Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Bro mim na umri kama wako na nilipoteza pesa 1.2million ilipotea hivihiv sikirudisha hata 100 mkuu sikuvuna faida yake hata theluthi.. huwa sitak hata kukumbuka na wala sijawahi kumsimulia mtu yoyote wa karibu kwakua nataka nisahau...

Ila nimejifunza kuwa hakuna pesa rahis na sasa imenijengea kitu kimoja cha kutokumuamin mtu yoyote... Kuwa makin usije kupoteza na hiyo pesa uliyoipata kwa ushawish ambao ni mbovu.
 
Nunua Bajaji hutojutia piga mwenyewe inayobaki chukua kiwanja zungusha fensi anza kufuga mifugo ngombe nguruwe n.k achana na kamali
 
Una roho ya aina gani wewe?
 
Dah naumiaga sana kusikia habari kama hii.
Ukavu macho unawapotezea sana muda vijana. Forex ni "ponzi scheme" ya karne hii.
 
Dah naumiaga sana kusikia habari kama hii.
Ukavu macho unawapotezea sana muda vijana. Forex ni "ponzi scheme" ya karne hii.
Mkuu ulishawahi kujihusisha na forex trading?
 
Haupati mahusiano yeyote au kariba kati ya FX na "Ponzi scheme"?
Ndio mkuu, ndio maana kwanza nilianza kukuuliza swali pengine nikajua hujui unachokizungumzia.

Unajua unaposema tu neno ponzi scheme. Lazima ihusishe group of people ambao wako katika stream fulani ili biashara ifanyike. Nitofauti kabisa na forex ambayo huitaji mtu yoyote bali wewe mwenyewe.
 

Sasa una "trade" nini?
Biashara halisi ni "three P's" People,process to product. Sasa FX unatrade nini kwa nani?
Unajua maana ya "upatu"?
 
Sasa una "trade" nini?
Biashara halisi ni "three P's" People,process to product. Sasa FX unatrade nini kwa nani?
Unajua maana ya "upatu"?
Hitajio lako Biashara halishi au pesa??
 
Sasa una "trade" nini?
Biashara halisi ni "three P's" People,process to product. Sasa FX unatrade nini kwa nani?
Unajua maana ya "upatu"?
Mkuu kwenye forex tunatrade commodities karibia zote maize, cassava, gold, oil, crude oil, cotton ,Silva
Pia tunatrade currencies zoote usd,gbp, rand, euro etc
Kwenye stock market kuna vitu vingi asee siwezi andika vyote ebu ukipata nafasi jaribu kutembelea tovuti ya DSE usome kidogo kuhusu share,government bond, cooperate bonds,
Pia huku unaweza jihusisha kununua vipande vya makampuni makubwa mfano vodacom,crdb apple, Facebook, cocacola, Nike

Biashara sii tu kuchukua nyanya point A na kuziuza point B dunia inaenda kasi sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…