Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
unatumia broker yupi mkuu?
 
Weekend bhana, leo nimefurahi sana

Unajua bana mimi chuo nilisoma BSc. Petroleum Chemistry hapo UDSM, basically hii ni sayansi inayohusika na refinery ya gas na mafuta. Yani crude gas and oil tunazibadili kua final usable products kama LPG, CNG, Ammonia, ammonium fertiliser, mambo ya diesel, jet fuel, gasoline nk nk. Hapo chuo tulikua wachache watu kama 21 hivi, so Prof ni rahisi kujua darasa zima.

Sasa tulikua na Prof mmoja, alikua kama mama'etu. Yani kwenye pindi lake alikua anatuPump vby mno na kututamanisha kuhusu hii field yetu, kua kuna pesa vby mno, site kuna marupurupu, incentives, mishahara ya kibabe... Basi kila akiwa anakuja pindi watu wanatamani kumsikiliza yule mama, anafundisha kidogo anaruka kwenye mambo ya site, michongo na madili ya gas na mafuta... yani hapo sisi tunakua tunahamasika vby mno, yani tukampendaga bure yule mama. Akawa kama rafiki yetu, akawa academic advisor wa karibia sisi wote... yani she was more than a friend.

Leo bana kuanzia saa 5 asubuhi nilikua Golden Tulip na mtu wangu wa faida. Tumekaa pale, tumezungumza sana, tukala lunch na kila kitu. Mchana mida ya saa 8.30 akaja huyu Prof wangu wa chuo, nikamuona ila yeye hakuniona. Akawasha PC yake akaagiza kinywaji, akaendelea na shughuli zake, baadae kidogo akaja mwenzie ambae ni km mzungu wakaagiza misosi wakawa wanakula.

Mimi nikamshtua muhudumu, nikamwambia yule mama pale nipo nae, so anipe bill yake. Bill ikaletwa nikailipia... Baadae Prof anataka kulipa ndio anaambiwa tyr bill yao imeshalipwa, kucheki ni mimi... Dah basi tukaanza pale story baada ya story.

Madam ananiuliza vipi bana unafanya kazi wapi?? Nikamwambia bado sijaajiriwa Prof, akashangaa sasa imekuaje unaweza kuja huku na kutumbua pesa. Akawa ananilaumu nimesoma Petroleum bure, bora ningesoma hata education hiyo mambo niwaachie watu wengine - kwamba niliwazibia watu wengine nafasi. Ndio nikamweleza kua kusoma petroleum kumenisaidia kuweza kua na uelewa mpana wa OIL hata sasa naweza kutrade OIL professionally. Nikaanza kumwambia mambo ya Spot Crude oil (USOIL.sp), Spot Brent Oil (UKOIL.sp), July Crude Oil (USOIL), July Brent Oil (UKOIL). Prof akabaki anatumbua macho - yani nimempoteza haelewi kitu.

Prof wangu nikaanza kumkamulia pindi pale - prof akawa anatikisa tu kichwa. Nikamwonesha trading platform yangu, yani ndio nikamchanganya kabisa - alivyoona figures ndio akachanganyikiwa kbs tena zikiwa ktk international currencies - yani 1/3 ya mshahara wake wa mwezi mimi naupata in few trading hours Edited: screen shot nilivyoTrade OIL ijumaa pekee

Yani Prof kawa very inspired, anatamani classes zianze hata leo... kachukua namba zng za simu kanitumia text za kutosha kua nisimsahau. Hahahaaa!!
 
Kaka na mm usinisahau pls!
Umetolea mfano rorya nikakumbuka home tulivyo!

Pls don't 4get me!
 
Ila Ontario kwa navyosoma andiko lako tu ulikosea kusoma Hiyo kitu ungesoma Public relation and marketing ungekuwa mbali sana kwa unavyowaita tu watakuja watake wasitake.
 
We kijana utakuja kuua watu kwa presha wewe[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
By the way naomba umtaje yule Broker anayetoa 25% baada ya kufungua akaunti!!
 
Ila Ontario kwa navyosoma andiko lako tu ulikosea kusoma Hiyo kitu ungesoma Public relation and marketing ungekuwa mbali sana kwa unavyowaita tu watakuja watake wasitake.

Boss huko mbali ni wapi - ni umbali gani kutoka hapa nilipo sasa - marketers waliomaliza UDBS 2016 wapo wapi now??

Mimi ni adventurous boy yani tangu zamani, penda sana kufanya mavitu ambayo watu wengine hawayafanyi kwa visingizio visivyomake sense. Kitu kama marketing ni kitu ambacho ni very dime-store, ukisoma vitabu viwili vya Seth Godin, biography ya Steve Jobs na ukisubscribe web ya Gary Vaynerchuk unaimaster A-Z. Tofauti na kitu kama Petroleum ambayo inabidi uchimbe na kuchimbua ili uwe vzr.

Afu bana kusoma Public relationship ingekua kama humiliation kwa hustle za advance. Nilisoma one of the worst schools hapa bongo, nikakomaa kinyama nikapata one of the top most scores nchini, ndio ikawa tiketi ya kusoma Oil & Gas. Sasa kusoma PR ingekua ni kudhalilisha my hustle aisee!!
 
We kijana utakuja kuua watu kwa presha wewe[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
By the way naomba umtaje yule Broker anayetoa 25% baada ya kufungua akaunti!!
Unajua boss kama umegundua kuna baadhi ya info nimekwepa sana kuzishare - nina sababu zangu. Forex is big boys' game. Unacheza na pesa ambazo sijui umezitoa ktk mazingira gani, sijui hustle uliyotumia. Forex unatengeneza pesa - una download pesa, pia forex unapoteza pesa kama mvuke, in a milli second ushapoteza $1000.

Najua kuna info nikitoa watu vidole vinawawasha, wamesoma chapter 2 za trading on the zone, na kuangalia YouTube wanahisi wamekua gurus tyr. Sasa nikitoa info zote kuna watu wataenda kuchinjwa na soko, kisha mimi nitakuja kutukanwa hapa bila sababu. Kitu ambacho sikitaki in my life. Ndio maana hata walioingia live wakikutana na manyota nyota ya sokoni hawawezi kuja kunilaumu, coz it was on their own risk. Lkn naamini mtu akiwa vzr, akausoma mchezo vzr basi ni ngumh kuchoma account mara 1. Hiyo stage 98% ya nyinyi hamjafika - ndio maana sitaki kuzungumza vitu vyote kuepusha lawama.

Pia nakukumbusha... Books will give u only 40% ya unachotaka kukijua kuhusu forex, the market will give u the remaining 60% ya unachotaka kukijua sasa ukiingia kwa mihemuko utatoka na mihemuko pia. Na pia utafahamu skills nyingi sana sana sana - But what matters most in forex ni the skill of Buying and selling, lkn ili wewe ufanikiwe unahitaji 10% tu ya trading skills hizo 90% ni psychology, narudia psychology.
 
Kwako ww Ku master marketing ni kumsoma Steve jobs,Soma vitabu vya Marketing Strategic utagundua unachokifanya ni Marketing na advanced Public relation Marketing ina deal na strategies ndizo unazotumia sisemi ni vibaya ila tu nimependa mbinu unazotumia.
 
Habari yako mkuu ONTARIO

1.Nimesoma cooment yako ya nyuma kwamba ulitrade mafuta, Hapa umenuchanganya sana maana i thought forex inahusisha tu pesa za nchi mbali mbali na wala sio mafuta.

2. Mpaka sasa nimeshindwa kupata vitabu vya forex, Ka vp naomba unipe list nivishushe.

Ni hayo tu ambayo ningeomba unieleweshe
 


Mkuu ONTARIO kwanza nianze kwa kusema asante sana hasa kwa kutumia dakika zako ulizopewa na Mungu siku ya leo ku-spot makosa ambayo wenda yangeendelea kuwa na madhara sio kwangu tu hata kwa member wengine(bila kujali ni mzoefu au lah)!

Kwangu mimi hamna kitu nathamini kama TIME, kama mtu kutumia muda wake ku-add value katika maisha ya wengine!!!

Once again shukran sana mkuu!!

Pili, It is a mistake that I commit several times (I must admit this), na kupitia haya makosa tunayoyafanya leo ndio tunakua bora kesho!! Hii ni kosa ambalo nililifanya likani-cost kipindi flani na mpaka naandika hapa nilika sijui kama ni moja ya makosa!! Boss, watu wali-risk mengi mpaka leo hii tuna Tanzania iliyo huru, naimani hili kosa nilililofanya litakua fundisho sio kwangu tu bali na kwa wengine pia!!

Zaidi ya yote ningeomba maelezo zaidi katika hii paragraph...


-Nimeelewa uliposema nisinunue na kuuza the same currency kwa muda mmoja!

-Mfano, Je ni sahihi kununua EURUSD na kuuza EURGBP at once??

-Je ni sahihi kuuza EURUSD na kuuza EURGBP??

Tuendelee kuwekana sawa mkuu na kukumbushana pale inapobidi!!
 

Kwa nilivyomuelewa hapo katika kununua XAU/USD na kuuza AUD/USD Technically haiwezi kuwa sawa kwa sababu kimahesabu utakuwa umezicancel position zako. Ukiangalia katika hizo pair zote, USD ni counter currency na ipo katika denominator. Na unaposema unabuy maana yake utapatafaida price ikienda juu, na price ikienda juu maana yake ni kwamba denominator/USD inakuwa imepungua thamani dhidi ya currency iliyokuwa katika Numerator. Na unaposema unasell maana yake ili wewe upate faida ni lazima price ishuke, na price ikishuka maana yake USD inakuwa imepanda thamani dhidi ya currency iliyo katika numerator.

Ukiangalia hapo logicaly na technicaly, lazima position moja uloose.
 
soma walau page 20 za awali za thread utakutana na vitabu viwili,ukiendelea mpaka mwisho utakutana na vingine,inawezekana kumaliza hii thread yote kwa kuisoma ,rejea mtaka cha uvunguni......
 
Maelezo mazuri, acha nifwatilie zaidi! shukrani sana mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…