Vip ulianza na kiasi gani?