Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Hata ukiweka position moja tu ya 0.02 kwenye 4hr au daily pia utachoma akaunti?
Ishu Ni kuwa stop loss utaweka tight Sana, na price huwa inacheza Sana, Sasa ikicheza kidogo tu ndio position Ina close unapata hasara

Nadhani dola 100 mtu uwe scalper tu
 
Kwa pesa iyo kama utaweza nunuwa gari ndogo ufanye uber nadhani biashara hii itakupa muda wa kutosha uku ukiendelea kupiga forex ,ist,vitz, used itakufaa
 
Ishu Ni kuwa stop loss utaweka tight Sana, na price huwa inacheza Sana, Sasa ikicheza kidogo tu ndio position Ina close unapata hasara

Nadhani dola 100 mtu uwe scalper tu
Kwani stop loss inaweza kuwa sawa tu na yule anayetrade na standard lot (1.0 lot). Kinachotofautisha kiasi unachorisk ni lot size unayoitumia. Chukulia kwamba tunatrade pair ya usd/jpy mimi na dolla mia nikiweka stop loss ya 30 pips kwa lot size ya 0.02 ina maana kama trade ikieenda vibaya nitapoteza roughly 6usd lakini wewe mwenye 1000usd+ ukiweka stoploss ya 30 pips na lot size ya 1.0 utapoteza 300 usd. So issue siyo stoploss pekee bali lot size pia unayotumia kutrade upatoze hela.
 
Kuwa scalper kwa 100usd ni kupoteza muda tu. Scalpers unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa kibongobongo kama 1000 usd au zaidi maana scalpers wengi wanatarget kupata pips kati ya 10-30 kwa kila trade hivyo ukiwa na mtaji mkubwa utakuwezesha kutrade lot kubwa na kupata profit kubwa ndani ya muda mfupi hiyo ndiyo maana halisi ya scalping.
 
Scalpers unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa kibongobongo kama 1000 usd au zaidi maana scalpers wengi wanatarget kupata pips kati ya 10-30 kwa kila trade hivyo ukiwa na mtaji mkubwa
#1. Swala sio mtaji katika scalping, Waweza ukawa na $100 na ukafanya vyema na pia waweza kuwa na $1000 ukashindwa kufanya vyema.

#2. Swala ni Entry sahihi, exit sahihi na kwa wakati sahihi katika Trading session sehihi husika.

Hii namba #2 ndio hutofautisha profitable trader na looser

#3. Imbalance ya pair husika kati ya seller na buyer , - Mfano hapa chini utaona USDCHF (Sell Scalping) iko vyema zaidi, pamoja na EURUSD ( Buy scalping )
1603555582408.png

1603555717154.png

---
Nina hakika point namba tatu hujanielewa kabisa.

Mfano hai: Scalping kwa 0.1 [ 5m TF ]
1603556076251.png
 
#1. Swala sio mtaji katika scalping, Waweza ukawa na $100 na ukafanya vyema na pia waweza kuwa na $1000 ukashindwa kufanya vyema.

#2. Swala ni Entry sahihi, exit sahihi na kwa wakati sahihi katika Trading session sehihi husika.

Hii namba #2 ndio hutofautisha profitable trader na looser

#3. Imbalance ya pair husika kati ya seller na buyer , - Mfano hapa chini utaona USDCHF (Sell Scalping) iko vyema zaidi, pamoja na EURUSD ( Buy scalping )
View attachment 1610771
View attachment 1610780
---
Nina hakika point namba tatu hujanielewa kabisa.
Utakuwaje fx trader kama huna system ya entry na exit? Kama huna hivyo vitu then wewe unafanya bahati nasibu. Kaka kama tayari una skills zinazotakiwa then mtaji una nafasi yake pia.

Huwezi kuniambia kwamba mwenye 10000 usd a/c anatrade sawa na mwnye 10 usd a/c kwa maana ya profit watakyoipata. Huwezi kulinganisha genge na supermarket kwa profit. The higher the investment the higher the return!
 
