Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Okay. Kwa Program yako naamini unaweza kuwa Business Analyst, budget or research analyst. Kwa sasa kuna wafanya biashara wengi tu wanahitaji watu wanaoweza kuwasaidia biashara zao ziende vzuri.

Nashahuri jaribu kuangalia ni wapi watu wana changamoto za biashara za namna ya kuandaa budgets au wanaohitaji analysis ya biashara zao.

Wewe tumia ujuzi wako kuwasaidia na hapo ndipo utakuwa umejiwekea mazingira mazuri ya kupata wateja watakaokulipa fedha nyingi sana kwa kila project utakayofanya.

Kuanzisha huduma zako haichukui mwaka au miezi, ni siku utakapoamua kuanza utaanza kupata wateja tena wengi sana.

Niamini, anza leo utaona faida yake. Biashara nzuri siku zote ni ile unayotatua changamoto za watu sio lazima uuze bidhaa, anza kuuza huduma ndugu yangu.

According to your definition of good business, Je unawasemeaje akina warren buffet na Soros ambao hawatoi servise wala kuuza bidhaa? Je wao hawafanyi biashara nzuri?
 
According to your definition of good business, Je unawasemeaje akina warren buffet na Soros ambao hawatoi servise wala kuuza bidhaa? Je wao hawafanyi biashara nzuri?
When you talk about business, you must offer either a service of a product with monetary exchange for modern businesses. Na ili kile unachokiuza kinunuliwe, lazima kihitajike na kundi fulani la watu, ndiyo maana nikamshahuri rafiki yangu kuwa si lazima atafute biashara ya kuuza bidhaa, anaweza kuuza hata huduma.
Na ukweli ni kwamba, kama biashara yako haina utatuzi wa changamoto kwa kundi ulilolenga haiwezi kuwa biashara nzuri maana itakufa tu. Ili iwe biashara nzuri lazima wale ulowalenga kama wateja wako wawe tayari kulipia kile unachokiuza na ili walipe lazima bidhaa au huduma yako iwe na uwezo wa kutatua changamoto walizonazo.
Nahisi utakuwa na miss interpretation ya huduma ndiyo maana ukatoa mfano wa Buffet wakati huyo Buffet unayemsemea ana makampuni zaidi ya 6 anayoendesha sasa sijapata Logic ya swali lako.
 
Wewe ngedere acha upuuzi wewe Kama umeijua forex kuanzia 2019 ni wewe na hao wapuuzi wenzio. Wenzio tumeijua tangu 2009 , na Kuna wabongo kibao wameijua long time eti unakuja kusema ndio inachupa ...



Kichwa maji weww

Sent using Jamii Forums mobile app
Daa asee wee kiazi unajua unachekesha sana

Sasa mimi hiyo 2009 inanisaidia nini

Mimi nakwambia wewe ni mjinga unasema eti 2021 mtabaki 100 kadanganye hao mafala wenzako sio mimi

Kifupi hata ungekuwa umeenza BC mimi forex huna kipya cha cha kuniambia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna biashara ningekushauri lkini kwa experience hiyo ngoja kwanza
 
kuna biashara ningekushauri lkini kwa experience hiyo ngoja kwanza
Mkuu shukran sana kwa moyo huo

Huu uzi ni wa muda kidogo nilifanikiwa sana kupata ushauri wa kimawazo na connection pia

