Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
The primary aim ya bureau de change ni kwa ajili ubadilishaji wa pesa za kigeni ambao pesa huwa ni kwa ajili ya matumizi mengine mfano kufacilitate international trade. ukienda kwa lengo la "speculative" ww tayari umeshajiingiza kwenye kamali.
Watu wengine bwana... Kwa hiyo uuzaji na ununuaji wa hisa na bond ni kamari?
 
Pesa kamwe haiwezi ikawa bidhaa pesa ni kwa ajili ya medium of exchange. Unazungumzia mimi kuhusu basics za hii betting nimesoma mpaka kukaa kufuatilia mambo mengi tu yanayohusu financial markets siyo hii betting tu mnayofanya.

Kabla ya hapo kulikuwa kuna mkata wa Bretton Woods agreement ambapo huu uliwapa ugumu wacheza kamali("speculators") kujihusisha na trading kwa maana lengo la foreign exchange lilikuwa ni kwa ajili ku-overseas travel na biashashara ya kimataifa.

Baada ya huu mkata kuvunjika mwaka 1970 na demand ya foreign exchange kuongezeka hapo ndipo financial institutions zilipoona kwamba hii ni fursa mpya ya kutengeneza kwa njia ya "speculation" ambayo hii inaenda kinyume na lengo la mwanzo kabisa la foreign exchange.

Sasa leo hii 90% ya foreign exchange inafanywa kwa ajili ya speculation tu ambapo 5% tu ndio inafanywa kwa ajili ya lile lango la mwazoni la kuisaidia international trade, malipo na mambo ya kusafiri nje ya nchi, hii ndio lilikuwa lengo la fore.x. hakuna njia unaweza tenganisha fore.x trading na gambling hii ni advanced form of betting.
 
Haijalishi kuwa inafanywa nani kwamba ndio iwe au isiwe gambling bali fore.x haina misingi ya kuitwa biashara na nimekotolea aina mojawapo ya fore.x ambayo ni spread betting . hakuna njia mnaweza tenganisha fore.x na kamali.
 
Wakati kitimoto/nguruwe ni haramu kwa baadhi ya watu duniani kwa wengineo ni halali,vile vile kwa watu wengi duniani mbwa ni haramu na haliwi basi kuna baadhi ya watu,na tunasikia baadhi ya wachina wanakula mbwa.mifano ni mingi tu.Forex inaweza kuwa gambling kwa baadhi ya watu na inaweza kuwa biashara kwa watu wengine.Kama ilivyo ngada ni haramu kwetu lakini kuna makundi ya watu hasa hasa Amerika ya kusini kwao ni biashara mubashara kabisa.Kwangu mimi uhalali au uharamu wa kitu ni mtazamo wa mtu binafsi au jamii fulani tu.Cha msingi kuhusu Forex ni kuwa kweli ipo na inahitaji umahiri wa kuijua basics and fundamentals zake,na humo humo kwenye Forex forest kuna matapeli wengi tu.
 
Maelezo kwa ufupi.
Forex ni soko la kimataifa la biashara ya sarafu. Soko hili huamua viwango vya ubadilishaji wa sarafu za kigeni, huku, likijumuisha vipengele vyote vya kununua, kuuza na kubadilishana fedha kwa bei za sasa au zilizopangwa. Kwa upande wa biashara hiyo ni soko kubwa zaidi duniani, likifuatiwa na soko la Mikopo (credit market)

Washiriki wakuu katika soko hili ni mabenki makubwa ya kimataifa, pamoja na vituo vya kifedha kote ulimwenguni vikifanya kazi kama nanga za biashara kati ya aina nyingi za wanunuzi na wauzaji muda wote isipokuwa mwishoni mwa wiki.

Kwa kuwa sarafu zinazoteuliwa huwa kakatika pea, soko la fedha za kigeni halitekeleza thamani kamili ya sarafu na badala yake huamua kukadiria thamani yake ya karibu kwa kuweka bei ya soko ya sarafu moja ikiwa imelipwa kwa mfano $ dola moja ina thamani ya Tsh. Kadhaa nk.

Ila kuwa makini kwa siku za karibuni kumekuwa na vikampuni mbalimbali vinavyowashawishi watu kujiunga na kile ambacho hukitaja kama biashara ya kimataifa wakitaka uchague ama Forex au Binary options tambua kuwa kampuni hizi hazina tofauti DESI YAANI KUPANDA MBEGU na kama ukijiunga nao usishangae yakikutokea ya DESI.

Naomba kuwasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…