Mkuu kwenye forex tunatrade commodities karibia zote maize, cassava, gold, oil, crude oil, cotton ,Silva
Pia tunatrade currencies zoote usd,gbp, rand, euro etc
Kwenye stock market kuna vitu vingi asee siwezi andika vyote ebu ukipata nafasi jaribu kutembelea tovuti ya DSE usome kidogo kuhusu share,government bond, cooperate bonds,
Pia huku unaweza jihusisha kununua vipande vya makampuni makubwa mfano vodacom,crdb apple, Facebook, cocacola, Nike

Biashara sii tu kuchukua nyanya point A na kuziuza point B dunia inaenda kasi sana mkuu
Forex trading usiingilie Kama hunaelimu yake,tafuta Ada kasome elimu ya forex trading njoo u trade, la sivyo njoo DM nikupeleke group la Mafunzo la Forsage desensitized platform.
 
Forex is not getting reach quick thing chief inahitaji kusoma, kujifunza nakufanya practise yakutosha before kuinvest kiasi kikubwa cha pesa. Overal ukiwa mtu wavkuhitaji kupata hela chap chap aisee forex itakufanya kitu mbaya uta burn account kila saa
 
Kwa wale wapenzi wa Crude Oil , ni mwendo wa ku buy tuu. hii ndio faida ya ku trade bidhaa zinazotabirika uelekeo wake
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza mimi ni kijana umri miaka 23 nimehitimu chuo mwaka huu .lakini kutokana na changamoto za ajira vijana wengi tumekuwa tukitafuta njia tofauti tofauti za kutokea ilimradi tupunguze ukali wa njaa iliyoko mtaani.

Kifupi wakati nilikuwa nasoma nilikuwa na hofu sana kuwa nikimaliza masomo yangu nitafanya nini nisipopata Ajira kitu ambacho kilinifanya niwe nachukua muda mwingi hapa jamii forum kusoma mada mbalimbali za baishara kilimo na ujasiliamali.

Mwaka 2017 wakati niko likizo nimemaliza mwaka wa kwanza nilipata kusoma mada inayohusu forex humu jukwaan kwakweli nilihamasika sana japo nilikuwa sina uwezo wa kuhudhuria mafunzo nilisema nitakomaa mwenyewe mpaka nielewe ,nilitumia muda mwingi youtube kudownload vitabu na kusoma mpaka nikapata mwanga kidogo.

Wakati tunaenda Kuanza mwaka wa pili kumbe kunajamaa yangu alihudhuria mafunzo kabisa akaanza kutupa muongozo namna soko linavyofanya kazi ukweli kutokana na tamaa ya kupata pesa tuliunda kikundi kila mmoja akafungua acc baada ya boom kutoka tukadeposite nakuanza kutrade.

Tulitumia muda mwingi kujadili forex mimi na wenzangu kuliko kituchochote kusoma ilikuwa kama part time muda wote unakuta tumekodolea macho kwenye simu nakufanya analysis kuhusiana na currencies tofauti.

Mbali na hapo tulikuwa tukijadili jinsi tutakavyo nunua magari makali siku ya graduation tuendenayo mlimani city .Halafu tukimaliza tukodishe ofisi kwenye lile jengo refu pembeni ya mawasiliano tower tuwe tunafundisha watu kuhusu foreign exchange.

Lakini kadri ya siku zilivyokuwa zinazidi ndio soko lilivyokuwa linazidi kuwa gumu maana Leo umepata faida dola 100 kesho umepigwa dola 150 ,kesho umeingiza 50 kesho kutwa umepigwa 100 maisha yalienda hivyo performance kwenye masomo ikashuka lakini hatukujali kwani tulijua kwa usawa wa magu ajira hakuna ,bora tukomae na forex ipo siku tutatoka.

Kifupi mpaka kufika mwaka wa tatu jamaa zangu walikuwa na madeni makubwa maana walianza kuchukua pesa kwa wanafunzi wengine wanatrade kwa riba na pesa zinaungua tu walianza kuuza vitu vya ndani laptop freezer subwoofer ili waongezee pesa za mtaji na wafidie madeni, wakati huo mimi bado nilikuwa nimebebana na jamaa yangu mabibo hostel wote 3rd year.

Nilikaa nikafikiri maisha ya nyumbani sio mazuri na forex ndio nilijua itanitoa kimaisha japokuwa inachangamoto ndogondogo nikiangalia acc ya benki sina hata shilingi zaidi ya pesa ya kula maboom nimebaki nayo mawili nikasema nijibane hiyopesa niichanganye ifike milioni moja nitrade kwa uangalifu labda itanitoa maana niliamini million 1 inakaribia kwenye dola 500 .