Nilifanikiwa kuanzisha biashara yangu tena kwa kushikwa mkono maana huo mtaji hapo juu ulikuwa hautoshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
When you talk about business, you must offer either a service of a product with monetary exchange for modern businesses. Na ili kile unachokiuza kinunuliwe, lazima kihitajike na kundi fulani la watu, ndiyo maana nikamshahuri rafiki yangu kuwa si lazima atafute biashara ya kuuza bidhaa, anaweza kuuza hata huduma.
Na ukweli ni kwamba, kama biashara yako haina utatuzi wa changamoto kwa kundi ulilolenga haiwezi kuwa biashara nzuri maana itakufa tu. Ili iwe biashara nzuri lazima wale ulowalenga kama wateja wako wawe tayari kulipia kile unachokiuza na ili walipe lazima bidhaa au huduma yako iwe na uwezo wa kutatua changamoto walizonazo.
Nahisi utakuwa na miss interpretation ya huduma ndiyo maana ukatoa mfano wa Buffet wakati huyo Buffet unayemsemea ana makampuni zaidi ya 6 anayoendesha sasa sijapata Logic ya swali lako.
Huduma gani buffet na soros wanatoa mkuu? Inajulikana wawekezaji na wafanya bisashara katika hisa (buffet) na hedge fund/forex (soros) ndio maana nikauliza je wao hawafanyi biashara nzuri kwa mujibu wa definition yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
When you talk about business, you must offer either a service of a product with monetary exchange for modern businesses. Na ili kile unachokiuza kinunuliwe, lazima kihitajike na kundi fulani la watu, ndiyo maana nikamshahuri rafiki yangu kuwa si lazima atafute biashara ya kuuza bidhaa, anaweza kuuza hata huduma.
Na ukweli ni kwamba, kama biashara yako haina utatuzi wa changamoto kwa kundi ulilolenga haiwezi kuwa biashara nzuri maana itakufa tu. Ili iwe biashara nzuri lazima wale ulowalenga kama wateja wako wawe tayari kulipia kile unachokiuza na ili walipe lazima bidhaa au huduma yako iwe na uwezo wa kutatua changamoto walizonazo.
Nahisi utakuwa na miss interpretation ya huduma ndiyo maana ukatoa mfano wa Buffet wakati huyo Buffet unayemsemea ana makampuni zaidi ya 6 anayoendesha sasa sijapata Logic ya swali lako.
Mkuu ushauri mzuri sana

Nitaufanyia kazi japo kwa sasa nadili na bidhaa moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forex ni 50/50 , upande mmoja gambling upande Mwingine knowledge hii ni Kwa sababu kuna watu maalum wanaocontrol soko.....
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi ni kijana umri miaka 23 nimehitimu chuo mwaka huu .lakini kutokana na changamoto za ajira vijana wengi tumekuwa tukitafuta njia tofauti tofauti za kutokea ilimradi tupunguze ukali wa njaa iliyoko mtaani.

Kifupi wakati nilikuwa nasoma nilikuwa na hofu sana kuwa nikimaliza masomo yangu nitafanya nini nisipopata Ajira kitu ambacho kilinifanya niwe nachukua muda mwingi hapa jamii forum kusoma mada mbalimbali za baishara kilimo na ujasiliamali.

Mwaka 2017 wakati niko likizo nimemaliza mwaka wa kwanza nilipata kusoma mada inayohusu forex humu jukwaan kwakweli nilihamasika sana japo nilikuwa sina uwezo wa kuhudhuria mafunzo nilisema nitakomaa mwenyewe mpaka nielewe ,nilitumia muda mwingi youtube kudownload vitabu na kusoma mpaka nikapata mwanga kidogo.

Wakati tunaenda Kuanza mwaka wa pili kumbe kunajamaa yangu alihudhuria mafunzo kabisa akaanza kutupa muongozo namna soko linavyofanya kazi ukweli kutokana na tamaa ya kupata pesa tuliunda kikundi kila mmoja akafungua acc baada ya boom kutoka tukadeposite nakuanza kutrade.

Tulitumia muda mwingi kujadili forex mimi na wenzangu kuliko kituchochote kusoma ilikuwa kama part time muda wote unakuta tumekodolea macho kwenye simu nakufanya analysis kuhusiana na currencies tofauti.

Mbali na hapo tulikuwa tukijadili jinsi tutakavyo nunua magari makali siku ya graduation tuendenayo mlimani city .Halafu tukimaliza tukodishe ofisi kwenye lile jengo refu pembeni ya mawasiliano tower tuwe tunafundisha watu kuhusu foreign exchange.

