Weekend bhana, leo nimefurahi sana
Unajua bana mimi chuo nilisoma BSc.
Petroleum Chemistry hapo UDSM, basically hii ni sayansi inayohusika na refinery ya gas na mafuta. Yani crude gas and oil tunazibadili kua final usable products kama LPG, CNG, Ammonia, ammonium fertiliser, mambo ya diesel, jet fuel, gasoline nk nk. Hapo chuo tulikua wachache watu kama 21 hivi, so Prof ni rahisi kujua darasa zima.
Sasa tulikua na Prof mmoja, alikua kama mama'etu. Yani kwenye pindi lake alikua anatuPump vby mno na kututamanisha kuhusu hii field yetu, kua kuna pesa vby mno, site kuna marupurupu, incentives, mishahara ya kibabe... Basi kila akiwa anakuja pindi watu wanatamani kumsikiliza yule mama, anafundisha kidogo anaruka kwenye mambo ya site, michongo na madili ya gas na mafuta... yani hapo sisi tunakua tunahamasika vby mno, yani tukampendaga bure yule mama. Akawa kama rafiki yetu, akawa academic advisor wa karibia sisi wote... yani she was more than a friend.
Leo bana kuanzia saa 5 asubuhi nilikua Golden Tulip na mtu wangu wa faida. Tumekaa pale, tumezungumza sana, tukala lunch na kila kitu. Mchana mida ya saa 8.30 akaja huyu Prof wangu wa chuo, nikamuona ila yeye hakuniona. Akawasha PC yake akaagiza kinywaji, akaendelea na shughuli zake, baadae kidogo akaja mwenzie ambae ni km mzungu wakaagiza misosi wakawa wanakula.
Mimi nikamshtua muhudumu, nikamwambia yule mama pale nipo nae, so anipe bill yake. Bill ikaletwa nikailipia... Baadae Prof anataka kulipa ndio anaambiwa tyr bill yao imeshalipwa, kucheki ni mimi... Dah basi tukaanza pale story baada ya story.
Madam ananiuliza vipi bana unafanya kazi wapi?? Nikamwambia bado sijaajiriwa Prof, akashangaa sasa imekuaje unaweza kuja huku na kutumbua pesa. Akawa ananilaumu nimesoma Petroleum bure, bora ningesoma hata education hiyo mambo niwaachie watu wengine - kwamba niliwazibia watu wengine nafasi. Ndio nikamweleza kua kusoma petroleum kumenisaidia kuweza kua na uelewa mpana wa OIL hata sasa naweza kutrade OIL professionally. Nikaanza kumwambia mambo ya Spot Crude oil (USOIL.sp), Spot Brent Oil (UKOIL.sp), July Crude Oil (USOIL), July Brent Oil (UKOIL). Prof akabaki anatumbua macho - yani nimempoteza haelewi kitu.
Prof wangu nikaanza kumkamulia pindi pale - prof akawa anatikisa tu kichwa. Nikamwonesha trading platform yangu, yani ndio nikamchanganya kabisa - alivyoona figures ndio akachanganyikiwa kbs tena zikiwa ktk international currencies - yani 1/3 ya mshahara wake wa mwezi mimi naupata in few trading hours
Edited: screen shot nilivyoTrade OIL ijumaa pekee
Yani Prof kawa very inspired, anatamani classes zianze hata leo... kachukua namba zng za simu kanitumia text za kutosha kua nisimsahau. Hahahaaa!!