Asee sijui ilikuwa ni bahati maana nilichanganya zote nikatrade nikapata kama dola 2600 ndani ya kama wiki 3 maana nilikuwa nafungua tu order na risk management nilikuwa sifanyi vizuri ,nilitoa dola 1300 kama million 3 hivi nikaenda riverside nikapanga chumba self 100000 per month ndio napoka mpaka sasa ,kwa miezi sita nikanunua kitanda godoro, nikanunua TV 500k, feni, gesi, meza na viti, subwoofer,Friji getto likajaaa .

Kwenye Trading acc nilibaki na dola 1300 nikasema hii siwezi poteza nitakuwa na trade natoa pesa kidogo kidogo hata dola 50 per day ambayo ni zaidi ya 100k nikaona maisha nimeyapatia sisumbuki kutafuta kazi nikutrade full time .nikawa nikiingia humu jamii forum natafuta ule uzi wa magari mazuri naangalia nikijua anytime navuta mkoko.

Daa baada ya kumaliza chuo nikawa mimi na soko ,soko na mimi nilijitahidi nikapandisha acc mpaka dola 1600

Asee siku ya mkosi ilivyofika ilikuwa ni kwenye muda wa saa 1 1 jion kulikuwa na newz ya gbp nimeingia na kama lotsize ya 1 forex trader mnanielewa vizuri soko lilienda agaist na mimi nikajikuta naongeza tena lot ya 1 huwezi amini pesa yote ilichomeka sikubaki hata na Mia kwenye acc

Nilihisi kuchanganyikiwa na ukubwa wote nilionao nililia kama mtoto mdogo siku pata usingizi siku nzima huku lawama zote nikimtupia mungu kwa nini ameruhusu pesa yote zaidi ya 3.7m kupotea ndani ya masaa machache.

Pesa niliokuwa nimebakinayo mpesa ilikuwa laki 4 kwa kile kipigo niliogopa kurudisha hiyo pesa kwenye forex kwani ilikuwa haifika hata dola 200 nikaanza kujiuliza nitaishi vipi hapa town na sina mtu hata wakuomba sh 100 . Nikaanza kuona simu za mama nazikwepa kwani nilikuwa nimezoea kumtumia pesa nashindwa akiniomba nitafanyaje.

Baasi nikatafuta rafiki yangu alikuwa anauza karoti ilala boma kwenye meza najua wenyeji wapale wanaelewa vizuri nikwamwabia anitafutie eneo kweli akaniambia per day meza unalipia 1000 na ushuru sasa mwenye meza anataka 60k ya miezi miwili nikasema poah ,nikampatia jamaa yangu pesa .

Akaniambia mwenye eneo amesema mkataba wa mtu anaetakiwa kuondoka unaisha baada ya siku 3. zikifika nikaanze biashara nikaenda kununua mzani kkoo wa kupimia 80k daa nilisubiria eneo jamaa aliekuwa anatakiwa kunipisha haondoki nikawa nimetapeliwa hivyo. Jamaa yangu kwa kuona hivyo akaniambia twende tukashitaki polisi turudishiwe pesa yetu.

Nikafikiria pesa niliyopoteza 3.7m kwa 60k nikaamua nipotezeee ,yule jamaa yangu akahisi labda anamakosa akaniambia kwenye meza yake niwe nachukua mzigo tunachanganya nikakubali lakini profit perday ilikuwa tunapata kama 15k nikaona namzibia jamaa riziki yake nikamwabia nimepata kazi mahali nikaondoka na mzani nikamuachia.

Nikarudi kukaa geto mpesa nikawa nimebaki na 170000 nikasema nizunguke hata kwenye karakana za furniture labda naweza kupata kazi huku nikijifunza wapi ,viwanda vya matofali unakutana na vibarua tu wanapiga kazi.

Nikahisi kukata tamaa nikatafuta kila njia ikashindikana nikasema nifanyeje nikapata wazo nijaribu kufanya betting kwani kipindi cha nyuma nilikuwa nafanya ndani ya wiki moja nikawa nimepoteza pesa yote hata pesa ya kula nikakosa ikabidi nimfate yule jamaa wa ilala nikamwabia kazi imebuma anipatie 30k nimuachie ule mzani akanipatia nikanunua msosi geto.

Huwa sina tabia ya kuuza vitu hovyo lakini nilitafuta mteja nikauza friji kwa bei ya hasara kama 300k hata miezi mitatu ilikuwa haija maliza, nikaendelea kubet .kila nilipikuwa naendelea kubet ndio pesa ilivyokuwa inazidi kupotea kila siku kuliwa tu asee asikwambie mtu betting sio kazi ya kutegemea inaweza kukuaibisha muda wowote.

Mwezi uliopita kwenye tarehe 20s nikafuma mikeka mitatu siku moja yote nikala zaidi ya 8m siku hiyo siku lala kwa furaha nikiwithdraw kama 7m nikawa nazo getto nimetunza nilibakiza 1m nikabet tena yote nikala 1.5m .wiki ikiyopita nikabet 500k nikala 2.6m jumla nikawa na kwenye acc na 3.6m .
Juzi na Jana nimebet nikapoteza 1m nimeona nitoe 2.6m nichanganye na ile 7m iwe 9.6m.

Nimeona kwa hiki kiasi cha 9.6m najua humu kunawataalam wa biashara wanaweza kunisaidia kunipatia wazo ama ushauri nifanye biashara ipi maana mimi nilikuwa na wazo nifungue kaduka niwe nauza vinywaji vinywaji vikali nichanganyanye na soft drink. Ama nitafute sehemu niuze hata nafaka ila mtaji ndio sijui unahitajika shilingi ngapi.

Note biashara ambayo nimewahi kufanya tofauti na hizo kamali hapo juu ni ufugaki kuku tena zamani sana huko j4.

Nitashukuru sana kwa mchango wako wowote ule utakao utoa maana umri unasogea na majukumu yanazidi kuongezeka.


Sent using Jamii Forums mobile app
weka hadi hiyo pesa vizuri hadi miezi miwili ijayo halafu nunua mazao hasa yale yasiyo haribika haraka na soko lake liko juu kila wakati .
 
#1. Swala sio mtaji katika scalping, Waweza ukawa na $100 na ukafanya vyema na pia waweza kuwa na $1000 ukashindwa kufanya vyema.

#2. Swala ni Entry sahihi, exit sahihi na kwa wakati sahihi katika Trading session sehihi husika.

Hii namba #2 ndio hutofautisha profitable trader na looser

#3. Imbalance ya pair husika kati ya seller na buyer , - Mfano hapa chini utaona USDCHF (Sell Scalping) iko vyema zaidi, pamoja na EURUSD ( Buy scalping )
View attachment 1610771
View attachment 1610780
---
Nina hakika point namba tatu hujanielewa kabisa.

Mfano hai: Scalping kwa 0.1 [ 5m TF ]
View attachment 1610787Hii biashara nzuri lakini inahitaji maarifa,hekima na busara.Binafsi nimesoma nimeijua hii biashara miaka 10 iliyopita na terminology nyingi nazijua lakini kuna tofauati kubwa kati ya kufanya forex trading na kufanya stock trading.Forex trading ni kamali fulani ya hali ya juu na wansema weka pesa ambayo uko tayari kuipoteza,na usiwe na mategemeo makubwa sana au tamaa unapofanya maana unaweza kupata mshtuko mkubwa pale unapopata hasara au faida.Kwa kifupi inahitaji kucheza kwa umakini mkubwa sana.Stocks trading kidogo rahisi maana unaangalia mwelekeo wa stocks husika (mfano Gold) dakika kadhaa zilizopita halafu unatabiri mwelekeo wake dakika zijazo unakula pesa.
 
Kubeti nakushauri usiache uzuri mtaji unao betia mtaji mkubwa kama 200k na kuendelea nilikuwa na mtaji wa 100k wa kubetia aisee kwa week mbili tu nilisha mla muhindi 4M[emoji23][emoji23][emoji23] ila mpaka sasa sijui nini kimenotokea nime liwa pesa yote sasa nina 1200M tu
 
Kubeti nakushauri usiache uzuri mtaji unao betia mtaji mkubwa kama 200k na kuendelea nilikuwa na mtaji wa 100k wa kubetia aisee kwa week mbili tu nilisha mla muhindi 4M[emoji23][emoji23][emoji23] ila mpaka sasa sijui nini kimenotokea nime liwa pesa yote sasa nina 1200M tu
Hahaha pole chief ulikuwa unacheza option gani?
 
Back
Top Bottom