Lakini kadri ya siku zilivyokuwa zinazidi ndio soko lilivyokuwa linazidi kuwa gumu maana Leo umepata faida dola 100 kesho umepigwa dola 150 ,kesho umeingiza 50 kesho kutwa umepigwa 100 maisha yalienda hivyo performance kwenye masomo ikashuka lakini hatukujali kwani tulijua kwa usawa wa magu ajira hakuna ,bora tukomae na forex ipo siku tutatoka.

Kifupi mpaka kufika mwaka wa tatu jamaa zangu walikuwa na madeni makubwa maana walianza kuchukua pesa kwa wanafunzi wengine wanatrade kwa riba na pesa zinaungua tu walianza kuuza vitu vya ndani laptop freezer subwoofer ili waongezee pesa za mtaji na wafidie madeni, wakati huo mimi bado nilikuwa nimebebana na jamaa yangu mabibo hostel wote 3rd year.

Nilikaa nikafikiri maisha ya nyumbani sio mazuri na forex ndio nilijua itanitoa kimaisha japokuwa inachangamoto ndogondogo nikiangalia acc ya benki sina hata shilingi zaidi ya pesa ya kula maboom nimebaki nayo mawili nikasema nijibane hiyopesa niichanganye ifike milioni moja nitrade kwa uangalifu labda itanitoa maana niliamini million 1 inakaribia kwenye dola 500 .

Asee sijui ilikuwa ni bahati maana nilichanganya zote nikatrade nikapata kama dola 2600 ndani ya kama wiki 3 maana nilikuwa nafungua tu order na risk management nilikuwa sifanyi vizuri ,nilitoa dola 1300 kama million 3 hivi nikaenda riverside nikapanga chumba self 100000 per month ndio napoka mpaka sasa ,kwa miezi sita nikanunua kitanda godoro, nikanunua TV 500k, feni, gesi, meza na viti, subwoofer,Friji getto likajaaa .

Kwenye Trading acc nilibaki na dola 1300 nikasema hii siwezi poteza nitakuwa na trade natoa pesa kidogo kidogo hata dola 50 per day ambayo ni zaidi ya 100k nikaona maisha nimeyapatia sisumbuki kutafuta kazi nikutrade full time .nikawa nikiingia humu jamii forum natafuta ule uzi wa magari mazuri naangalia nikijua anytime navuta mkoko.

Daa baada ya kumaliza chuo nikawa mimi na soko ,soko na mimi nilijitahidi nikapandisha acc mpaka dola 1600

Asee siku ya mkosi ilivyofika ilikuwa ni kwenye muda wa saa 1 1 jion kulikuwa na newz ya gbp nimeingia na kama lotsize ya 1 forex trader mnanielewa vizuri soko lilienda agaist na mimi nikajikuta naongeza tena lot ya 1 huwezi amini pesa yote ilichomeka sikubaki hata na Mia kwenye acc

Nilihisi kuchanganyikiwa na ukubwa wote nilionao nililia kama mtoto mdogo siku pata usingizi siku nzima huku lawama zote nikimtupia mungu kwa nini ameruhusu pesa yote zaidi ya 3.7m kupotea ndani ya masaa machache.

Pesa niliokuwa nimebakinayo mpesa ilikuwa laki 4 kwa kile kipigo niliogopa kurudisha hiyo pesa kwenye forex kwani ilikuwa haifika hata dola 200 nikaanza kujiuliza nitaishi vipi hapa town na sina mtu hata wakuomba sh 100 . Nikaanza kuona simu za mama nazikwepa kwani nilikuwa nimezoea kumtumia pesa nashindwa akiniomba nitafanyaje.

Baasi nikatafuta rafiki yangu alikuwa anauza karoti ilala boma kwenye meza najua wenyeji wapale wanaelewa vizuri nikwamwabia anitafutie eneo kweli akaniambia per day meza unalipia 1000 na ushuru sasa mwenye meza anataka 60k ya miezi miwili nikasema poah ,nikampatia jamaa yangu pesa .

