Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Jibu hoja MATUSI hayana tija Mkuu!!
Ujue ugonvi wangu na wewe uko wapi? hivi nikipandisha post zote za nyuma si utasema mimi mchawi?
Post zangu zina ufanano sana sasa sasa nikipost kwa sasa ni kwamba napingana na kitu fulani.

Nafanya jitihada zipandw zote kama nitaweza then uone halafu ulinganishe na za wakati huu then ulete majibu
 
Ujue ugonvi wangu na wewe uko wapi?


Sina ugomvi na wewe ninachokikataa ni MATUSI yako unayonitumia kwa PM, hoja zote ziko hapa iwaje wewe unifuate kwa PM na kiniporomoshea matusi?

Huo ndo udhaifu wako, bishana kwa hoja, hata mimi nilikuwa siijui Forex nashukuru wenye uelewa nayo wametufungua Macho na nilishawishika kuikubali baada ya kusoma hoja za msingi na mimi kufanya utafiti wa kutosha kupitia vyanzo mbali mbali ndiyo nikaikubali.

Nyinyi mnaoipinga hamna hoja za msingi bali ni matusi kwa PM na maneno ya shombo Jukwaani basi. Hivi unafikiri nani anaweza kushawishika na hoja zenu mufilisi? Kijana jifunze kutokana na makosa yako unaowaparamia wengine si saizi yako! Wewe endelea kuuza Kuku na Mayai haya mambo mengine huyawezi, forex is not for everyone! Maisha yanachangamoto zake usilazimishe usichokiweza utaumbuka.

Mwisho nikupe tena tahadhari sihitaji unitumie PM za matusi, period!!!
 
wewe tangu juzi unanifuatilia tu. nikakuambia post zangu ziko hivyo na bado ninazo nyingi tu mkuu za muelekeo huo
 
Salaam wana jukwaa,

Naona tangu TMT ianzishwe kumekuwa na hamasa kubwa katika kutaka kuitumia fursa hii na wengine wamekuwa na mashaka nayo huku wengine wakitumia hisia za mashaka kuipinga na wengine kupinga kinachofanywa na TMT.

Binafsi naona mwisho wa haya malumbano ni kupata majibu ya maswali yafuatayo:

1. TMT imesajiriwa na BRELA? Na je ilisajiwa kwa ajili ya kutoa huduma zipi? Je inafanya mambo kinyume na yale iliyosajiriwa kwayo?

2. Tofauti na ada ya kujifunza kuhusu Forex, je ipo fedha nyingine inayotozwa?

3. Je wakati wa live trading unafika wanakulazimisha kujiunga na broker wanayemtaka wao au una uhuru wa kuchagua broker?

4. Na kama wanakushawishi utumie broker wao, je usimtumia huyo ukachagua mwingine wanaendelea kukupa mentorship kama wale wanaotumia broker suggested by TMT?

5. Je broker wanayemshauri/mtaka atumike amesajiriwa na nchi anakotoka? Ana historia yoyote mbaya ya kufanya/kujaribu kufanya frauds?

6. Is FOREX real(this was to be the first question)

Kama akipata majibu ya hayo maswali utafanya maamuzi mazuri sana.
 
Uko vizuri kwa hoja na ndivyo tunavyohitaji Mkuu si kama wengine hawana hoja na kulazimisha tu wenzao wawaamini kuwa Forex ni Scam kumbe wana agenda zingine nyuma ya pazia.
 
Are TMT a broker to say that they will steal money of people?

And in your news is there anywhere they mention TMT as a scam?
 
Bado unatapatapa? pole sana
 
Reactions: 911
Uchu wa kupata utajiri haraka haraka hauwezi kumwacha mhusika salama.

Michezo yote ya kuwekeza fedha ni kama bahati nasibu ni pata potea.

Hakuna mahali popote unaweza kuwa tajiri pasipo kufanya kazi labda uibe au ufanye udanganyifu kwa wanaodanganyika.
 
1. TMT imesajiriwa na BRELA? Na je ilisajiwa kwa ajili ya kutoa huduma zipi? Je inafanya mambo kinyume na yale iliyosajiriwa kwayo?
Imesaliwa na wanalipa kodi TRA kama kawaida, Fuatilia alichoandika hapa.
Kwenye hii Link: Bringing FOREX from the world to Tanzania - The road to financial freedom
2. Tofauti na ada ya kujifunza kuhusu Forex, je ipo fedha nyingine inayotozwa?
Hakuna tozo jingine lolote.
Wewe binafsi baada ya kupata mafunzo, ni uamuzi wako ni kiasi gani cha fedha utaanza nacho kama mtaji. Hii ni fedha yako.
3. Je wakati wa live trading unafika wanakulazimisha kujiunga na broker wanayemtaka wao au una uhuru wa kuchagua broker?
Hakuna anaye lazimishwa. Ila utapewa ushauri kwa nini utumie broker flani. Hivyo uamuzi bado ni weako katika hili.
4. Na kama wanakushawishi utumie broker wao, je usimtumia huyo ukachagua mwingine wanaendelea kukupa mentorship kama wale wanaotumia broker suggested by TMT?
Hapa utahitajika ufafanuzi toka kwa ONTARIO
5. Je broker wanayemshauri/mtaka atumike amesajiriwa na nchi anakotoka? Ana historia yoyote mbaya ya kufanya/kujaribu kufanya frauds?
Amesajiriwa na yuko regulated. Ni broker pekee kwa Africa anayefanya vizuri. Ukiwa na uwezo wa kuwithdraw fedha ndani ya masaa 2 hadi 6. Kumbuka broker wengine wote huwa ni kuanzia siku 3 hadi 7 ndio unapata fedha yako.
6. Is FOREX real(this was to be the first question)
Kutokana na uwepo wa thread nyingi kuhusu Forex hapa JF, sikutegemea uwepo wa hili swali.

Ninamashaka kuwa hii thread na comment zake hujaisoma: Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!
Pia jaribu hata kutumia Google utapata majibu stahiki.

Kimsingi FOREX imekuwa ikifanywa kwa muda mrefu na Taasisi kubwa za kifedha hapa nchini na mataifa mengine.

Na kwa mtu mmoja mmoja ilikuwa ni siri kwa walio wengi kwa hapa nchini.

Ila ni kitu cha kawaida kwa mataifa mengine. Ontario ndio aliyetufungua macho kwa kuierezea kwa kina na wengi tukaelewa na kuchukua hatua.

Kibaya zaidi wengi walimlaumu kwa nini ameweka wazi JF, yaani kwa nini amemwaga mchele kwa kuku wengi.
 
Umeifungua hii ID mpya ( 9 October 2017) maalum kwaajili ya kuponda forex. Nakushauri ili ueleweke vizuri tumia ile ID yako ya zamani
 
majibu murua sana
 
Mkuu nkuelewa vizuri. Na msingi wa kupose hayo maswali ni kumsaidia mtu ambaye anapinga kuhusu hili swala linalofanywa na TMT. Mimi niko nao na nategemea kutoka huku kwetu Bukoba niende Dar au Dodoma kwa ajili ya Training. Kwa bahati mbaya sana sikuweza kujoin program ya kwanza.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…