Mimi kila nikimaliza kitabu kimoja najiona bado sijaelewa ndo nazidi kutamani kukamata kitabu kingne kiufupi hii mambo haihitaji kuipaparukia hongera sana kwa wale ambao wameanza na demo ila ninaimani bado wanahitaji kusoma zaidi kuliko kufurahi kwa kuona balance ya profit walizotengeneza kwenye demo.
Mimi binafsi nimejipa miezi sita nisome vizuri ili nijue a,b,c ya hii mambo, kitabu kwa kitabu na kupitia youtube kidogo naimani nitakuwa vyema zaidi all in all nitaendelea kumpigia salute mkuu, the boss
ONTARIO kwa kunifanya ning'amue haya mambo japo bado nahitaji support yake kubwa zaidi ili nitimize ndoto zangu za kuwa professional investor.
Natamani sana nifikie hatua aliyopo sandile shezi akina MLU n.k lakini inahitaji umakini wa hali ya juu nafahamu kabisa hii kitu haihitaji kukurupuka unaweza ukalala tajiri ukaamuka fukara wa kutupwa....
By the way tunahitaji muda mwingi sana wa kujisomea na kupractice ili tukiingia sokoni tuwe na uelewa wa kutosha zaidi.
Much respect kwa wale wanaoleta mirejesho ili tushee idea akina
Bavaria punje haradari Mpiga Nyoka jinimtu na wengine wengi sitoweza kuwataja lengo kila mmoja wetu apate mwanga acha mimi niingie chimbo nitakuwa nachungulia tu kuona mirejesho inayoletwa nalinganisha nami wapi nimefikia tuombeane uzima tu..