Akaniambia mwenye eneo amesema mkataba wa mtu anaetakiwa kuondoka unaisha baada ya siku 3. zikifika nikaanze biashara nikaenda kununua mzani kkoo wa kupimia 80k daa nilisubiria eneo jamaa aliekuwa anatakiwa kunipisha haondoki nikawa nimetapeliwa hivyo. Jamaa yangu kwa kuona hivyo akaniambia twende tukashitaki polisi turudishiwe pesa yetu.

Nikafikiria pesa niliyopoteza 3.7m kwa 60k nikaamua nipotezeee ,yule jamaa yangu akahisi labda anamakosa akaniambia kwenye meza yake niwe nachukua mzigo tunachanganya nikakubali lakini profit perday ilikuwa tunapata kama 15k nikaona namzibia jamaa riziki yake nikamwabia nimepata kazi mahali nikaondoka na mzani nikamuachia.

Nikarudi kukaa geto mpesa nikawa nimebaki na 170000 nikasema nizunguke hata kwenye karakana za furniture labda naweza kupata kazi huku nikijifunza wapi ,viwanda vya matofali unakutana na vibarua tu wanapiga kazi.

Nikahisi kukata tamaa nikatafuta kila njia ikashindikana nikasema nifanyeje nikapata wazo nijaribu kufanya betting kwani kipindi cha nyuma nilikuwa nafanya ndani ya wiki moja nikawa nimepoteza pesa yote hata pesa ya kula nikakosa ikabidi nimfate yule jamaa wa ilala nikamwabia kazi imebuma anipatie 30k nimuachie ule mzani akanipatia nikanunua msosi geto.

Huwa sina tabia ya kuuza vitu hovyo lakini nilitafuta mteja nikauza friji kwa bei ya hasara kama 300k hata miezi mitatu ilikuwa haija maliza, nikaendelea kubet .kila nilipikuwa naendelea kubet ndio pesa ilivyokuwa inazidi kupotea
kila siku kuliwa tu asee asikwambie mtu betting sio kazi ya kutegemea inaweza kukuaibisha muda wowote.

Mwezi uliopita kwenye tarehe 20s nikafuma mikeka mitatu siku moja yote nikala zaidi ya 8m siku hiyo siku lala kwa furaha nikiwithdraw kama 7m nikawa nazo getto nimetunza nilibakiza 1m nikabet tena yote nikala 1.5m .wiki ikiyopita nikabet 500k nikala 2.6m jumla nikawa na kwenye acc na 3.6m .
Juzi na Jana nimebet nikapoteza 1m nimeona nitoe 2.6m nichanganye na ile 7m iwe 9.6m.

Nimeona kwa hiki kiasi cha 9.6m najua humu kunawataalam wa biashara wanaweza kunisaidia kunipatia wazo ama ushauri nifanye biashara ipi maana mimi nilikuwa na wazo nifungue kaduka niwe nauza vinywaji vinywaji vikali nichanganyanye na soft drink. Ama nitafute sehemu niuze hata nafaka ila mtaji ndio sijui unahitajika shilingi ngapi.

Note biashara ambayo nimewahi kufanya tofauti na hizo kamali hapo juu ni ufugaki kuku tena zamani sana huko j4.

Nitashukuru sana kwa mchango wako wowote ule utakao utoa maana umri unasogea na majukumu yanazidi kuongezeka.


Sent using Jamii Forums mobile app
Una bahati Sana,umekimbia mjini very lucky,any way nunua mazao Kama huogopi.
 
Nafurahi Sana forex kuwapiga hasara watu kibao walio ivamia Kama uvamimizi wa nzige... Watu waliingia kwa mihemko wakapigwa hasara za hatari.


Kwasasa Hali imetulia tuliiii, webaki wakongwe kazi zinaendelea Kama kawaida. Nawaomba nyie vijana na wapenda kufanya kila fursa mnayoisikia. Kuwa kabla ya kufanya Kitu chochote fanyeni uchunguzi wa kina.


Nina amini mpaka 2021 forex Trader wa ukweli Tanzania nzima hawatafika 100.


Asante Mungu kwa kutuondolea takataka kwenye industry yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee wa TOP DOWN ANALYSIS ..nakuelewa sana mkuu[emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom