Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Hitajio lako Biashara halishi au pesa??
Mkuu kwenye forex tunatrade commodities karibia zote maize, cassava, gold, oil, crude oil, cotton ,Silva
Pia tunatrade currencies zoote usd,gbp, rand, euro etc
Kwenye stock market kuna vitu vingi asee siwezi andika vyote ebu ukipata nafasi jaribu kutembelea tovuti ya DSE usome kidogo kuhusu share,government bond, cooperate bonds,
Pia huku unaweza jihusisha kununua vipande vya makampuni makubwa mfano vodacom,crdb apple, Facebook, cocacola, Nike

Biashara sii tu kuchukua nyanya point A na kuziuza point B dunia inaenda kasi sana mkuu

Asante sana kwa kunielimisha mkuu.
Kwa iyo nikitaka ku "trade" hati fungani niwaone?
 
Asante sana kwa kunielimisha mkuu.
Kwa iyo nikitaka ku "trade" hati fungani niwaone?
Nenda Dar es salaam stock of exchange. Pia kama unapesa nyingi waweza wekeza kwenye vipande vya serikali. BOT wanatoa data za hayo maswala kila wiki unaweza pia watembelea ukapata data zaidi.
 
Kama stori hii ni kweli, una mkono na akili ya kamari ndugu. Tumia strategy uliyokuwa unatumia wakati una shida. Weka mental state ya umakini kama vile ulivyokuwa una shida.

Cheza na 10% ya hela yako katika hizo forex na kamari kidogo kidogo kama una laki. Una skills tayari za kufikisha 100m ila naona akili yako haijakubali kufunction vizuri muda wote mpaka iwe do or die.

Utapofika hapo 100m anza hayo mambo ya kudivertify. Kwa sasa endelea kuishi kidogokidogo. Hela utapata ila nasisitiza zisiingie akilinj. Ushafeli mara moja katika hilo usifeli tena. Usihame, usinunue gari, usiongeze allowance kwa mama, usigawe hela ovyo mpaka ufikishe 100m.
 
Tunza pesa mwez September uanze betting ya kboss,unatengeneza mikeka 10 kila mkeka wenye odds 3 afu unaweka stake ya 50,000 hapo ktk mikeka 10 ikiwin minne utakuwa umetengeneza 600,000 kwahyo utakuwa na faida ya 100,000 kwa siku
 
Ila nakusifu kwa kuwa na uwezo wa kuacha kamali pale unapoona inshu haziend Sawa,Kuna watu hawawez kujtuliza hata kwa WK moja
 
Mkuu hapo tafuta 1m upate 10m,uende voda wakupe uwakala(hii n biashara isiyo kuwa na hasara) location njoo huku kwetu mwanza Sengerema kijiwen
 
Duuh, si mchezo ila ninachojua pesa ya kamari haijawahi muacha mtu salama
 
Back
Top Bottom